Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Nilikua sijajua ubinafsi wa Wabongo hadi awamu ya 5 ilivyoingia na U turns na kujitoa akili kwa "Nzagamba" wengi wa JF

Pale mtoa uzi anapata “likes” 2 tu na mtoa comment kumuelimisha mtoa uzi bwana Ngabu anapata “likes” 7 and counting,inatakiwa Ngabu ujifikirie sana!

Post yako Ngabu ni ya kinafiki sana,and the numbers dont lie!

Watanzania spoke,7-2!
 
Vijana tafuteni fulsa za kuwakwamua kiuchumi kwa manufaa yenu na taifa kwa ujumla.
Siasa za Kiafrika zinaendana na upepo wa kutafuta fulsa za kuwaneemesha wanasiasa tu.
Mkiambiwa Muandamane mutauliwa huku Viongozi wanaowatuma wakila keki ya Taifa na wanasiasa wenzao wa chamatawala.
Mwenye Masikio na Asikie
 
Pale mtoa uzi anapata “likes” 2 tu na mtoa comment kumuelimisha mtoa uzi bwana Ngabu anapata “likes” 7 and counting,inatakiwa Ngabu ujifikirie sana!

Post yako Ngabu ni ya kinafiki sana,and the numbers dont lie!

Watanzania spoke,7-2!

I’m not here looking for Likes. Maybe you are...
 
Hujaridhika na kubeba box huko!? unatakabuteuzi?? Kwenye mambo ya hekima unaleta uboya? Kuna watu Tz wamefilisika na cheni nzima imepotea! Tuna tatizo la mifumo bunge ,mahakama, hakuna checks and balance!, Yapo maelekezo ya maandishi na sauti mkuu ubaguzi wa kisiasa ,nk; Democrasia ,
 
Wapo wengi hawana habari wala hawana uelewa wa kujuwa faida ya maridhiano.Wao wanachowazia ni kulinda nafasi ya madaraka na vyeo vyao.They need to maintain status quo.Slogans za hatuhitaji misaada ya mabeberu kwa kuwa wao wanashabikia demokrasia iwepo Tanzania ,sisi ni tajiri ela ipo ya kutosha haitoshi kuondoa impacts za mdororo wa uchumi unaonekana kwa jamii nyingi za watanzania.
 
Tanzania Amani imetawala
Amani ya kupiga risasi Watanzania tena kwenye maeneo ya Bunge tukufu
Amani ya kuteka watu na kuwapoteza
Amani ya kuzuia uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara
 
Hata sielewi haya maridhiano ni aina ipi?
1.Ni ya kitaifa kuwa labda kabila au kanda fulani lina uadui na jingine?

2.Ya Kichama, kuwa Chama tawala ni kinatesa vyama vingine na kuleta uhasama wa kitaifa?
Hilo no 1 ni big NO
Hilo no 2 . Ni sarakasi tupu. Kama chama fulani basi kiridhiane na chama kingine isiwe kiujumla
Mfano. ZZK wakati vyama vingine vinamgomea rais alipohutubia bunge na kutoka alibaki. Akaitwa msaliti. Hapo ccm na ACT walikuwa poa tu.
Leo CDM katia timu Sherehe za Uhuru . ACt ya zzk imekula buyu inaaasema CDM Wamewasaliti.
Mi nadhani kama chama fulani kinabifu na mwenzake nenda mkae mridhiano huko kama ufipa kwa lumumba maana hata hii ya CDM kwenda hatukushirikishwa kama wananchi.
Kama Cuf anabifu na ACT wakakae wao .
Sio maridhiano ya kitaifa .

Mbowe alihitajika kuomba kwenda kuonana na mwenyekiti mwenzake wamalize kisailensa hatarekodiwa kuwa anaenda KUTUBU . Wenzake mbona walienda leo wanakula goodtime. Sisi asitushirikishe kumtongozea

Go figure!

Wala hatuhitaji maridhiano....
 
Leo nimeisikiliza hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Bwana Freeman Mbowe.

Katika hotuba yake hiyo fupi, Bwana Mbowe kapendekeza Rais Magufuli aitumie nafasi yake ya urais kuleta maridhiano nchini.

Mimi sikubaliani na hilo. Maridhiano [reconciliation] ya nini? Kwani Watanzania tumetendeana ubaya kiasi cha kufikia hatua ya kuwa na maridhiano?

Afrika Kusini ilibidi wawe na maridhiano baada ya Apartheid kuondolewa. Hilo lilibidi kwa sababu ya ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu uliotendeka kipindi cha Apartheid. Ilibidi waandike ukurasa mpya wa historia ya taifa lao.

Rwanda nao ilibidi waunde tume ya kudumu ya Umoja wa kitaifa na maridhiano. Kilichotokea Rwanda nacho kilikuwa ni ukiukwaji mkubwa kupita maelezo wa haki za binadamu. Hakukuwa na njia nyingine ya kusonga mbele kama taifa kama wasingesameheana na kuridhiana kutokana na kilichotokea mwaka 1994.

Mwaka 2008 Kenya nao ilibidi waunde tume ya Ukweli, Haki, na Maridhiano kwa kile kilichotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na pia kwa matukio mengine yaliyotokea kabla ya hapo.

Sasa sisi Watanzania maridhiano ni ya nini?

