Uchaguzi 2020 Yaliyojiri sehemu mbalimbali Tanzania katika zoezi la upigaji kura za Rais - Oktoba 28, 2020
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ADA-TADEA, John Shibuda amegoma kupiga kura hadi pale mawakala wake katika Wilaya ya Maswa watakaporuhusiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura baada ya kuzuiliwa kwa kile kilichoelezwa hawana barua za utambuzi.
 
-Mgombea Urais wa JMT kupitia Chadema Mhe. Tundu Lissu akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar es salaam tayari kuelekea Mkoani Singida kushikiri zoezi la upigaji kura.
20201028_095850.jpg
 
Sijapenda kabisa,Jpm angeingia moja kwa moja tu ndani na akapiga kura na watu wake,ila hiki kilichofanyika amepanga mstari ila watu waliombele yake wanaingia ndani na kupita tu wakiambiwa na yule afisa usalama ndani piteni mtarudi baada ya Rais kupiga wakati tayari wamehakiki si sawa kabisa,nadhani hawajui kama wako Live.......

Najiuliza wale waliopita tayari wamewekewa tick ya kuwa wameshaingia ndani,watarudi vp kupiga tena kura?
 
Dkt. Magufuli na mkewe, Janeth Magufuli wamepiga kura kituo cha Idara ya maji kilichopo Ikulu, Chamwino.

MWANDISHI: Unazungumziaje taratibu za upigaji kura katika kituo chako? Mambo yanavyokwenda kwa ujumla, umeridhika?

DKT. MAGUFULI: Napenda niwapongeze watanzania wote kwa kuiona hii siku ya leo ambayo ni siku muhimu sana katika kukuza demokrasia katika Taifa letu, napenda niwapongeze pia wasimamizi wa uchaguzi katika kituo chetu cha hapa Chamwino ambacho mimi nimepiga kura pamoja na mke wangu, maandalizi yalikuwa mazuri, mstari wapiga kura wamejitokeza wengi kwa hiyo nawapongeza kwa usimamizi mzuri ambao unaendelea kufanyika hapa.

Wito wangu kwa Watanzania, tujitokeze kwa wingi katika siku hii ya leo kwenda kupiga kura, twende tukapige kura kwa ajili ya maamuzi ambayo kila mmoja atakuwa nayo katika moyo wake.

Lakini napenda nisisistize amani lazima tuendelee kuitunza kama Taifa kwa sababu kuna maisha hata baada ya uchaguzi, Mungu awabariki wapiga kura wote, Mungu aibariki Tanzania. Asanteni sana watanzania, nami nimeshapiga na kidole changu hiki hapa(Anakionesha), mke wangu nae ameshapiga, tumetimiza wajibu wetu wa kuchagua.

Magufuli.jpg
 
Huku nilikopigia Kura, nimepanga foleni na wazee miaka 45 na kwendelea

Sifahamu Kwa nini vijana mpaka muda huu hawaonekani vituoni

Unapigia kura kwenye kituo cha kulelea wazee halafu unataka uone vijana? Baba yangu ana miaka 57 lakini ni cdm damu, na kura yake ni kwa Lisu. Kwa taarifa yako Magufuli ameua ari ya watu kupiga kura. Uchaguzi huu kufikisha hata wapiga kura 15m ni muujiza.
 
Niliamka mapema na mke wangu kwenda kituoni kupiga kura. Saa 7.05 nilikuwa kituoni.

Mke wangu hajaweza kupiga kura kwakuwa jina lake halikuonekana kabisa pale kwenye daftari. Na walikuwepo wengi ambao majina yao hayakuwepo mahala ambapo yalitakiwa yawepo. Na yeye ni mfanyakazi amelazimika kuwahi kazini.

Naomba tume itoe tamko itatue hizi changamoto mapema kadiri inavyowezana kabla hatujafika mchana.
 
Hakujiandikisha
ƙwani alipaswa ƙujianɗiƙisha upƴa??? ...si alianɗikisha ƙwaajili ƴa 2015 ƙwahiƴo hapo alicho taƙiwa ni ƙuhaƙiƙi tu iƙiwa jina laƙe lipo ƙwenƴe ɗaftari la mpiga ƙura then atajua na sehemu ƴa ƙupigia ƙura!!!
 
Nilidhani unaongelea utabiri kuhusu Tanzania kumbe umehakisi, but huyo chahali hana lolote huyo dogo ni sawa na ccm, yaani anapenda kusifiwa tu ukimpinga anakublock, it shows bado kijana mdogo hajakuwa kifikra.
 
Back
Top Bottom