Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Mwananchi mwenzetu akisubiri kupogiwa kura [emoji23][emoji23][emoji23]
IMG_20200720_151016_100.JPG
 
Nimefuatilia upigaji wa kura kwa wagombea majimboni kwa wale waliotia nia kugombea Ubunge ama udiwani, kwa hiki nilichokiona imenikumbusha ule wimbo wa Mh, Capt Komba "Ccm ni ile ile"

Haiingii akilini kama hukuweza kubadirisha wajumbe wanao piga kura kumpata mgombea ukapata mgombea ambaye ni mpya, wajumbe wa kupiga kura wanatoka kwenye Kata ambako wawakilishi wengi ama ni wazee au wanajuana kwa vilemba!

Jambo hili linaudhi, linakera, na kukatisha tamaa sana! Mh, Rais alionesha mwelekeo mzuri wa kuibadiri Ccm lakini kwa aina hii na hiki kinachoendelea Ccm bila shaka Nusu ya wabunge Watatokana na Vyama vya upinzani. Binafsi niko tayari kumpigia kura mbunge yoyote wa upinzani (kijana) ntakayeona anafaa zaidi ya hawa wabunge (wakongwe) wanaoletwa na huu unaoitwa upigaji kura za maoni.
Mwisho Mh, Jpm usipokuwa makini

"UPINZANI UTAKAO PATA AWAMU HII UTAKUWA MGUMU NA MKALI KULIKO ULE WA 2020"

Upinzani huo utaletwa na vijana ambao wapo Ccm na wengi wanaona kama hawana nafasi tena ya kuwa wawakilishi ama kushika nafasi za maamuzi kwa Taifa lao.

Nawasilisha " time will tell."
Hayo ni mawazo yako sababu hujui historia ya ccm huko nyuma. Minyukano mingi ilisababishwa na mtu kukubalika lakini kundi la watu wachache linampitisha sababu ya rushwa.
 
Dr.Tulia Ackson ambaye ni mtia nia wa Jimbo la Mbeya mjini leo 20.07.2020 ameshinda kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi wa ndani wa CCM jiji la Mbeya kwa kupata kura 843 akifuatiwa na mshindi wa pili aliepata kura 16 na watatu kura 11.

1. Dk. Tulia Akson kura 843
2. Dk. Mahenge Mabula kura 16
3. Charles Mwakipesile kura 11.
Sasa hawa wengine walikuwa wanagombea ili iweje?
Dah
 
Back
Top Bottom