Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Daima ndani ya neno demokrasia, kuna maisha watu wanayaishi km Demo tu ya kifaa fulani.
Ukishindwa kuielewa basi utakuwa mpinzani

Sent from my J5 using JamiiForums mobile app
 
Watu wanacho furahia ni kuwa... WANANCHI WA DSM WAMEMKATAA MAKONDA.. HAYO YA KUTEULIWA VITI MAALUM HAITUHUSU. SALAAM ZIMEMFIKIA MTEUZI WAKE KUWA WANANCHI WA DSM HAWAMTAKI MAKONDA.
Mkuu usijenge daraja kabla hujauona mto,amini usiamini huu sio mwisho wa Makonda anaweza hata kuteuliwa kwa na mkuu kuwa mbunge na akawa waziri au hata kurudishwa kwenye ukiranja wa mkoa,au mumesahau ya Andengenye
 
Watoto wa kiume wa Mwalimu Julius Nyerere, Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Makongoro na Madaraka, wamekataliwa kwa kura nyumbani kwao Butiama, Mara.

Watoto hao wa Mwalimu Nyerere, walikuwa wakiomba ridhaa ya kupitishwa, kugombea ubunge na wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Bunda, kupitia chama cha CCM.

Katika mkutano huo ulifanyika leo, matokeo yanaonyesha kwamba vijana hao wa Mwalimu, wamebwangwa vibaya.

Hadi naandika hapa, matokeo yameonyesha kuwa Makongoro na Madaraka wote wameshindwa kuingia hata 10 bora.

Sasa wanasubiri kudra za Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kama atakuwa na njia ya kurejea jina la mmoja wao au wote, kati ya matatu ili kupata mmoja atakayepeperjsha benders ya chama hicho tawala kwa nafasi ya ubunge wa jimbo hilo.

Matokeo yanasomeka: Jumanne Sagini (kura 84), Frank Mahemba (80), Joseph Nyamboha (46), Manyerere Jackton (22), Makongoro Nyerere (3), Madaraka Nyerere (2).

Wagombea walikuwa 59, wapiga kura 555.

Akitangaza matokeo haya, msimamizi wa uchaguzi huo, Msafiri Mtemi amesema zoezi la kupiga kura lilifanyika kwa uwazi mkubwa na kuwataka wagombea wote kuheshimu matokeo.

Msimamizi huyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, amesema uamuzi wa nani atakuwa mgombea utatangazwa na chama chao baada ya kufanyika kwa mchakato mwingine katika mgazi za wilaya, mkoa na hatimaye halmashauri kuu.

Makongoro ambaye amewahi kuwa mbunge wa Arusha kupitia chama cha NCCR - Mageuzi na baadaye kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, wakati Madaraka ndiyo ameingia mara ya kwanza kujaribu bahati yake.

Haya matokeo ya kihuni mnaleta hapa mengi sio ya ukweli, kisha yakitoka matokeo rasmi tunakuta ni mambo tofauti. Hiyo figure yako haiendani na matokeo.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefanikiwa kushinda kura za maoni kwenye Jimbo la Ruangwa kwa kupita bila kupingwa kwa sababu alikuwa peke yake.



Matokeo ya kura za maoni ndani ya Chama Chetu. Jimbo la Bumbuli Jumla ya Wagombea 41 January Makamba kura 680 Anayefuatia kura 21



MATOKEO YA AWALI, RIDHIWANI, KURA 369 Pwani 20 Julai, 2020 Katika Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amepata kura za maoni 369 za kugombea nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akifuatiwa na Ramdhani Maneno, aliyepata kura 273
 
Screenshot_20200720-224449.png
 
Watu wanacho furahia ni kuwa... WANANCHI WA DSM WAMEMKATAA MAKONDA.. HAYO YA KUTEULIWA VITI MAALUM HAITUHUSU. SALAAM ZIMEMFIKIA MTEUZI WAKE KUWA WANANCHI WA DSM HAWAMTAKI MAKONDA.
Haya huyo mteuzi hamtaki na alisha mchoka akakosa 7bu ya kumtoa, ndo imepatikana fursa sasa, hatalaza damu, tupilia kuleeeeeeeeh
 
Matokeo ya kura za maoni CCM katika jimbo la Mtera - Lusinde atetea kiti.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai atetea nafasi yake Kongwa katika Kura za Maoni CCM... Ashinda kwa 96%


Zoezi la kuhesabu kura katika jimbo la Ilala limekamilika na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Zungu amepata kura 148. Mussa Zungu -148 Sophia Mjema -103 Mendrad Mpangala- 07


Uchaguzi2020 Zoezi la kuhesabu kura za maoni, Jimbo la Kisarawe limekamilika na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo ameibuka mshindi. Selemani Jafo-588 Hassan Bangusilo- 1 Fransis Gosbert -1 Mohamed Masenga-1 Ally Goha -2 Zemba Mumbi -2 Zainabu Zowange-2 Chaulembo -3
 
Huko kwetu jenista kazoa kura zoteeeeeeeeeh, mwenzake et 2 tyuuuh [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huyo Mama kumshinda ni kazi Sana, hao ndio wenye ccm yao na muda wote yuko jikoni tu.
 
Kwani hao wazee waislam ndio wanaopiga kura peke yao? au wao ndio wasimamizi wa uchaguzi? Nini kimepelekea hadi kuingiza udini katika hili? au ni chuki zako tu kwa waislam?
Kasome vizuri historia ya nchi hii ujue mchango wao na jinsi walsivyokuwa na uchu wa madaraka ila wanapenda haki.
Utakuwa huijui Kigoma vizuri wewe.
Wazee wa ujiji ni level nyingine asee
 
Back
Top Bottom