Umeongea ukweli mtupu, walijasahau kama walivyokuaga wamejisahau CCM zamani. Hawakujua nini sasa na tulikua tunaongea hayo hayo kila siku

 
Aende zake tu akaishi Ubelgiji...watanzania bado wanahitaji kichapo cha miaka mitano tena wajitambue...Nchi ikiwekewa vikwazo ndipo tutajua kuwa kumbe tamu huwa ni chungu...Amefanya kwa nafasi yake...Big up!!!!
Kuiba mmeiba
 
Lissu tumpe pongezi jamani. Amepata kura 2 katika jimbo la Gairo. Kajitahidi sana kwa kweli.
TUNDU LISSU UPO FREE TUNAOMBA UKAPANDE MWENDO KASI TENA UKANUNU KADETI TENA PIA UPITE MLIMANI CITY NAKUHAKIKISHIA SAFARI HII UTAZOMEWAA ........HUKUTUJUA WAZELENDO TUMEKUNYOOOSHA ETI WATANZANIA WAKADAI HAKI YAO 🤣😂😂😂😂😂😂😂🤣😂😂 Ila wewe kijana Lissu nakukubali ni CCM mojaa hahaha umefanya kazi tuliyokutuma sasa unawaagiza wakale kichapo
 
🤣😂😂😂😂😂😂😂🤣😂😂mwamba tuvushe
 
Kama ilikiwa Huru na haki kwa nini baadhi ya vituo matokeo ya kura na Idadi ya waliopiga kura vinatofautiana.
 
MiMi ni CCM haswaa ila NAKUSHAURI TUNDU LISSU ANZISHA CHAMA ILA PIGA CHINI HAO KINA MBOWE KINA MNYIKA KINA ZITTO, SIJUI HECHE ,KINA MDEE KINA BULAYA PIGA CHINIII....MIMI NITAKUUNGA MKONO UTALETA UPINZANI WA TIJA NA UTAKUWA UMEKOMAA KISIASA ACHANA NA CAHADEMA ...ILA UKITAKA MSAADA WANGUU ACHE MATUZI DHARAU NA KEBEHI KWA VIONGOZI WENZAKO..PIA UTUBUVKWA WATANZANIA NA UWEKE MASLAHI YA WATANZANIA MMBELE
 

Ni kweli! grassroot ni ile ya OCD wa Jeshi la Polisi Tanzania kutangaza matokeo wiki mbili kabla ya kura
Kura kwenye mabegi, zote za CCM halafu zina mhuri wa NEC na kila kitu. grassroot

Kwa hili Wapinzani waliambiwa hawakusikia
1. Nikupe gari na mshahara halafu umtangaze mpinzani
2. Tutafuta upinzani nchini
3. OCD na Jeshi la Polisi, NEC, Msajili, TCRA , TBC halafu CCM washindwe, ningewaona CCM wapuuzi

Kuna kitu kimoja watu hawakioni. Miaka 5 ya kampeni peke yao, rasilimali za nchi, kuwafunga wapinzani lakini chuki iliyopo dhidi yao kitu cha kutafakari sana

Unaona dhahiri kuwa wananchi hawajali ndege wala madaraja, wamejawa chuki na wanaichukia na kuwachukia to the core. Badala ya kushangilia wizi, wangekaa kitako na kujiuliza !

Wakae chini wajitahmini, wajiulize na watakafakari kwanini Inachukiwa na wanachukiwa kiasi hicho
 
Acha kutafuta sababu isiyo kwepo, wakati wa Slaa uongozi wa Mkapa na kikwete angalau ulikuwa na utu na kujali demokrasi na hiyo ndiyo unaona kama walikuwa makini. Uongozi wa sasa hauna utu Umejaa majivuni usiojali utu wa watu wake! kiongozi mkuu anajiona yeye ndiye pekee na hakuna kama yeye. Mtu kama MBOYE ni mangapi yamempata? angekuwa legelege kitambo sana angeunga juhudi.
 
Mitandao itakuwa inapatikana? Maana hii JF yenyewe lazima uisearch haiji moja Kwa moja.
Tindo nakusalimia ndugu yangu. Kampeni yako ya kuzuia watu wasijiandikishe naona imezaa matunda.
 
Chama hakina viongozi wa mashina unadhani kitapata wapi wapiga kura; hii ya kulalamikia polisi na NEC ni utoto sana. Unamkuta mtu anvunja sheria hadharani kwenye vituo vya uchaguzi halafu akishughulikiwana vyombo vya sheria analalamika.
 
Malalamiko ni yale yale miaka nenda miaka rudi.

1. Kama yote haya yanajulikana, kwa nini wapinzani wanakubali kushiriki chaguzi hizi? Tena bila kuungana? Ni tamaa ya ruzuku au ni nini? Wapinzani wote mngegomea chaguzi hizi mpaka pawepo na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Ingefika mahali hata jumuia ya Kimataifa ingewaelewa na mwishowe katiba ya Warioba ingepitishwa tu.

2. Hebu tuchukulie kuwa unayosema yote ni kweli, nini sasa kifanyike hasa ukizingatia kuwa siasa siyo mchezo wa kulia lia kila mwaka na kutafuta kuhurumiwa?
 
Bila katiba mpya wapinzani hata wafanyeje hawataweza kuiondoa CCM madarakani

Full stop !!!
 
Kama ilikiwa Huru na haki kwa nini baadhi ya vituo matokeo ya kura na Idadi ya waliopiga kura vinatofautiana.
Ni changamoto za kawaida, makosa madogomdogo kutokea kwa nchi kubwa kama hii. Hivi kwa akili tu ya kawaida ulitegemea Lisu kushinda huu uchaguzi? Kwa kuonewa huruma kwamba kapigwa risasi? Mkakati uliotumiwa na wapinzani mwaka huu ni dhaifu sana, bora hata ule wa 2015 ambapo upinzani uliungana na kutengeneza UKAWA. Ajabu ni kuwa kadri siku zinavyokwenda upinzani wenyewe unadorora, unazidi kupotea. Then wategemee huruma kwa wananchi, wakati huo CCM imezidi kujiimarisha. Hizi ni ndoto za alinacha. Siasa siyo matukio, ni mkakati wa hali huu, siyo blah blah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…