Daaaah... Kwa kweli nmeshangazwa Sana. Kumbe kosa la Diamond Ni kushiriki kampen za ccm au kuwa mwanaccm!!!!
Mbona hizi Ni siasa za kishamba Sana hata kule Pemba wameziacha.. utakumbuka Pemba waligawana misikiti, maduka misiba na harusi, waliacha kuoleana na kusuhubiana kwa mnasaba wa itikadi za kidini kwamba CCM akifa au kufiwa basi akazikwe na wanaccm wenzie , akasali kwa wanaccm wenzie. Kifupi huu Ni ujinga kabisa kuliko hata upumbavu wenyewe. Tena inakuwa ujinga zaidi Kama kampeni hizi zinafanywa watu wanaopigania Uhuru wa kujieleza na kujiamulia Mambo yako ,demokrasia na usawa.
Hivi umewahi kujiuliza Kama shughuli unazofanya zikiamuliwa na itikadi ya kivyama utabaki salama!?
Kama wewe Ni muajiriwa basi bosi wako akiwa CCM akutoe atafute wakufanana nae, ukiwa na duka lako waje wanamageuzi tu CCM wasifike, familia yako mjigawe kwa misingi hiyo nduguzo wawe CDM tu aliyeko CCM apite kule ....itakuwaje!?
Hivi wewe unajitambua kweli!?
Mwenzio katumia Sanaa yake kutafuta tonge, katumia Uhuru wake kuchagua CCM, katumia uwezo wake kukampenia ccm. Ingekuwa ndio wewe wanaccm nao waamue kukuadhibu kwa kuipigania chadema ungejisikiaje fala were!??