Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Jimboni kwako au sio
 
Kumbe una watoto...aisee wee huna shida ya budget utatesa watoto. Kama una kipato chini ya mil3 wala usiwe na budget wee kula vizuri na watoto wako
 
Eva inaelekea umeajiriwa, tafuta hela za pembeni usijistress san

eva unajilipia vyote hivo hauna sponsa
Hela hazitoshi aseee 😒

Kabla ya kuwaza nipige tafu lazma nawe ujijue una nini, hata Mungu alimuuliza Musa una nini mkononi, nae akajibu nina fimbo.....😁
 
Hii ya weekely nadhani ni nzuri kwa kuanzia, thanks......
 
Hili suala wanaweza sana jamii za Asia,
Wajapan, Wachina hata Wahindi.
Watoto wanaanza kufundishwa kubajeti tokea wameanza shule.
Kuna Mjapan nilikutana naye kila atakacholipia kwa fedha anakiandika kwenye notebook.
Mwisho wa mwezi anapiga mahesabu amenunua vitu gani na ametumia sh ngapi.
Hii inamsaidia kufahamu vitu anavyotumia sana na pia inamsaidia kupunguza vitu visivyo vya msingi.
Ili kufanikisha hili mtu anatakiwa awe anaandika chini kila anachonunua au kulipia hela kila mwisho wa mwezi anapitia hii itasaidia kujua matumizi yako kwa mwezi, kufahamu gharama za matumizi ya lazima na pia itasaidia kujua matumizi yasiyo ya lazima na hivyo kuwezesha kufanya adjustment.
Nilishajaribu kufanyaga hivyo nilipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana
Ila kwa sasa siwezi mambo yamekuwa mengi mara mambo ya ujenzi, mara mpangaji (nina vijiapartment) anakupigia simu kuna tatizo kwenye nyumba,, mara kulima mara upo bored unaamua tu kwenda bar kunywa,mara anaibuka mtu wako wa karibu anakuomba msaada.
Kwa kweli kubajeti matumizi inakuwa shida mtu unaishi jinsi siku inavyokuja na jinsi mfuko unavyoruhusu
 
Sasa ni mwanamke ndo anatafuta mwanaume au vice versa?
 
Muda wako wa kuamka ni mzuri sana.
Jitahidi sana kitu cha kwanza unapoamka asubuhi ni kumuomba Mungu wako kwa imani yako.
Fanya hivyo minimum siku 40.....then rudi hapa tupe mrejesho
 
Bajeti ngumu wewe nilinunua vyakula kwa bulk system vya mwez mzima, na matumizi yote. Shida nilinunua konyag kubwa nne kila wiki ninywe moja ila nilizinywa ndani ya siku nne tu
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hadi hapo bajeti ikavurugika inabidi utafute hela nyingine ya kununua konyagi nyingine.

Namie huwa inatokea hivo sasa mipango inavurugika japo mie sio kwenye kilevi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…