Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Utaratibu wa ulivyo ni kwamba kura za maoni za leo ni mwanzo na wala sio mwisho wa mchakato. Hayakatwi majina, hayachujwi majina bali baada ya wagombea wote kupigiwa kura na wajumbe, Kamati ya Siasa ya Wilaya inapeleka matokeo na mapendekezo yao (rating and ranking) kutegemea nidhamu, uzalendo kwa nchi, utii kwa Chama na Serikali, kiwango cha elimu na uzowefu na usafi wa maadili kwa vikao vya juu kwa maamuzi ya mwisho

Jina moja linapitishwa kutokea juu na wengine wote waliogombea watalazimika kumuunga mkono mteule wa CC tena bila kinyongo wala fikra za kumuhujumu kwani adhabu yake ni kufukuzwa uanachama!

Maelezo yangu ni ya jumla, yamezingatia taratibu za kwenye kanuni za Chama na miongozo kuhusu chaguzi za teuzi, sina taarifa za ndani kama Mzee Gentamycine mwenyewe
 
Kwani hao wazee waislam ndio wanaopiga kura peke yao? au wao ndio wasimamizi wa uchaguzi? Nini kimepelekea hadi kuingiza udini katika hili? au ni chuki zako tu kwa waislam?

Kasome vizuri historia ya nchi hii ujue mchango wao na jinsi walsivyokuwa na uchu wa madaraka ila wanapenda haki.
Issue ni shule, we umesoma madrasa huko uje umuongeze nani 😟

Shukuruni saivi mnapelekwa angalau kidogo shule bado jinsia ke mnaikandamiza lakini waangalieni na wao
 
Ila maisha yanaenda kasi sana kwa kweli, wiki iliyopita nikiwa kwenye Tv yangu namuona Makonda anakagua miradi na huyo mwakifamba na hao wote waliopo meza kuu wakijinyenyekeza kwake, leo wiki moja baadae eti Makonda ndio anaomba huruma ya wale wale waliojinyenyekeza kwake.

Kuna uwezekano jina lake litarudishwa na kamati kuu lakini kuna somo kubwa atalioata na wengine tutakuwa tumelipata kupitia yeye.
 
Au sio
Screenshot_20200720-183313.jpg
 
Ameshinda katika Familia yako na siyo kwa wana CCM na kwa Jimbo la Kigamboni.
Duh, GENTA hutaki mchezo kabisa kwenye swala hili. Mwenye namba yake ya simu anitumie ili nimtumie hii clip kwa WhatsApp awe anatazama na mkewe kama kumbukumbu ya kiburi chake.

 
Back
Top Bottom