Uchaguzi 2020 Yaliyojiri sehemu mbalimbali Tanzania katika zoezi la upigaji kura za Rais - Oktoba 28, 2020
Screenshot_20201028-074224_Chrome.jpg
 
Umati wa vijana waliokuwa wakifurika mikutano ya Tundu Lissu haupo kwenye vituo vya kupiga kura

Wamejaa watu wazima tu wanaume na wanawake .
 
Nashukuru sana Mungu kwa siku hii ya leo.

Nimefika kituo cha kupiga kura tangu saa 9:15 alfajiri, hali ni shwari kabisa mahala nilipo na mvua inapiga kwa mbali.

Ile siku imewadia [emoji3577][emoji3577][emoji3577]
We ulienda kuvizia wapiga kura uwakabe kabali!! Kura gani ulienda kupiga saa tisa za usiku? Kwa nini tusiamini kuwa wewe ni kibaka?
 
Aliyefungua uzi huu anamaana nzuri sana, tumpe nafasi. Pia tukumbuke leo siyo siku ya kampeni. Hapa tupate updates za kweli za yanayoendelea, siyo wish, ideas, hamu na mihemuko ya wachangiaji.
 
Hii ni test kwa wale walalamikaji humu....je wewe ni keyboard hero tu au field pia umeenda??

Nawachalenji KEYBOARD HEROES WOTE kuweka alama yao ya vidole ktk uzi huu kuonyesha wamepiga kura au laa....ukiweka ya mtu mwingine unakua umejifanganya mwenyewe...

Mie niko kwenye foleni hapa!
 
Tayari nishateketeza kibaraka wa mabeberu.

Turnout Inaridhisha ila kwakweli vijana ni wachache mno,

Asilimia kubwa ni watu wazima na wa umri wa kati.
 
Mimi tayari Niko kituoni. SAA 9:45.

SAA ya Ukombozi ni sasa, majuto ni Mjukuu, usifanye makosa
Tanzania ni nchi ya maajabu mengi, ikiwemo mlima mrefu sana na mbuga za wanyama wa kila aina; sasa tutaongeza ajabu jingine la watu wasiokuwa na majuto juu ya lolote.

Unaandika "majuto kuwa mjukuu"? Heri kama wasingekuwa wanajua litakalowatokea. Hawa majuto yote wanayajua na bado hawasikii chochote!
 
Shule ya msingi Mwenge mawakala wote wa Chadema wamezuiliwa kuingia vituoni na Wasimamizi wa Uchaguzi kwenye vituo hivyo.
 
Back
Top Bottom