Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Alipo huko atakuwa anaugulia maumivu tu, anajifanya ana umaarufu kiasi aweze kugombea jimbo lolote hapa nchini!

Afadhali angegombea kwao koromomije labda watu wange muonea aibu, anaichezea dsm ya wabongo?
Tuna kata keki hapa
IMG-20200720-WA0058.jpg
 
Watoto wa kiume wa Mwalimu Julius Nyerere, Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Makongoro na Madaraka, wamekataliwa kwa kura nyumbani kwao Butiama, Mara.

Watoto hao wa Mwalimu Nyerere, walikuwa wakiomba ridhaa ya kupitishwa, kugombea ubunge na wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Bunda, kupitia chama cha CCM.

Katika mkutano huo ulifanyika leo, matokeo yanaonyesha kwamba vijana hao wa Mwalimu, wamebwangwa vibaya.

Hadi naandika hapa, matokeo yameonyesha kuwa Makongoro na Madaraka wote wameshindwa kuingia hata 10 bora.

Sasa wanasubiri kudra za Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kama atakuwa na njia ya kurejea jina la mmoja wao au wote, kati ya matatu ili kupata mmoja atakayepeperjsha benders ya chama hicho tawala kwa nafasi ya ubunge wa jimbo hilo.

Matokeo yanasomeka: Jumanne Sagini (kura 84), Frank Mahemba (80), Joseph Nyamboha (46), Manyerere Jackton (22), Makongoro Nyerere (3), Madaraka Nyerere (2).

Wagombea walikuwa 59, wapiga kura 555.

Akitangaza matokeo haya, msimamizi wa uchaguzi huo, Msafiri Mtemi amesema zoezi la kupiga kura lilifanyika kwa uwazi mkubwa na kuwataka wagombea wote kuheshimu matokeo.

Msimamizi huyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, amesema uamuzi wa nani atakuwa mgombea utatangazwa na chama chao baada ya kufanyika kwa mchakato mwingine katika mgazi za wilaya, mkoa na hatimaye halmashauri kuu.

Makongoro ambaye amewahi kuwa mbunge wa Arusha kupitia chama cha NCCR - Mageuzi na baadaye kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, wakati Madaraka ndiyo ameingia mara ya kwanza kujaribu bahati yake.


Na huko Kyela mwanahabari wetu Benedicto Kikoromo (Ben Kiko) anaripoti ifuatayo 1. Ally Mlagila Jumbe (Kinanasi) 502
2. Hanta Albert Mwakifuna 288 3. Dr. Harison George Mwakyembe 252
1595273922470.png
 
*WALIO ANGUKIA PUA KURA ZA MAONI CCM*

*#TeamMwananzila*
1. Sophia Mjema
2. Paul Makonda

*#TeamKuungaJuhudi*
1. Mtulia
2. J. Nassari
3. Kafulila
4. Lijualikali
5. Silinde
6. Katambi
Abdalah Mtolea ..Temeke wamekula kichwa
 
Name recognition ndio factor kubwa nimegundua.

Kiwango ambacho wamesikia jina lako kwenye jamii, hata kama ni kwa udaku.

Erick Shigongo anashindaje siasa za ubunge?

Namshangaa Amber Rutti hajagombea.
Mzee watu wanawekeza kimyakimya!Shigongo si Mara ya kwanza kwenda huko,hata 2015 kama sikosei ndio alikuwa wa Pili baada Tizeba
 
Mbona hesabu inagoma, inawezekana vipi 84+80+46+22+3+2=237 alafu wajumbe 555 ina maana wajumbe 318 wamekataa kupiga kura?

Si inasemekana watia nia walikuwa 55?

Maana yake indelea kuzigawa kura hizo za hao 318 kwa wagombea wengine 49....
 
Makonda kala za shingo asubuhi sana
Najaribu kuwafuatilia wateule wa Rais Magufuli waliobwaga manyanga na kutia nia ya ubunge.

Yule aliyekuwa DC wa Dodoma mh Patrobas Katambi sijamuona popote, je hakuwahi kutia nia?

Maendeleo hayana vyama!
 
Mkuu,hutakaa uelewe SIASA kama fikra zako ni hizo.Hata kama Makonda Atarudishwa JUA KWAMBA Kigamboni litaenda kwa Wapinzani

Makonda hakubaliki Kigamboni na hata hizo kura 122 amezipata kwa gharama kubwa sana na kwa kutumia rasilimali nyingi sana za nchi pamoja na kutoa ahadi nyingi za uwongo.Hasa kwa wakina mama na wale wenye migogoro ya ardhi.Kitendo cha Makonda kunyimwa kurana kupata chini ya 50% ya kura zote ni ushahidi kwamba hana jipya wala hana mvuto.Hata wakirudisha jina lake itabidi na KURA wamuibie ila CCM Kigamboni wameshasema kwenye sanduku la KURA kwamba HAWAMTAKI.AENDE KOLOMIJE

Kwangu Mimi GENTAMYCINE hii ndiyo ' best post ' kuliko nyinginezo kwakuwa imeongelea Uhalisia na mambo ambayo ni ya Kweli sana tu. Heko!
 
Sina majibu, hii inamaanisha Nini kwenye siasa za Tanzania za Sasa.
 
Najaribu kuwafuatilia wateule wa Rais Magufuli waliobwaga manyanga na kutia nia ya ubunge.

Yule aliyekuwa DC wa Dodoma mh Patrobas Katambi sijamuona popote, je hakuwahi kutia nia?

Maendeleo hayana vyama!
Cheki Shinyanga mjini Bwashee, kashamwagwa na Masele kitambo tuu.
 
Back
Top Bottom