Silencer ya nini tena wakati hiyo kelele ndio psychological torture. Yani unasema tuwafanye mbwa wa ulinzi wasibweke wang'ate kimyakimya wakati sauti za kutisha huogofya.
Uko vitani, unasikia mizinga ya adui inaunguruma angani, hujui itadondokea wapi ila moja unaona imedondoka mita 30 mbele na kuna watu wanapiga yowe kumaanisha wameumia. Mzinga mwingine umedondoka mbali yenu ila miti imevunjika, kwingine unasikia mwangwi. Utakaa hapo?
Wajerumani waliwahi unda ndege inaitwa Junkers Ju-87 Stuka, ilikuwa inapiga kelele wakati wa kushambulia na zinatisha.