Uchaguzi 2020 Yaliyojiri sehemu mbalimbali Tanzania katika zoezi la upigaji kura za Rais - Oktoba 28, 2020
Naam.

Kipigo cha mbwa. Hicho ndo wanachokipata hawa so called ‘wapinzani’.

Kwa kweli wala siwaonei huruma. Maana kinachowatokea ndicho wanachokistahili.

Labda baada ya hapa ndo tunaweza kupata upinzani wa kweli kuliko hawa waganga njaa.

Hawa watu waliugeuza huo upinzani kuwa ‘a hustle’ na kusahau kabisa malengo na madhumuni yao.

Ukiwapa ushauri wa kujenga, wanakudharau. Wanakuona wewe ni zuzu au sijui ni zwazwa.

Haya sasa, siku ya siku imefika, imepita, na yale ambayo baadhi yetu tulikuwa tukiwaonya kuwa yatatokea, yameanza kutimia.

Sasa eti wameanza kulialia.

Wanalialia nini sasa? Kwani hawakujua ambacho kingetokea?

Mimi siwaonei huruma hata kidogo.

They deserve everything that’s happening to them and then some.

Now, maybe this will be their time of reckoning.

But, with this current bunch, I don’t have faith in it.

Let me repeat myself again [I know, I sound like a broken record here but oh well]; if you always do what you’ve always done, you’ll always get what you’ve always got.

Read and weep.

Umeongea ukweli mtupu, walijasahau kama walivyokuaga wamejisahau CCM zamani. Hawakujua nini sasa na tulikua tunaongea hayo hayo kila siku

 
Aende zake tu akaishi Ubelgiji...watanzania bado wanahitaji kichapo cha miaka mitano tena wajitambue...Nchi ikiwekewa vikwazo ndipo tutajua kuwa kumbe tamu huwa ni chungu...Amefanya kwa nafasi yake...Big up!!!!
Kuiba mmeiba
 
Lissu tumpe pongezi jamani. Amepata kura 2 katika jimbo la Gairo. Kajitahidi sana kwa kweli.
TUNDU LISSU UPO FREE TUNAOMBA UKAPANDE MWENDO KASI TENA UKANUNU KADETI TENA PIA UPITE MLIMANI CITY NAKUHAKIKISHIA SAFARI HII UTAZOMEWAA ........HUKUTUJUA WAZELENDO TUMEKUNYOOOSHA ETI WATANZANIA WAKADAI HAKI YAO 🤣😂😂😂😂😂😂😂🤣😂😂 Ila wewe kijana Lissu nakukubali ni CCM mojaa hahaha umefanya kazi tuliyokutuma sasa unawaagiza wakale kichapo
 
Lissu, CHADEMA wenzako wamekuangusha! Umefanya ulichoweza lakini cowards hawakuwa hata na uwezo wa kuongea na dunia mara kwa mara kupinga dhulma za wazi. Embu ona hata ballot papers hazijulikaniki zimepritiwa wapi! Uchaguzi gani huo!
Hamna lolote mtafanya! Kesho business as usual.

CHADEMA leadership ni cowards! Mbowe limejificha huko! Eti mwamba tuvushe! Pimbi tu wewe! Umejificha Hai kipindi karibu chote cha campaign! Haya sasa wamekudhulumu yaani!
🤣😂😂😂😂😂😂😂🤣😂😂mwamba tuvushe
 
Uchaguzi ulikuwa wa huru na haki, wananchi kwa utashi wao wamewakataa upinzani walaghai, Lisu alikuwa ananadi matusi badala ya sera, alikuwa anatafuta kura za huruma. Wananchi wameamua kuchagua maendeleo, hakuna cha kuwekewa vikwazo wala nini. Nadhani, kwa sasa upinzani ujipange, ujitafakari walipojikwaa ili 2025 waje wakiwa wamejipanga kwa sera mbadala ya kuiondoa CCM!
Kama ilikiwa Huru na haki kwa nini baadhi ya vituo matokeo ya kura na Idadi ya waliopiga kura vinatofautiana.
 
