Thibitisha kama ni hadithi kweli
Kwanza, Biblia imejaa utata wa kimantiki (logical contradictions) nyingi sana kitu ambacho unaona wazi hizi ni hadithi zilizotungwa na watu tu, kufurahisha na kuburudisha watu tu.
Nitakupa mfano wa utata huu wa kimantiki.
Hii hapa juu ni attachment inayo onyesha utata wa kimantiki uliopo kwenye kitabu cha Mwanzo cha Biblia.
Ukisoma Mwanzo 1:3-5, Inasema siku ya kwanza Mungu aliumba mwanga, kisha akatenganisha mchana(mwanga) na Usiku(darkness).
Hapohapo kwenye kitabu hichohicho cha Mwanzo, ile sura ya kwanza mstari wa 14-19, Inasema
Jua (ambalo ndio mwanga wenyewe, ambalo hutenganisha mchana na usiku🌓) liliumbwa siku ya nne!
Hapa tayari unaona kabisa kuna utata wa kimantiki uliopo kati ya Mwanzo 1:3-5 na Mwanzo 1:14-19.
Kwa sababu kama mwanga uliumbwa siku ya kwanza, iweje tena JUA☀️ ambalo ndio hutoa mwanga wenyewe, lije kuumbwa siku ya nne?
Ni EITHER Jua ☀️ liliumbwa siku ya nne na mwanga hauku umbwa siku ya kwanza. Kukawa giza hadi siku ya nne.
AU Mwanga uliumbwa siku ya kwanza, Na jua halikuumbwa siku ya nne.
Huu ni mfano mmojawapo wa logical contradictions katika Biblia. Na kuna zaidi ya logical contradictions 100 kwenye Biblia.
Sasa haiwezekani kitabu ambacho kinadaiwa kwamba ni cha Mungu mkamilifu na mwenye kujua yote, kiwe na utata wa kimantiki. Kwa sababu Mungu mkamilifu mwenye kujua yote hawezi kuwa na kitabu chenye utata wa kumuelezea yeye!
Ni dhahiri kwamba kitabu hichi cha Biblia si cha Mungu bali cha wanadamu wasio wakamilifu ndio maana kimejaa utata wa kimantiki unaotokana na binadamu wenye mapungufu.
I hope umeelewa
Bushmamy
Pia link hii hapa ina logical contradictions ambazo zipo kwenye Biblia.
View: https://www.scribd.com/document/399098454/Bible-Inconsistencies-Bible-Contradictions-Part-1
50 Contradictions in the Bible: The Most Shocking Differences
50 Contradictions in the Bible: The Biggest, Most Shocking Differences