Lisu hata kwa mtutu hawezi kuwa rais wa tz full stop.
Mitutu tena?? Mitutu ni ya wasiojulikana.

Hata kwa mtutu?? Mlisema hivyo hivyo Lissu hatarudi akarudi, mkajiapiza hadi kufa eti hawezi kupitishwa na NEC zikapangwa njama wakishirikiana na mahakama zikafeli.

Hivi kwanini mnakuwa wagumu kuelewa Nguvu ya Lissu?? Its devine power ndani yake.
 
Nyota njema huonelana asubuhi. Bab yenu kafanya mkutano mmoja tu yuko hoi. Leo lala siku ya tano na siku zinakatika kama barafu kwenye moto. Vijana makamanda wanachanja mbuga tu.
Buddy leo tuu magu na mama samia wanafanya jumla ya mikutano tisa... Magu akimalizia singida na mama samia kilosa just a single day wote watakuwa wamewafikia watu wangapi.

Lissu leo unakuwa mkutano watano kwa siku tano ndugu tazama nachokuambia kwa big picture sio narrow spectrum of understanding.
You have a work to do fanyeni kampeni kwa speed kuwafikia watu wengi ndugu hamuonekani kama u really need this.

Huku social media mnadanganyana tu.
 
Duhh umetukumbusha mengi kweli. Mimi ni mmojawapo ambae sijaona alichofanya Magufuli kama raisi, nimeona kama waziri wa ujenzi. Nitawashangaa wananchi wanaoamini utendaji wake. Ninatabiri yafuatayo 1. Raisi aliyeko madarakani anaweza kupata kura nyingi sana kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi 2. wapinzani wanaweza kupata kura nyingi sana kutoka kwa wapiga kura, lakini kwa sababu wapinzani wako wengi watazigawana na hivyo kila mmoja kupata kura chache. Kwa mwenendo huu wa Upinzani hamuwezi kamwe kuitoa ccm madarakani jiongezeni tafuteni mbinu mbadala
 
Buddy leo tuu magu na mama samia wanafanya jumla ya mikutano tisa... Magu akimalizia singida na mama samia kilosa just a single day wote watakuwa wamewafikia watu wangapi...
Hahaha eti social media hata mikutano huioni? Mtaendelea kubisha hivyo hivyo sisi tunachana mbuga tu. Hao wazee waende huko na uzee wao. Inabdi wajigawe hivyi hivyo kwenda na kasi ya Lissu hawawezi
 
Anahubiri uhuru yeye mwenyewe yuko huru alipo.

Ahahubiri kutaka haki iwepo, wakati tuna mahakama ambao ni mhimili wa kutoa haki upo imara kabisa
Sera za kuongeza mdege tano. Yaani hapo kajitahidi kubadili upepo wa kampeni.😀😀
 
Nguvu ipi buddy... Hili ni kosa mnalifanyaga sana kuamini mshashinda wakati ni mwanzo wa mbio... Uzeni sera kwa watanzania wawaelewe
Mark words ndugu lema hashind arusha mjini na Lisu atapata kura less ya magufuli na trust me wala hawataibiwa kura zao...
 
Kwa sera hizi za Lissu na zile sera za kununa ndege tano za


Magufuli basi nashauri Magufuli atafute kazi nyingine ya kufanya.View attachment 1555267
Muheshimiwa yupo Vizuri; ILA naomba ufafanuzi wa Agenda #1 kuwa atafanyaje ili kuongeza ajira kwa vijana ili ajitofautishe na viongozi wengine wanaotamka tu bila uhalisia...
 
Baba sera zinauzika na matunda tunayaona. Uwe unataka au hutaki huo ndio ukweli.
 
Lissu ni failure, hana mikakati, hadi kampeni zinakuja kuisha atakuwa amepita nusu tu ya majimbo Tz bara, hata nyumbani kwao Singida Magu atamshinda vibaya sana. Hakuna mkoa hata mmoja ambao Lissu anaweza mshinda Magu.
 
