Hayo mambo ya kuhusu watu kujiweka utupu yanategemea, mila na jadi na mtu alipotokea. Wengi wa wakosa maadili utakuta wametokea kwenye familia zilizoacha kujifunza na kufunza vizazi vyao maadili kutokana na mafundisho ya dini.
AlhamduliLlah, Uislam unahimiza stara popote tulipo. Nasisitiza, tusichanganye Uislam na Muislam.
Ninewaona Waislam wengi ambao utamkuta katupia khanga moja tu mbele ya watu na hata hajali kabisa, kinyume kabisa na mafundisho ya Uislam.
Hali kadhalika kwa wasio Waislam.
Tatizo la kutokuwa na maadili ni watu kuwacha kusoma na kusomesha dini watoto zetu.
Hutokuta upuuzi wa maadili kwenye familia zinazofata na kushika mafundisho ya dini.
Tunaishi kutokana nanayoyaona kwenye nedia za kimagharibi, ambayo yote uliberali (ushetani).
Hatujachelewa kurudi kwenye maadili kwa kufata mafundisho ya dini. Tukumbushane mara kwa mara, asaa tutamuokoa japo mmoja.