Uchaguzi 2020 Yaliyojiri sehemu mbalimbali Tanzania katika zoezi la upigaji kura za Rais - Oktoba 28, 2020
Wale ambao tumeshindwa kupiga kula kwa sababu ya kukosa nauli njooni hapa tuongee.
 
Dr Magufuli amepiga kura yake Chamwino huko Dodoma na kuwataka wananchi waendeleze umoja na Upendo kwani kuna maisha hata baada ya uchaguzi.

Tuilinde amani yetu na kudumisha umoja wetu, amesema Dr Magufuli.

Source ITV

Maendeleo hayana vyama!
 
Acha ushari . Ondoa chuki moyoni mwako ubaki na upendo, ni maagizo ya Mungu.
Hapa nilipo nimepiga kura wa kwanza kabisa, basi nakuapia mbele ya Mungu huyu Wakala wa chadema anaulizwa kupiga kura anasema hajajiandikisha. Sijui mtashindaje uchaguzi.
Hahaha CCM story zenu hizo kila mwaka, huku mnatuibia.

Magufuli Chinja chinja huu ndio mwisho wake.
 
ElZ1uz0X0AAkMjI.jpeg
 
Fanya hivi kila kituo kina wapiga Kura 400-500 kwa mujibu wa tume. Tuchukulie wako 200. Kama kila mmoja kama atahudumiwa kwa dakika 3, inahitajika masaa 10 wote 200 ndio wamalize kupiga kura. Pita kwenye zaidi ya 75% ya vituo vya wapiga kura, wasimamizi wa vituo wanapiga story na mpiga kura anakuja mmoja mmoja. Ni hivi idadi ya wapiga kura 29m+ ni ya kupika, mbali ya kuwa ni ya kupika, watu pia wamepuuza huo utoto uitwao uchaguzi.
Sio uchaguzi ndio maana wamezima mitandao.
 
-
NEWS ALERT from MASASI

Kituo kimoja cha Kata ya Nyasa, kijana mmoja kakamatwa na makaratasi mengi ya kupigia kura feki yaliopigwa tiki tayari. Wananchi walitaka kumchoma moto bahati mbaya polisi waliwai eneo la tukio. Kahojiwa na wananchi amesema walipewa kazi na CCM
 
Iwapo kwenye karatasi ya kura uliweka tick kwa mgombea aliepo mwishoni mwa karatasi jua kabisa ni roho mtakatifu alikuongoza hata ukawaruka wagombea wengine na ukamchagua wa mwisho.

Nilipopewa karatasi ya kupigia kura sikutaka kukitazama kiumbe chochote kwenye karatasi nilienda mpaka mwisho mwa karatasi na kudondosha tick moja yenye afya kwa Mh Tundu Lissu(Rais wa awamu ya 6),nami nikasikia malaika wakishangilia mbinguni kwa vifijo,nderemo,vinubi na zumari.
 
-
Jimbo la Masasi

Hadi sasa Mawakala wetu 53 wamekataliwa kwa sababu za kukosa kitambulisho.

Kata ya Chanika Nguo.... 13
Kata ya Jida.................... 24
Kata Mumbaka................16

Tunaendelea kufuatilia kata zingine za jimbo
 
-Voting reports indicate widespread irregularities in the form of preventing our polling agents from accessing polling stations. Stuffed ballot boxes seized in Kawe, Dar. If this continues, mass democratic action will be the only option to protect the integrity of the election.Tundu Lissu
Ujinga huu
 
-Kwenye Vituo Vingi Jimbo La HAI Fomu Ya Kujazia Matokeo Ya Mbunge Kwenye Kituo (Fomu Namba 21) Haipo. Hivyo Majumuisho Ya Kura Za Mbunge Kwenye Kituo Hayawezi Kuhesabiwa Wala Kubandikwa Kwasababu Fomu Haipo.
 
Back
Top Bottom