Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
naomba kuuliza hivi huu mwenge huu unafaida gani
leo umekesha huku tabata nakatiza kwenda job
nakuta watoto wa shule wanakata viuno
dada huyoo ameolewa dada huyo ameolewa


nikatafakari ,,ni pesa kiasi gani zimetumika kupamba uwanja
kulikuwa na msafara wa magari kibaaaoooo
kwanini zisifanyie kingine cha maana looh
 
Faida ndo hiyo, wa Tabata mmepata burudani bure usiku kucha.
 
Habari wana jamvi

Samahani wakuu, hebu tupeana fursa kidogo ya kusema chochote kuhusu mwenge wa uhuru ktk maslahi ya taifa hili,
Hebu sema chochote kuhusu mwenge huu.....
 
sipendi kusikia mwenge hata kidogo leo niliona kwenye tv nikabadili chanel fasta.
 
Sihoni kama kuna tija maana ukikumulika tu hunakuwa zezeta we kazi yako kushabikia magamba tu hata kama kilo ya unga ikifika elfu kumi
 
Mwenge ni namna ya kuwazuga wajeda kwa posho na kutumia fedha kwa maendeleo ya kinadharia zaidi. Upuuzi mtupu!
 
Enzi zake ulikuwa ni Alama Ya UHAI na Utu wa Taifa!! Lakini sasa Mwenge unasimamia kinyume cha UHAI ... Yaani Neno LIVE ...and you spell it in Reverse ...What do you get ... E ... V ... maalizia!!
 
leo ulipitishwa msasani kimweri road, kwanza watu hawakujua ni nini baada ya kuona misululu ya magari na ving'ora, hata baada ya kujua kila mmoja akawa na lake la kusema... wenye kusema wanaiba hela hayaaaa. wenye kusema wanatusababishia foleni hayaaa... kwa kifupi watu hawakuwa na mzuka nao kabisa.
 
leo ulipitishwa msasani kimweri road, kwanza watu hawakujua ni nini baada ya kuona misululu ya magari na ving'ora, hata baada ya kujua kila mmoja akawa na lake la kusema... wenye kusema wanaiba hela hayaaaa. wenye kusema wanatusababishia foleni hayaaa... kwa kifupi watu hawakuwa na mzuka nao kabisa.


kwa maoni yangu naona mwenge unatupotezea muda na resources. huu ni mradi mwingine wa kula pesa kiulaini.
mbio za mwenge zifutwe, hazina tija
 
Mbio za mwenge ambazo zimekuwa zikiratibiwa na UVCCM na CCM pamoja na serikali na kutumia pesa nyingi za walipa kodi kwa ajili ya Timu nzima inayokuwa inakimbiza huo mwenge nchi nzima kwa kugharimia malazi na posho,na kununua mafuta ya huo mwenge na mafuta ya Magari!

Kwa karne hii mwenge unasaidia nini? Zaidi yakutembelea miradi iliyopo nchini na zaidi miradi yote ni ile inayogharimiwa na wahisani kama mashirika ya kimataifa,Tasaf kwa kupitia World Bank!

Mimi kwangu sioni kama huu mwenge unatija yoyote kwani ni uharibifu wa pesa za walipa kodii!

Ni bora hizo pesa zingeelekezwa kwenye huduma ya jamii,mahosptalini,mashuleni watoto wetu wangekuwa wanakalia madawati na siyo kukaa chini!
 
Salam wana jf wote. Huu mwenge kwakweli nimeuona uko zaidi kwa maslahi sijui ya nani? Serikali inawekeza kiasi kikubwa cha fedha kukimbiza kitu ambacho naamini hakina faida.Miradi ya kijamii yaweza funguliwa bila mwenge lakini pia miradi mingine ni mibovu inafunguliwa kiroho ngumu tu. Kwenye majimbo ya vyama pinzani nako wabunge wake wakumekuwa wakiutetemekea huu mwenge? Mikoa na wilaya mpaka idara wanautetemekea sana kwenye katiba mpya hiki ifutwe ni ujanjaujanja hakuna faida yoyote.
 
Ungeuliza hasara zitokanazo na mwenge ningepata cha kusema lkn faida sizijui,ngoja nizisubiri
 
Back
Top Bottom