Shida ni uwasilishaji wake na kejeli dharau na matusi. Atapata kura za wapenda fujo tuu, wapenda maendeleo wanamchagua Magufuli.
 
Marekani changamoto ya ajira ipo tena sana
Labda marekani ya chato!!!

Magufuli kaajiri marubani wawili tu kwa kipindi cha miaka sita. Hizo ndizo ajira tunazoambiwa na ccm.

Ajira za marubani wawili na "air hostages" sita!
 
Lissu ni failure, hana mikakati, hadi kampeni zinakuja kuisha atakuwa amepita nusu tu ya majimbo Tz bara, hata nyumbani kwao Singida Magu atamshinda vibaya sana. Hakuna mkoa hata mmoja ambao Lissu anaweza mshinda Magu.
Sasa kama.atakuwa amepita Nusu ta Majimbo si ndio vizuri ili nyinyi chichiem mshinde??
Kazi kweli kweli
 
Labda marekani ya chato!!!

Magufuli kaajiri marubani wawili tu kwa kipindi cha miaka sita. Hizo ndizo ajira tunazoambiwa na ccm.

Ajira za marubani wawili na "air hostages" sita!
Ameshindwa kuajieri hata wafanya kazi milioni moja kwa miaka mitano. Huyu jamaa hata apewe miaka 30 atakuwa anatupotezea muda tu.
 
Shida ni uwasilishaji wake na kejeli dharau na matusi. Atapata kura za wapenda fujo tuu, wapenda maendeleo wanamchagua Magufuli.
Kuna mtu mpumbavu kama Jiwe? Kwa jinsi anavyowasilisha matamshi yake?
 
Ata hili bima kwa watanzania wote nalenyewe ni kusadikika HALIWEZEKANI!!!
Hayo yote yanawezekana mkuu! Ni suala la utashi tu wa serikali! Kama tujenga madaraja hadi baharini, tukajenga mengine hewani, Kwanini suala Bima ya afya kwa kila mtu lishindikane? Mbona Nyerere hakuchimba madini na wala hakuwa na soko pana la watalii, hakuwa taasisi rasmi za kukusanya mapato kama ilivyo sasa TRA, Lakini alitoa elimu bure mpaka University na wengine wakasomeshwa hadi nje ya nchi! Alitoa huduma za afya bure!

Alilipa walimu mishahara na posho za kufundishia, yaani kila mtumishi kwa kada yake alikuwa na mshahara na posho ya kiofisi na refreshment nyingine kibao! Wanafunzi wa shule za boarding walipewa hadi usafiri wa kupelekwa makwao nyakati za likizo! Je sisi na utitiri wa makusanyo toka vitegauchumi vyote hivi vilivyotuzunguka tumerogwa na nani hata tushindwe kutekeleza hayo? Kinachofanywa sasa ni misslocation of funds!

Tunawekeza kwenye vitu visivyo na faida! Mfano kugharamia watu wanaotukana na kunyanyasa wapinzani, kuandaa matamasha na makongamano ya wasanii wakati shule hazina madawati!

Hivi serikali ingefanya kutembea na hawa wasanii mikoa yote kuhamasisha uchangiaji wa madawati na huduma kwa miaka hii yote mitano sasa hivi matatizo hayo si yangekuwa historia! CCM acheni kuwa ving'ang'anizi wa madaraka, Pisheni watu wenye maono na mitazamo mipya watuvushe tulipokwama!
 
Sasa kama.atakuwa amepita Nusu ta Majimbo si ndio vizuri ili nyinyi chichiem mshinde??
Kazi kweli kweli

Kwani CCM kushinda ni swali ? Huu ni uchaguzi wa kutafuta Magu atashinda kwa % ngapi , ni banda la 90% au 80 au akishuka sana 75%.
 
Kwani CCM kushinda ni swali ? Huu ni uchaguzi wa kutafuta Magu atashinda kwa % ngapi , ni banda la 90% au 80 au akishuka sana 75%.
Sasa unalalamika nini?? Kwanini uumie kwa sisi kwenda mwendo wa kinyonga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…