MiMi ni CCM haswaa ila NAKUSHAURI TUNDU LISSU ANZISHA CHAMA ILA PIGA CHINI HAO KINA MBOWE KINA MNYIKA KINA ZITTO, SIJUI HECHE ,KINA MDEE KINA BULAYA PIGA CHINIII....MIMI NITAKUUNGA MKONO UTALETA UPINZANI WA TIJA NA UTAKUWA UMEKOMAA KISIASA ACHANA NA CAHADEMA ...ILA UKITAKA MSAADA WANGUU ACHE MATUZI DHARAU NA KEBEHI KWA VIONGOZI WENZAKO..PIA UTUBUVKWA WATANZANIA NA UWEKE MASLAHI YA WATANZANIA MMBELE
 
Tuacheni propaganda za kutafuta scapegoats za kushindwa na kuchafua jina la nchi kwa sababu za kipuuzi.

Nashindwa kuelewa chama kisichokuwa na grassroots kudai kuwa kinaibiwa kura! Mwaka 1995 mimi nikiwa NCCR-mageuzi tulihamasika sana pale Dar tukajua Mrema atachukua nchi, lakini tukasahau kuwa tulikuwa maarufu Dara na miji michache tu kwani hatukuwa na network kuzunguka nchi yote.

CHADEMA imerudia makosa hayo ya kudhani kuwa ushabiki wa kwenye mitandao ndio kura za nchi nzima; ng'o!

Ni kweli! grassroot ni ile ya OCD wa Jeshi la Polisi Tanzania kutangaza matokeo wiki mbili kabla ya kura
Kura kwenye mabegi, zote za CCM halafu zina mhuri wa NEC na kila kitu. grassroot

Kwa hili Wapinzani waliambiwa hawakusikia
1. Nikupe gari na mshahara halafu umtangaze mpinzani
2. Tutafuta upinzani nchini
3. OCD na Jeshi la Polisi, NEC, Msajili, TCRA , TBC halafu CCM washindwe, ningewaona CCM wapuuzi

Kuna kitu kimoja watu hawakioni. Miaka 5 ya kampeni peke yao, rasilimali za nchi, kuwafunga wapinzani lakini chuki iliyopo dhidi yao kitu cha kutafakari sana

Unaona dhahiri kuwa wananchi hawajali ndege wala madaraja, wamejawa chuki na wanaichukia na kuwachukia to the core. Badala ya kushangilia wizi, wangekaa kitako na kujiuliza !

Wakae chini wajitahmini, wajiulize na watakafakari kwanini Inachukiwa na wanachukiwa kiasi hicho
 
Haya mnayo yaona leo ni matokeo ya mtu mmoja Mbowe ya kumleta Lowasa Ukawa,hili lilikuwa bonge la kosa ambalo kwa mtu makini kabisa kwa kosa lile alitakiwa ajihudhuru, ila Mbowe anadunda, untouchable, ukimkosoa humu watu wanakushambulia.
images (23).jpeg


Nilikiwa mwanasiasa kindakindaki wa CHADEMA chuo kuanzia 2009,ila baada ya Lowasa kuingia nilikaa pembeni,nikabezwa,nikapondwa baada ya UKAWA kupata viti vyingi bungeni,ila baada ya wabunge kuanza kurudi CCM ,kuna watu niliwaambia 2020 hali itakuwa mbaya sana na leo tuna yaona.

CHADEMA mlivyo mleta Lowasa UKAWA na kujiamini kwamba mpo imara,kumbe mliacha nyumba yenu mliyokuwa mnaijenga kidogo kidogo kwenye mwamba na kwenda kujenga kwenye mchanga kisa tu kuna urahisi.Sasa angalieni leo mnayo yapata ni haki yenu hamjaibiwa hata kura moja.

CHADEMA mkitaka kusimama tena mnabidi muanze upya mfumue chama chote na mkijenge CHAMA kupitia vijana wenu na watu wenu mlio waandaa nyinyi na si kunyakua wanasiasa kutoka CCM na mnatakiwa kiwaamini watu wenu.

