JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Kumekuwepo na video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kuwa inaonesha baadhi ya wanachama wa CHADEMA wakiandamana kupinga uwepo wa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche. Video hiyo imeambatana na ujumbe unaosema:"CHADEMA wamefanya maandamano makubwa wakitaka Makamu Mwenyekiti wao, John Heche, ajiuzulu kutokana na tuhuma za wizi wa fedha za chama." Je ni upi uhalisia wa video hiyo?
Kumekuwepo na chapisho linalosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Instagram, likidai kuwa Hashim Rungwe amefichua siri kwamba viongozi wa vyama vya siasa walilipwa fedha ili kushiriki kikao kilichoitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan. Chapisho hilo limeambatanishwa na kipande cha video kilichokatwa, kinachomuonesha Hashim Rungwe akizungumza katika kipindi cha Medani za Siasa kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Star TV. Chapisho hilo lilianza kusambazwa mara baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya kikao maalumu na viongozi wa vyama vya siasa nchini kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Hata hivyo, ufuatiliaji uliofanywa kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya mtandaoni umebaini kuwa baada...
Azaki amesema Viongozi wakuu wa chama cha CHADEMA wamekuwa wakikosolewa mara kwa mara kwa kuendesha harakati zao kwa misingi ya tamaa ya madaraka na ubinafsi badala ya masilahi mapana ya taifa. Wakosoaji wengi wanabainisha kuwa maamuzi mengi ya kimkakati ndani ya chama hicho, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wagombea na mwelekeo wa kisiasa, yamekuwa yakihodhiwa na kundi dogo la watu wanaotafuta kulinda nafasi zao na kujinufaisha kibinafsi. Hali hii inajidhihirisha pale chama kinaposhindwa kujenga misingi thabiti ya demokrasia ya ndani na badala yake kutegemea majina ya watu binafsi, hatua inayowafanya wananchi wengi kuamini kwamba kiu ya viongozi hao kuingia madarakani haitokani na nia ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa mtanzania wa...
Kumekuwapo na madai mengi kuhusu radi ambayo mengine si ya kweli, yafuatayo ni madai 10 pamoja na uhalisia wake. Dhana Potofu 1: Radi haipigi sehemu ileile mara mbili. Uhalisia: Radi inaweza kupiga sehemu ileile mara nyingi, hasa ikiwa ni eneo lenye kitu kirefu, chenye ncha kali na kilichojitenga. Kwa mfano, jengo la Empire State Building hupigwa na radi takribani mara 25 kwa mwaka, na wakati mwingine zaidi ya mara 10 ndani ya dhoruba moja. Dhana Potofu 2: Radi hupiga vitu virefu pekee. Uhalisia: Radi inaweza kupiga popote. Inaweza kupiga ardhi, gari, maegesho ya magari au sehemu nyingine, si lazima kitu kiwe kirefu zaidi. Dhana Potofu 3: Ukiwa nje wakati wa radi, ni salama kujikinga chini ya mti. Uhalia: Hii ni mojawapo ya sehemu...
Nimekutana na hii video Insta wanasema, "wanachadema haujawapatia majibu ya million 900 zilipoenda kwa ujasiri Unakuja mbele za watu eti unaomba mil 30 kwaajili yako zikupe motisha, motisha gani akati umeshawaibia wanachadema mil 900 na hutaki kusema zilipo Kwa tunavokufahamu wewe ingekua sio kweli lazima ungesema kuwa sio kweli ila badala yake unafukuza wote wanaohoji ili uwanyamazishe, wewe na mnyika wote ni wezi wakubwa"
kumekuwepo na chapisho linalosambazwa kwenye mitandao ya kijamii likiwa na picha inayomuonesha waziri wa mambo ya ndani ya nchi, patrobas katambi, likidai kuwa amesema:"mnaotaka kunishitaki nendeni mahakamani niwasweke ndani, sitaki kuwapa faida kwa sasa." chapisho hilo linaambatana na ujumbe unaosema:"kama mnahisi sina mamlaka hayo na mnakwenda mahakamani mkijua kabisa mimi ndiye waziri wa mambo ya ndani ya nchi, basi tukutane hukohuko ili niwabane vizuri kwenye utawala wa sheria. kwa sasa siwezi kujibu maana nitawapa faida tu watu hao." — patrobas katambi. je ni upi uhalisia wa nukuu hiyo?
Kumekuwa na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Instagram, ikimuonesha Mkuu wa Kitengo cha Habari wa CHADEMA, Brenda Rupia, akitoa kauli ambazo zimefasiriwa kuwa chama hicho kina ajenda ya kufanya vurugu. Katika chapisho hilo, mwandishi amedai kuwa:"Huyu ni msemaji wa CHADEMA. Inashangaza kuona binti mdogo kama huyu akiunga mkono ajenda za uvunjifu wa amani na kukaa mbele ya kamera akisema kuwa chama chao kinapanga kufanya fujo." Aidha, chapisho hilo limeendelea kudai kuwa:"Bila shaka taarifa aliyoisoma iliandaliwa na Heche, na yeye akakabidhiwa tu ili aisome. Hata hivyo, ukweli ni kwamba Watanzania hawahitaji fujo; hawahitaji kuona miundombinu wanayoitumia kila siku ikiharibiwa wala mali zao zikiibiwa...
Wakuu nimekutana na hii taarifa uhalisia ni upi? "Hii picha ni ya mwaka 1970 mwanamfalme wa Uingereza Prince Charles ambae kwa sasa ndio Mfalme wa Uingereza aliposhuka uwanja wa ndege wa Njombe kukagua ujenzi wa barabara ya Makambako kwenda Songea uliokuwa ukijengwa kipindi hicho kwa msaada wa Serikali ya Uingereza Kutoka kushoto kwa Price Charles alievaa kombati ya kijivu ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa wa wakati huo Dr. Wilbert Kleruu. Kulia kwake mwenye kombati ya kaki ni Mbunge wa NJOMBE wa miaka hiyo Ndugu Jackson Makweta. Miaka mingi imepita sasa tangu kumbukumbu hizi zichukuliwe."
Back
Top Bottom