Arusha: Ole Sabaya na wenzake wamefikishwa Mahakamani, kesi yaahirishwa
Kesi inayomkabili Ole Sabaya na walinzi wake imetajwa tena kwenye Mahakama ya Arusha na kuahirishwa hadi July 2 , kwa kile ambacho mwendesha mashitaka amedai upelelezi wake bado haujakamilika .

Sabaya ambaye Suti aliyoivaa leo inaonekana kumpwaya , amerejeshwa rumande ya Kisongo akisubiri kesi itakapotajwa tena .
Upelelezi haujakamilika?
 
Wacha watalam wapeleleze kwa taratibu ili wajiridhishe vizuri[emoji1787][emoji1787]
Huoni kama hayo ni maandalizi ya kesi kufutwa

Sabaya atalipa faini kwa DPP na kurudi kumzodoa mbowe kama kawaida
 
Sabaya kwanza unaweza kukuta hakuwa rumande!

Na atawashinda mapema tu! Au ataambiwa alipe faini kwa DPP kama kina SETH
"unaweza kuta hakuwa rumande" ww ni mkuu wa gereza ?
kesi ya kina seth na sabaya hazifanani..
 
Badala ya kumrudisha rumande angenyongwa kabisa wakati akisubiri upande wa mashitaka ukamilishe uchunguzi
 
Aliyekua DC wa Hai Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake leo wamefikishwa tena kwenye Mahakama ya Wilaya iliyopo Sekei Arusha, ili kujibu tuhuma zinazowakabili, Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matano.

Itakumbukwa June 04,2021 Sabaya na wenzake walifikishwa Mahakamani hapo ambapo baadaye Tumaini Kweka, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka anayeshughulika na usimamizi wa kesi alisema———-“uchunguzi katika baadhi ya makosa yanayomkabili Lengai na wenzake umefikia kwenye kiwango ambacho tunasema ni tamati ya kuweza kuwafikisha Mahakamani”

“Mkurugenzi wa Mashtaka baada ya kujiridhisha kwamba kweli tuhuma zilizokua zinamkabiki Lengai na wenzake kisheria zinatengeneza kosa akaamua leo wafikishwe Mahakamani, kama mlivyoona alikua akituhumiwa kuongoza magenge ya kihalifu, vitendo vya rushwa, kutakatisha fedha haramu ambayo ni matokeo ya vitendo vya rushwa”

“Vilevile Mkurugenzi alijiridhisha kwamba kuna unyang'anyi wa kutumia silaha, ndio maana amefikishwa Mahakamani leo kwa hayo makosa matano lakini kwa unyang'anyi wa kutumia silaha ni makosa mawili aliyatenda katika wakati mmoja lakini kwa wakati tofautitofauti, na kama tuhuma nyingine zitathibitika basi Mkurugenzi wa Mashtaka ataamua vinginevyo"

Zaidi, soma: Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

My Take: Mahakama na DPP huu ndiyo wa kutuaminisha umahiri wenu. Chapa ilale

======

PICHA: Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake, wakiwasili mahakamani mkoani Arusha kwenye kesi yao, leo Juni 18,2021 Ijumaa

View attachment 1822516View attachment 1822517View attachment 1822519
View attachment 1822525
Ilitakiwa aje hapo anachechemea uyo jambazi sugu, Hawa KM (special force) wa magerezani wametuangusha kwakweli
 
Mbona wanamuwahisha mapema Sana mahakamani kwann asikae kama miaka 6 hivi kama wazee wa escrow au uhamsho kusubiria ushahidi kukamilika ndipo aanze pelekwa mahakamani.Hii sio dabo standard kweli
Kingine ilitakiwa leo aje anachechemea Jambazi uyo
 
Back
Top Bottom