Uchaguzi 2020 Yaliyojiri sehemu mbalimbali Tanzania katika zoezi la upigaji kura za Rais - Oktoba 28, 2020
Mungu Baba ninatubu kwa dhambi zangu na taifa letu Tz, tuonee huruma, tujalie hekima na busara tukafanye wajibu wetu kupiga, kuhesabu, kutangaza matokeo kura itakayo leta HAKI na ustawi wa taifa letu.

Amina
 
Haya nendeni mkapige kura sasa then mrudi sio tumeongea wee kumng’oa dikteta jiwe alafu siku yenyewe kura hampigi. Mi nimeshangaa familia nzima wananiambia hawapigi sababu mshindi ashapangwa nikawaambia acheni ujinga, watanzania ambao wanakaa bila kupiga kura huku uwezo wanao wasije hata kulaumu wanachofanyiwa na hili tako.
Wahamasishe tu waende mkuu, kura zao ni za muhim sana.
 
Eti jina la Magufuli ndio la kwanza na la Lissu ndio la mwisho!

Mambo ya kitoto sana...
Hivyo ndivyo ballot ilivyo; majina yamepangwa kulingana na order ya kurudisha form. Magufuli alikuwa wa kwanza kurudisha forma wakati Lissu alikuwa wa mwisho kurudisha form.
 
Ni advantage kwa wote
Hii ina favour kwa Ccm maana kuna ambao hawajui hii paper ilivyo so kwa watakao kua na kapressure kidogo pale ndan wakifikir wanachukua mda mrefu, wakishuka mpak no 10. Wasipoiona Chadema wanaez piga kwa mwngine ili tu wasiipe Ccm. Na itakua loss kwa Chadema. Hii ndo technique wanadhan itawap afadhal, wameequailize kidog kuliweka mwsho kuondoa tafran na hata kukataliwa kwa ballots.
 
Bado maandalizi

Ni dk 7 ss
20201028_070606.jpg
 
Kusema ukweli kumtoa rais alie madarakani Ni jambo ngumu kidogo.
Walao ile 2015 ndio tungeweza kuzungumza hivi, lau tusubiri hio 2025 labda tunaweza kuongea lugha hii.

Muhimu mliojaliwa kupiga kura nendeni mkapige kura huku Mungu akiwa ndie mwongozo maana bila Mungu hakifanyiki chochote kilicho sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo hata ukimaliza kunya huwa Mungu unamwambia aje akutawaze?! Mungu amekupa utashi wa kuamua mabaya na mazuri. Mabaya ya Jiwe yanajulikana usisubiri Mungu akuonyeshe. Usiwe kipofu hivyo ukaambukiza upofu wengine.
 
Eti sababu ni kwamba Magufuli alirudisha fomu wa kwanza na Lissu wa mwisho. Utetezi usio na mashiko kabisa.
Lakini baada ya Lissu kurudisha kuna waliorudisha nyuma yake kama sikosei. Na ikumbukwe alirudisha mapema akawekwa bench muda mrefu. Na lengo lilikuwa si jema baadaye wakaona dunia itasimama ndiyo ikabidi zipokelewe.
 
Utujuze, niko hapa kwenye kituo cha kupigia kura,mapema kabisa nataka niweke historia ya mpiga kura wa kwanza kabisa kufanya maamuzi machachu na magumu
Haahaa kura Ina UZITO ule ule.
Hiyo Ni human nature.
Kuna watu wanapenda wawe wa kwanza kwenye KILA Jambo...that's Good
 
Tumesha sign petition ya Ngurumo, dunia ujue yanayo endelea Tanzania.
Kwahiyo dunia pia ndio itaingia kwenye maandamano incase Lissu akiporwa ushindi?

Hapo ndio tunapokosea Watanzania, jitetee mwenyewe usisubiri kutetewa na dunia. Mpaka hapa ni dhahiri Magufuli anarudi Ikulu na hakuna fyoko itakayofanyika na hiyo dunia itabaki busy na mambo yake.
 
Ila wamekosa plan, maana the opposite is true, sasa mtu ukimwambia akika kwenye karatasi jina la mwisho ndo uweke tik si sawa na ukimwambia jina la kwanza ndo uweke tik, hakuna tofauti, ni ujinga tu ambao watu wachache wanaona unawasaidia!
Uko vizuri
 
Kwahiyo dunia pia ndio itaingia kwenye maandamano incase Lissu akiporwa ushindi?

Hapo ndio tunapokosea Watanzania, jitetee mwenyewe usisubiri kutetewa na dunia. Mpaka hapa ni dhahiri Magufuli anarudi Ikulu na hakuna fyoko itakayofanyika na hiyo dunia itabaki busy na mambo yake.
Petition ikifikia sahihi 2,000 mhusika anapelekewa summons.
 
Eti jina la Magufuli ndio la kwanza na la Lissu ndio la mwisho!

Mambo ya kitoto sana.
yaani huyu ndugu yako akipata kura chini ya 90% atakuwa kafeli vibaya, uchaguzi huu kawekea upinzani hujuma kibao ukiacha ile kubebwa ya moja kwa moja kikatiba!

mabango yote nchi nzima, media zote, kufungia wenzie wasifanye mikutano kwa kivuli cha kamati ya maadili, mamlaka ya anga kuzuia TL kufanya baadhi ya mikutano, kivuko "kuharibika" kisa TL ashindwe kwenda mkutanoni visiwani ziwa victoria nk nk
 
Back
Top Bottom