Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Tupo uku jengo la utamaduni chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere makonda kainama ila matokeo bado sijayajua
Kama kainama unategemea nini hapo ni sign ya jambo la hatari kwamba hakutegemea
 
Kule jimbo
Jimbo la moshi mjini Mr shayo na Mr priscus walijiandaa kwenye utoaji wa rushwa kwa kipindi kirefu Sana.Hivyo ccm tusipoangalia majina hayo kwa ukaribu sana.chama kinaelekea mikono isiyo salama ya rushwa.Kinondoni Kura xinaendelea kuhesabiwa, Lukuvi anapeta
Kinondoni ipi wewe?
 
Nimefuatilia upigaji wa kura kwa wagombea majimboni kwa wale waliotia nia kugombea Ubunge ama udiwani, kwa hiki nilichokiona imenikumbusha ule wimbo wa Mh, Capt Komba "Ccm ni ile ile"

Haiingii akilini kama hukuweza kubadirisha wajumbe wanao piga kura kumpata mgombea ukapata mgombea ambaye ni mpya, wajumbe wa kupiga kura wanatoka kwenye Kata ambako wawakilishi wengi ama ni wazee au wanajuana kwa vilemba!

Jambo hili linaudhi, linakera, na kukatisha tamaa sana! Mh, Rais alionesha mwelekeo mzuri wa kuibadiri Ccm lakini kwa aina hii na hiki kinachoendelea Ccm bila shaka Nusu ya wabunge Watatokana na Vyama vya upinzani. Binafsi niko tayari kumpigia kura mbunge yoyote wa upinzani (kijana) ntakayeona anafaa zaidi ya hawa wabunge (wakongwe) wanaoletwa na huu unaoitwa upigaji kura za maoni.
Mwisho Mh, Jpm usipokuwa makini

"UPINZANI UTAKAO PATA AWAMU HII UTAKUWA MGUMU NA MKALI KULIKO ULE WA 2020"

Upinzani huo utaletwa na vijana ambao wapo Ccm na wengi wanaona kama hawana nafasi tena ya kuwa wawakilishi ama kushika nafasi za maamuzi kwa Taifa lao.

Nawasilisha " time will tell."
 
Mtu kama Makonda sio rahisi ashindwe kwenye kura za maoni. Atakuwa amejitayarisha. Ninarudia tena kuna nafasi ndogo sana jina lake kurudi toka kwenye vikao vya Chama.
 
Back
Top Bottom