Ndiyo, kuna matukio ya hapa na pale ambayo yametokea. Baadhi ya matukio hayo yana mwelekeo na harufu ya kisiasa na yenye kukiuka haki za kibinadamu.

Lakini, kama taifa, bado kabisa hatujafikia kiwango cha kuwa na sababu ya maridhiano.

Watanzania bado tuna umoja. Kwa ujumla hatuchukiani kwa misingi ya kikabila, kidini, wala kisiasa.

Tumechanganyikana mno. Waislamu wameoana na kuzaa na Wakristo. Wasio na dini nao wamo humo humo.

Watu wamechangiana makabila. Unakuta mtu babu yake ni Mpare, bibi yake ni Mnyamwezi, mke wake ni Mhaya, yeye mwenyewe ni nusu Mnyamwezi nusu Mhaya, wanae wana asili ya Uhehe, Upare, Uhaya, Unyamwezi, na kadhalika.

Ambalo naliona ni la muhimu ni ustaarabu.

Ustaarabu [civility] katika namna tunavyotendeana licha ya kuwa na tofauti zinazotutenganisha kisiasa na kiitikadi.

Tumezikubali siasa za vyama vingi. Siasa za vyama vingi ni siasa za kiushindani. Ushindani una mambo mengi. Mambo hayo, kwa uchache, ni propaganda, hisia kali, kutambiana, na kadhalika.

Sasa, kwenye muktadha huo wa ushindani, tunaweza kukumbushana kuhusu ustaarabu na uungwana, utawala wa kisheria, haki sawa kwa wote, na ufuatwaji wa katiba. Kwenye hayo sina tatizo.

Lakini hizi habari za kusema sijui tuwe na maridhiano sizikubali. Bado kabisa hatujafika huko.

Najua mpo mtaosema kwamba si busara mpaka tufike huko ndo tuwe na maridhiano na blah blah.

Nami nasema hivi, kama hatujafika huko kwa nini tufanye kitu juu ya jambo ambalo halipo ilhali kuna mengine tuwezayo kuyafanya ili kuboresha hali iliyopo?

Hatuhitaji maridhiano. Tunachokihitaji ni ustaarabu na uungwana katika vile tunavyotendeana.
Usipotoshe mawazo ya busara,usilete UHUNI wako katika mambo ya msingi ,wewe ni nani mpaka usihitaji?
 
Hujaridhika na kubeba box huko!? unatakabuteuzi?? Kwenye mambo ya hekima unaleta uboya? Kuna watu Tz wamefilisika na cheni nzima imepotea! Tuna tatizo la mifumo bunge ,mahakama, hakuna checks and balance!, Yapo maelekezo ya maandishi na sauti mkuu ubaguzi wa kisiasa ,nk; Democrasia ,

Uteuzi wa nini mimi..?
 
I’m not here looking for Likes. Maybe you are...

Yeah blah blah blah

“Sipo hapa kwa ajili ya likes...yara yara yara”

Jibu jepesi sana hilo na linafahamika!

Reality ni kwamba,numbers dont lie!

Umetoa post,hizi ndio reactions za viewers ambao ndio haswa audience yako!

Hizi ndio reactions with real numbers mzee!
 
Maridhiano maana yake ni ku share ulichonacho hili taifa lenu liwe na ustawi wa kiuchumi,kisiasa na kijamii.''Integration ya makundi mbali mbali ni muhimu kuliko wale wanaounga mkono 100% yote yanayotolewa bila kutoa mchango wao kwa kuogopa kupoteza nafasi ya vyeo vyao ''KARAMA ZA KILA BINADAMU UTOFAUTIANA'' TUSIBEZANE BALI TUCHANGIE KTK UJENZI WA TAIFA LETU.''
 
Kwa mfano kukiwa na maridhiano tutapungukiwa nn we mbeba box?
Hujamuelewa.

Maridhiano ni Mapatano, sasa Mbowe anasema waridhiane / wapatane JE ni kutokana na ugomvi upi? Wa lini?

Nafikiri mleta mada amemaanisha hivyo.
 
Safi Sana Mwamba Mbowe TUVUSHE.

Leo ndiyo nimethibitisha kuwa ninyi wafuasi wa chadema ni manyumbu. Si mlimkataa kuwa Magu siyo Rais?

Leo mmeenda kumlamba mguu na kisarenda baada ya kuona Magu hana matani na wanaokwamisha maendeleo.

Huyu ni jiwe hatikisiki wala hapepesi macho
 
Hujamuelewa.

Maridhiano ni Mapatano, sasa Mbowe anasema waridhiane / wapatane JE ni kutokana na ugomvi upi? Wa lini?

Nafikiri mleta mada amemaanisha hivyo.

Kujadiliana na makamanda kwa kutumia akili ni mateso!!
 
Leo ndiyo nimethibitisha kuwa ninyi wafuasi wa chadema ni manyumbu. Si mlimkataa kuwa Magu siyo Rais?

Leo mmeenda kumlamba mguu na kisarenda baada ya kuona Magu hana matani na wanaokwamisha maendeleo.

Huyu ni jiwe hatikisiki wala hapepesi macho
Sikiliza Wewe Sisi ndio wataalamu,Siasa ni Kucheza karata yako vizuri sio bao la kuhesabu kete lile na kujua unatua wapi.
 
Back
Top Bottom