Munyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kwa mara ya kwanza kabisa tokea mfumo wa vyama vingi, uingia hapa nchini, nimeona demokransia na uwazi kura za maoni ccm. Pia nampongeza mk/ wa chama kwani amesimamia na kuimiza uwazi kakika kupiga kura na kuhesabu kura mpaka kumtangaza mshindi. Sijaona eti kunamgombea amekosea kujaza fomu wala sijasikia wagombea wakilalamika kuwekewa pingamizi. Kila kitu kimefanyika kwa uwazi. Na mk/ wa ccm taifa aliwaasa wazimamizi kuwa uchaguzi ukifanyika kwa haki chama kitabaki salama . HATA MIMI NAAMINI KILA MTU AKIPATA HAKI YAKE HAKUNA MALALAMIKO. Ombi langu, kwa vwile mwekiti wa ccm DK MAGUFULI pia ndiye rais wa nchi hii na amiri jeshi wa majeshi yetu. Nakuomba usimamie mchakato wa uchaguzi mkuu ili uwe huru na wazi. Sitegemei kuona eti mtu kakosea kujaza fomu,pingamizi na kamata kamata kwa wapinzani. Naomba kuona uwazi katika kupiga kura, kuhesabu kura na hata kutangaza matokeo. Wapigakura waruhusiwe kuona kura zao zikihesabiwa vituoni na matokeo yatangazwa kwa wapiga kura vituoni. Naamini uwazi kama huo mlioutumia ukifanyika kwenye uchaguzi mkuu, kila mgombea atatoka amelizika. Manung'uniko kwa wagombe na wapiga kura yatakuwa yameisha.NAKUSII KWA NEEMA YAKE MUNGU,JOMBO ILI LIZINGATIWE