FT: Tanzania 0-2 Morocco Kufuzu Kombe la Dunia, Novemba 21, 2023
Huyu kipa ni kama yule Ayubu wa Simba!! Hamna kitu hapo!! Shuti toka katikati ya uwanja linamkuta kipa kajisahau na kushangaa mpira anauona ndani ya nyavu!!

Unaweza kukuta mlango umefungwa kumbe kitasa hakijafungwa na ufunguo wala komeo haipo!! ukisema ngoja nijaribu kuufungua unashangaa unafunguka vizurti tu!! Ndivyo alivyojaribu yule mfungaji wa morocco toka katikati ya uwanja!! HAMNA KIPA HAPO!!
Mchezaji wa moroco aliyekuwa mbele yake ndio aliemchanganya akashindwa kufanya maamuzi kwa haraka
 
Sisi TZ tunafanya mambo yetu kwa mihemko na njia za mkato.

Sasa hivi focus imekuwa kutafuta wachezaji wanaocheza nje ya nchi, lakini tunasahau kuweka miundombinu ya kuzalisha wachezaji wazuri hapa ndani.

Mfumo wa kuzalisha na kukuza vipaji haupo, mfano mdogo; toka Hashim Thabit aende kucheza Marekani miaka mingi iliyopita hakuna hamasa wala yeyotr mwingine aliyetoka, iko hivyo kwa michezo mingine pia.
 
Roma haikujengwa siku Moja, tumecheza na timu iliyotuzidi ubora sana, Morocco ni timu namba Moja kwa ubora Africa na ya 13 Duniani

Hawa wamemfunga portugal,Spain and the like mpaka kufika nusu fainali kombe la Dunia,... Unafungwa na Morocco yenye wachezaji Bayern Munich, psg, Galatasaray, man UTD eti unataka kosa afukuzwe??
Si mlisema watakufa taifa
 
Back
Top Bottom