Dkt. Magufuli na mkewe, Janeth Magufuli wamepiga kura kituo cha Idara ya maji kilichopo Ikulu, Chamwino.
MWANDISHI: Unazungumziaje taratibu za upigaji kura katika kituo chako? Mambo yanavyokwenda kwa ujumla, umeridhika?
DKT. MAGUFULI: Napenda niwapongeze watanzania wote kwa kuiona hii siku ya leo ambayo ni siku muhimu sana katika kukuza demokrasia katika Taifa letu, napenda niwapongeze pia wasimamizi wa uchaguzi katika kituo chetu cha hapa Chamwino ambacho mimi nimepiga kura pamoja na mke wangu, maandalizi yalikuwa mazuri, mstari wapiga kura wamejitokeza wengi kwa hiyo nawapongeza kwa usimamizi mzuri ambao unaendelea kufanyika hapa.
Wito wangu kwa Watanzania, tujitokeze kwa wingi katika siku hii ya leo kwenda kupiga kura, twende tukapige kura kwa ajili ya maamuzi ambayo kila mmoja atakuwa nayo katika moyo wake.
Lakini napenda nisisistize amani lazima tuendelee kuitunza kama Taifa kwa sababu kuna maisha hata baada ya uchaguzi, Mungu awabariki wapiga kura wote, Mungu aibariki Tanzania. Asanteni sana watanzania, nami nimeshapiga na kidole changu hiki hapa(Anakionesha), mke wangu nae ameshapiga, tumetimiza wajibu wetu wa kuchagua.