MMEVUNA MLICHO KIPANDA.
Acha kutafuta sababu isiyo kwepo, wakati wa Slaa uongozi wa Mkapa na kikwete angalau ulikuwa na utu na kujali demokrasi na hiyo ndiyo unaona kama walikuwa makini. Uongozi wa sasa hauna utu Umejaa majivuni usiojali utu wa watu wake! kiongozi mkuu anajiona yeye ndiye pekee na hakuna kama yeye. Mtu kama MBOYE ni mangapi yamempata? angekuwa legelege kitambo sana angeunga juhudi.
 
Mitandao itakuwa inapatikana? Maana hii JF yenyewe lazima uisearch haiji moja Kwa moja.
Tindo nakusalimia ndugu yangu. Kampeni yako ya kuzuia watu wasijiandikishe naona imezaa matunda.
 
Ni kweli! grassroot ni ile ya OCD wa Jeshi la Polisi Tanzania kutangaza matokeo wiki mbili kabla ya kura
Kura kwenye mabegi, zote za CCM halafu zina mhuri wa NEC na kila kitu. grassroot

Kwa hili Wapinzani waliambiwa hawakusikia
1. Nikupe gari na mshahara halafu umtangaze mpinzani
2. Tutafuta upinzani nchini
3. OCD na Jeshi la Polisi, NEC, Msajili, TCRA , TBC halafu CCM washindwe, ningewaona CCM wapuuzi

Kuna kitu kimoja watu hawakioni. Miaka 5 ya kampeni peke yao, rasilimali za nchi, kuwafunga wapinzani lakini chuki iliyopo dhidi yao kitu cha kutafakari sana

Unaona dhahiri kuwa wananchi hawajali ndege wala madaraja, wamejawa chuki na wanaichukia na kuwachukia to the core. Badala ya kushangilia wizi, wangekaa kitako na kujiuliza !

Wakae chini wajitahmini, wajiulize na watakafakari kwanini Inachukiwa na wanachukiwa kiasi hicho
Chama hakina viongozi wa mashina unadhani kitapata wapi wapiga kura; hii ya kulalamikia polisi na NEC ni utoto sana. Unamkuta mtu anvunja sheria hadharani kwenye vituo vya uchaguzi halafu akishughulikiwana vyombo vya sheria analalamika.
 
Kwa namna yoyote, uchaguzi uliofanyika jana ni kilele cha kiburi cha hali ya juu cha watawala kuonyesha dharau mbele ya wananchi.

Watawala kwa kutumia TISS, NEC, Polisi, Jeshi wamefanya kila aina ya uhuni dhidi ya wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Wamepiga risasi na kuua watu Zanzibar, Wameondoa mawakala wa upinzani kwenye vituo vya kupigia kura, kabla ya hapo tangu kipindi cha kampeni wamevamia wagombea wa vyama vya upinzani na kuharibu mali zao na kuwaharass kwa kila namna, Wameingiza kura feki kibao katika sehemu mbalimbali za nchi.

Sasa ndugu zangu, kuna uchaguzi hapo?

Mimi nivipongeza vyama vya upinzani, Vimetimiza wajibu wao wa kuwa sauti mbadala katika nchi kwa tabu, mauivu na machungu mengi.

Kushiriki kwenu kwa tabu nyingi, kumesaidia kutuonyesha na kuuonyesha uimwengu aina ya utawala wa kidhalimu tulio nao

Nawaonea huruma Polisi wetu, Uslama wa Taifa na hata Wanajeshi wanadhani kwa kuwalinda watawala na udhalimu wao basi wao maisha yao yatakuwa bora. Masikini laiti wangalijua, Wanalinda mfumo wa kidhalimu utakaowaumiza hata wao wakiwa waevua hayo magwanda na bunduki zao zibazowafanya wajihisi wako juu mbinguni.

Ndugu zangu, CCM kamwe haitong'oja kwa vikaratasi hivi viitwavyo kura katika set up tuliyonayo hivi sasa. The Next step ya action ya vyama vya upinzani, mwananchi mmojammoja, taasis binafsi, lazima wajue kuwa CCM ilishakataliwa na wananchi atleast kuanzia mwaka 2010, Kilichofanyika kuanzia hapo ni uhuni, ghiliba, ulaghai, uonevu, hongo. Kwa hiyo uchaguzi huu uwe ni Jaribio la kuhitimisha(conclusive test) kuwa kamwe KATIKA MFUMO HUU TULIONAO, CCM KAMWE HAWATOKUBALI KUONDOKA KWA KURA. Wapanga strategy kwa ajili ya Tanzania mpya lazima mlitilie maanani hili jambo!

Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania, puuzeni huu ujinga wanaosema ni uchaguzi umefanyika jana, Ule siyo uchaguzi ni uhuni mtupu!
Malalamiko ni yale yale miaka nenda miaka rudi.

1. Kama yote haya yanajulikana, kwa nini wapinzani wanakubali kushiriki chaguzi hizi? Tena bila kuungana? Ni tamaa ya ruzuku au ni nini? Wapinzani wote mngegomea chaguzi hizi mpaka pawepo na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Ingefika mahali hata jumuia ya Kimataifa ingewaelewa na mwishowe katiba ya Warioba ingepitishwa tu.

2. Hebu tuchukulie kuwa unayosema yote ni kweli, nini sasa kifanyike hasa ukizingatia kuwa siasa siyo mchezo wa kulia lia kila mwaka na kutafuta kuhurumiwa?
 
Matokeo yameendelea kutangazwa na kila kunapotangazwa ushindi unakwenda kwa Madiwani wa CCM na Wabunge wa CCM. Tofauti ya Kura kati ya wagombea wa CCM na Wapinzani ni kubwa sana kiasi kwamba hauwezi kusikia kuwa yapo malalamiko kuwa wagombea wa CCM wameiba kura ama wameshinda kwa ujanja ujanja.

Iliwahi kusemwa kuwa Uchaguzi ni akili, maarifa na mipango na kwamba CCM kama Chama kilijipanga katika kila hatua ya kuelekea ushindi huu ambao umeendelea kutangazwa kwa wanaCCM, wakati CCM wakijiandaa na kufanya ground work ya kuhakikisha wanachama wao wanajiandikisha, wanakuwa na vitambulisho na wanapiga kura.

Wakati hayo yakiendelea CUF walikuwa na mgogoro uliopelekea kuvunjika kwa Chama chao na Maalim Kujiunga ACT Wazalendo ambayo nayo ilikuwa na mgogoro wa kiuongozi na kusababisha wanachama wake na viongozi wake wengi kukihama chama hicho na kujiunga na CCM hali ya kuwa CHADEMA ikiongozwa kuhamwa na wanachama wake na Viongozi wake hasa wabunge kutokana na matatizo ya kiuongozi yaliyokikumba Chama hicho yaliyotokana na Uchaguzi wa Ndani wa Chama hicho na hasa NAFASI YA UENYEKITI wa Chama.

Ninachokisema ni kuwa Wapinzani wanayo nafasi ya kujifunza na hasa wakiwa tayari kufanya hivyo, walipofanya uamuzi wa kugomea uchaguzi wa Serikali ya Mitaa walikuwa wanapaswa kutambua kuwa walikuwa wanajivunja miguu na kuwafanya washindwe kusimama tena.
Bila katiba mpya wapinzani hata wafanyeje hawataweza kuiondoa CCM madarakani

Full stop !!!
 
Kama ilikiwa Huru na haki kwa nini baadhi ya vituo matokeo ya kura na Idadi ya waliopiga kura vinatofautiana.
Ni changamoto za kawaida, makosa madogomdogo kutokea kwa nchi kubwa kama hii. Hivi kwa akili tu ya kawaida ulitegemea Lisu kushinda huu uchaguzi? Kwa kuonewa huruma kwamba kapigwa risasi? Mkakati uliotumiwa na wapinzani mwaka huu ni dhaifu sana, bora hata ule wa 2015 ambapo upinzani uliungana na kutengeneza UKAWA. Ajabu ni kuwa kadri siku zinavyokwenda upinzani wenyewe unadorora, unazidi kupotea. Then wategemee huruma kwa wananchi, wakati huo CCM imezidi kujiimarisha. Hizi ni ndoto za alinacha. Siasa siyo matukio, ni mkakati wa hali huu, siyo blah blah!
 
Back
Top Bottom