Nimekuwa nikijaribu kubadilisha station mara kwa mara ili kupata kile kinachoendelea ndani ya nchi, kuna matukio kama manne au matano yaliyotokea leo nje ya utangaazaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani. Leo kulikuwa na press conference ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Antipas Tundu Lissu kuhusiana na matokeo pia Mgombea Urais wa ACT Wazalendo Maalim Sharifu Hamad nae alikiwa na press conference, kuna tukio la kukamatwa kwake na vurugu zinazoendelea huko Pemba pia ila cha ajabu televison zote zipo busy na kusikiliza matokeo. Wanatunyima haki ya kujua nini kinachondelea ndani ya tanzania ukizingatia na mitandao nayo imefungwa