Good. Kwakuwa tumeshaikubaliana kuwa hiyo ni loan. Basi tunaenda vema.
Kwenye loan naomba wataalamu wa biashara waje kutupa mwongozo mzuri zaidi.
Lakini, jua kuwa si watumishi wote wanategemea mishahara. Mikopo ina mambo mengi kuliko unavyodhani. Kwahiyo kuweka akili kuwa amepata mkopo sababu ya ufisadi, sioni kama hiyo ni hekima, labda kama utalazimisha tuwe tunafanya maamuzi kwa mihemko.
Pia, angalia lengo la mpachaji wa iyo statement, motive behind. Ameficha kwa kukunja kunja sehemu inayoonesha kuwa iyo ni fedha ya mkopo badala ya kuweka wazi kabisa.
Pili, Statement haina muhuri au proof of authenticity, tuseme bas amefanya hivyo kutetea ugali wake, lakini je, wakiprint statement yenye jina lako wakaweka 2b, statement ambayo haina muhuri tutasema ni kweli una hizo ela?
Hata kama tunataka kukomboa nchi yetu, sio kwa kusingiziana na kuamini kila tunachokiona kwa mitandao. Leo amewekwa huyo. Kesho watatengeneza picha uko na mke wa mtu..na sisi tuamini bila kuthibitisha?