Nani aliwashauri kuziweka hizo tozo na viwango vyake mara ya kwanza kabla ya kusikia kilio hiki?
 
JF ni mshindi kwenye hili.. Pongezi kwa wote waliotoa michango yenye tija na kupaza sauti zao bila kuchoka
 
This is Magufurilistic...

"Kwa kuwa pesa hizi zitaipunguzia mapato serikali, Waziri ameelekeza Serikali ianze kubana matumizi yake mfano kwenye vikao, ...
 
Nani aliwashauri kuziweka hizo tozo na viwango vyake mara ya kwanza kabla ya kusikia kilio hiki?
Ccm inatawala maiti, ndio maana wanaweza kufanya lolote bila kufikiri halafu ndio wanafikiri baadaye.

Wenye tatizo ni Watanzania wenyewe na siyo Ccm wala serikali, mpaka mtakapoacha kugombea jezi za Simba na Yanga ndio utajuwa kuna mambo ya msingi.
 
Mpaka ameitwa "panya office" ndiyo akili imemrudia na kuziona tozo zake zina maumivu makali sana kwa wananchi.
 
Tunataka tozo zifutwe sio zipunguzwe,

Mtoza Tozo pia hatumtaki.
 
Sisi wa Tigo pesa na Mpesa mbona sioni chochote hapa?

Anatuletea mzaha?
 
Tozo ya ATM sijaielewa kabisa, yaan tozo watuwekee kwa nguvu zen kuitoa waiite msamaha tena kwa miamala isizidi 30k, imagine nmeweka bank akiba 500k, then wakat wa kuitoa mnikate kweli? Mtu kalipwa let say 300k mshahara wake, kuitoa bado akatwe tozo nakati keshalipia PAYE!

Hii tozo ya miamala ya bank kwa njia ya ATM inapaswa kutolewa maana ni wizi mtupu
 
Mwigulu amekuwa unpopular kwa kuweka kanuni za kiuchumi zinazomuumiza mwananchi. Angekuwa muungwana na kukiri alishindwa na kuachia nafasi yake kwa mwingine. Bahati mbaya sisi waafrika kujiuzulu ni msamiati mgeni.
 
Kufutwa tu kwa hizo tozo siyo suluhisho! Na Waziri mwenye dhamna alitakiwa kuwajibika.

Kiufupi tu hii Wizara tangu mwanzo tulisema haimfai! Angepangiwa Wizara ya Muungano na Mazingira huko, ila siyo Wizara ya Fedha na Uchumi.
 
Sasa wale waliohamia Burundi kwa maelekezo ya Waziri itakuwaje ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…