Uchaguzi 2020 Yaliyojiri sehemu mbalimbali Tanzania katika zoezi la upigaji kura za Rais - Oktoba 28, 2020
NI kweli Lissu Hana uzalendo.
Uzalendo ni kuiba kura na kutengeneza kura feki kwa ajili ya maslahi ya CCM izidi kubaki madarakani huo ndo uzalendo
kitu pekee ambacho simkubali lissu ni kua hana uzalendo, japo ameumizwa anajaribu kufanya maumivu yake kua ya nchi nzima.. na huko ataenda kuiponde raisi, ccm na mbaya zaidi anaweza kuipondea nchi kiujumla.
 
Mtu mmoja asiwe sababu ya wengi kuharibu maisha Yao, tutampuuza kama tulivyo wapuuza kwenye Kura!

Tanzania ni sehemu ya Edeni, ni lazima kufahamu namna nzuri ya kuendesha siasa ukiwa katika nchi nzuri kama Tanzania

Na ole wa nchi yoyote itakayo shupaza shingo kuinenea mabaya Tanzania, Atapigwa majanga ya kidunia asijue anapigwa na Nani

Idumu Tanzania, na Tanzania ni kubwa kuliko mtu mmoja

Anaye niuma ni Mbowe pekee, ni mstarabu aliyeweza kuielewa nchi na Watanzania
 
Ni Postmortem ya Uchaguzi jinsi ulivyofanyika, ila angesubiri kwanza matokeo ya Urais yatangazwe kwanza, wananchi wana shauku kufahamu kwenye Urais kura zimeenda nyingi kwa nani? Ila huu uchaguzi ilikuwa ni geresha tu mshindi alishajishindia siku nyingi
 
Sijui kama hatokamatwa maana hawa watu aibu hawana kbs
Hakamatwi wala nini. Nafikiri kutokumkata na kutokumkamata ilikuwa ni moja ya strategy za CCM tangu arejee na ndio maana hata maandamano ya kumpokea yaliruhusiwa. Walijua wakimkamata hata kama kavunja sheria, ni kumpaisha.

Waliacha ajikaange kwa mafuta yake mwenyewe. Jamaa alianza kampeni bila ilani, akifikiri watanzania wote wanajali kuwa alipigwa risasi. Kumbe watu wana mahitaji yao yenye umuhimu zaidi kwao.
 
kitu pekee ambacho simkubali lissu ni kua hana uzalendo, japo ameumizwa anajaribu kufanya maumivu yake kua ya nchi nzima.. na huko ataenda kuiponde raisi, ccm na mbaya zaidi anaweza kuipondea nchi kiujumla.
Maana ya uzalendo tafadhari
 
Back
Top Bottom