Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Ni kwamba CCM wanakula Sana hela za wagombea, Uchaguzi unavyoisha watu wanaanza maandalizi ya Uchaguzi wa miaka mitano ijayo.
 
CCM siyo chama rafiki kwa wanyonge. Pamoja na muamko mkubwa uliooneshwa wanyonge ktk uchaguzi huu kuchukuwa fomu za kugombea ubunge, lkn hakuna hata mmoja ambaye ni mnyonge atapata nafasi ya kupitishwa.

Kwanini? Kura za maoni wengi wao wamepata sufuri kabisaa! Ndiyo kisema hata majina yao hayawezi kupelekwa kwa " "mzee wa mood" (a.k.a inategemea nimeamkaje).

Wenye nazo tu ndiyo wamejizolea kura nyingi karibu kila Jimbo.

Shauri zenu......!!!!
Kasoro nyingine ni kuwa nimeona kwa mfano Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ambaye anawajua wajumbe wote wa mkutano wa kumchagua mbunge nae anaamua kuchukua fomu ili agombee ubunge, kwa mtu kama huyu utakuta tayari kawasuka hao wajumbe wasiozidi 500 na ni rahisi kwake kupita kwa kuwa katika miaka mitano ya uenyekiti amekuwa karibu na wajumbe wote,huu si utaratibu mzuri,ungewekwa utaratibu kuwa anayetaka kutia nia akiwa kama ni mbunge ,au waziri ,au mwenyekiti wa CCM kwenye jimbo basi anatakiwa ama atoe notisi kabla ya miaka 3 au 5 kuwa ama achague kuendelea na vyeo alivyonavyo au aachie akisubiri kuja kugombea ubunge katika msimu mwingine wa uchaguzi.Watia nia masikini na ambao hawana nyadhifa serikalini inakuwa vigumu kuweza kupata nafasi ya kuteuliwa kwa huu mfumo, sasa nafasi zitakuwa ni za wenye nyadhifa serikalini na kwenye chama,huu si mfumo rafiki kwa mlala hoi.
 
Pamoja sana mkuu. Hawa manyang'au ni lazima waoneshwe mlango wa kutokea. Naye msaliti Katani Ahmadi Katani kalambishwa sakafu huko Tandahimba, Mtwara.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan leo shangwe na furaha mitaani.
 
Mbona hesabu inagoma, inawezekana vipi 84+80+46+22+3+2=237 alafu wajumbe 555 ina maana wajumbe 318 wamekataa kupiga kura?
Jamaa analeta uwongo mweupe. Anadhani wote ni wajinga! Asante kumuaibisha, hajui hata kuufanya uwongo uonekane ni ukweli. Simple arithematic.
 
Tukiwa tunaelekea kwenye kinyang'anyiro cha kumpata mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kawe muda mchache ujao, ninapenda kutoa ushauri wa bure kwa Askofu Gwajima.

Tathmini ya wazi inaonyesha Askofu Gwajima hawezi kushinda, na huenda akaangukia pua vibaya, huku akipata fedheha na kudhihakiwa.

Mpaka muda huu ninapoandika, hakuna mtu hata mmoja aliyedandia treni kwa mbele (kuibuka tu na kutaka kugombea huku akiamini umaarufu wake kijamii utamvusha) ambaye ameweza kupenya.

Inavyoonekana ni kuwa, wajumbe wa CCM wanaopiga kura hawashawishiki kwa sera, umaarufu, elimu au nafasi aliyonayo mtu bali wanaweza kushawishika kwa ukaribu wako kwao toka kitambo, kujuana au kuwapa pesa.

Popote ulipo askofu Gwajima, pokea huu ushauri, hii ni sawa ni sauti ya mtu aliyepo nyikani. Linda heshima yako na taasisi unayoiongoza. Achana na hizo siasa za CCM.
 
Natafakari kila chama kama kingewezeshwa chini ya komredi Fred Mpendazoe baadhi ya wanaccm wangekuwa na chama mbadala.

Lakini kwa sasa ukiutaka ubunge kwa njia ya " dirishani" itabidi uingie Nccr mageuzi, TLP au UDP maana sina hakika sana kama CCJ haijafutiliwa mbali na msajili.

Maendeleo hayana vyama!
 
Bashite hawezi kuwa Mbunge hata angepita kura za maoni ccm lazima angechezea kichapo zero no zero tu
Mkuu usijenge daraja kabla hujauona mto,amini usiamini huu sio mwisho wa Makonda anaweza hata kuteuliwa kwa na mkuu kuwa mbunge na akawa waziri au hata kurudishwa kwenye ukiranja wa mkoa,au mumesahau ya Andengenye
 
Back
Top Bottom