JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Katika jamii za kiafrika hasa Tanzania kumekuwa na nadharia kuwa mtu aking'oa mvi moja kichwani inasababisha kuota nyingine nyingi. Baadhi ya watu wakiwa katika umri ambao si wakuota mvi au wale ambao wanaanza kuota mvi, mvi zikianza kuchipua kichwani wanazing'oa wakiamini hazitaota tena lakini baadhi ya watu wanawaonya kuwa wasizing'oe kwasababu zitaota nyingine nyingi. Je, ni upi ukweli kuhusu nadharia hiyo?
Katika uhandisi jeni (genetic engineering), clone ni nakala inayofanana kabisa kijeni (genetically identical copy) ya jeni, seli, au kiumbe, inayozalishwa kutoka kwa chanzo kimoja. Kwa ufupi: Gene clone – nakala nyingi za jeni moja. Cell clone – kundi la seli zenye DNA ileile, zote zimetokana na seli moja. Organism clone – kiumbe kilichotengenezwa ili kiwe na vinasaba (DNA) vinavyofanana kabisa na vya kiumbe kingine. Mfano katika uhandisi jeni: Jeni la kutengeneza insulini kutoka kwa binadamu linaweza kuingizwa kwenye bakteria. Bakteria huyo huzaliana na kutengeneza mamilioni ya bakteria wenye jeni hilo hilo. Bakteria hao huitwa clones, na hutumika kuzalisha insulini kwa wingi. Jamiicheck tunaomba hili nalo mkalitazame
Kumekuwa na machapisho kadhaa yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya na Tanzania, yakidai kuwa kijana Mtanzania, Isaiah Yunge, ametoa zaidi ya shilling billion 7 za Kenya ili kufanikisha ndoa yake na bintiye William ruto huko nchini Kenya Miongoni mwa machapisho hayo kuna ujumbe unaodaiwa kutolewa na Isaiah Yunge ukisema: I paid 7 billion Kenyan shillings as dowry for my beautiful wife Charlene Ruto. I added 2 choppers to the first family and also awarded my in-law George one nganya bus. I also bought my wife Charlene a golden ring worth 56 million. That is the little I could afford. I thank my father-in-law Dr. William Ruto for accepting my humble dowry. Aidha, baadhi ya machapisho yamekuwa yakisambaza nukuu inayodaiwa...
Back
Top Bottom