Mambo sasa hadharani. Siyo rocket science wala brain surgery. Ni hesabu rahisi tu za logic.
Ni hivi...
Kwa siasa za ndani na nje ya CCM, Makonda ni taswira ya JPM.
Huko Kigamboni, Makonda kaambulia 34.76% ya kura.
Hiyo ndiyo opinion ya wana CCM wa Kigamboni dhidi ya Makonda (mirroring JPM).
Hapana shaka kuwa huo ndiyo pia mtizamo miongoni mwa wana CCM walio wengi, wakiwamo wajumbe wa mkutano mkuu wao uliofanyika hivi karibuni kule Dodoma.... kwamba ndani ya mioyo ya wana CCM, JPM atakuwa anakubalika kwa 34.76% tu na siyo ile 100% ya maigizo.
Jee, ni nini tafsiri ya yote haya kuelekea uchaguzi mkuu October 2020?
Jibu ni rahisi.... kwamba kama uchaguzi mkuu ungekuwa unafanyika katika mazingira huru na haki, JPM asingeweza kuambulia hata 30% ya kura za Watanzania.
Makonda amekuwa ni barometer kuelekea October 2020.
Ni logic rahisi tu.