Ukitathimni matokeo ya uchaguzi wa jimbo la kigamboni ,Nzega mjini,Mtama utaona wakongwe waliotetea majimbo yao , Bashe na Nape Nauye wamewaacha mbali sana wapinzani wao ,mfano Nape anakura Mia nne na ushee anayemfatia Ana kura miambili na Bashe kapiga kura miatatu na ushee, anaemfatia ana kura kumi na mbili .
Kwa kigamboni Ndugulile alitakiwa amuaache mbali sana Makonda ,kwa sababu ni mbunge jimbo hilo kwa miaka 10,halafu anatofautiana na mgeni kwa kura 68, hii si nzuri kwake. Kama ilivyoada kwa ccm kuongoza kura za maoni sio tiketi ya jina kurudi.
Safari ndio imeanza kuhusu hili jimbo la kigamboni,wagombea wakapitishwe kwenye kamati ya wilaya ya siasa ,kamati ya mkoa ya siasa kisha yapelekwe Dodoma kwa wazee cardinal rule ndio jina lirudi. Wale mnaompinga Makonda msishangilie kwa sasa, baadae msije kujikuta mnasonya