Yaani hawa wanasiasa wanatuchezea sana. Suala ni simpo. Tupunguze sana kutumia simu za mkononi. Nadhani turudishe simu za line za ttcl. Kwani kule kuna tozo? Wakishituka tutatafuta mbadala. Ila na sisi tunazitumia sana hizo simu za mkononi. Kwani tusipozitumia itakuwaje? Mbona zamani hazikuwepo na maisha yaliendelea. Tujifunze kutozitumia sana. Yaani tupungue matumizi.
 
#Mwigulu must go#
Tulimwambia mama akusikia.
Tulio nje ya uwanja ndio tunawajua wachezaji.
 
mi naomba tushikamane hata kwa mke wangu ila sio kwenye pesa asee...
 
Sio kirahisi hivyo ndugu yangu
 
Katika ulimwengu wa tafakuri tunduizi, tunaamini kuwa "[k]ila binadamu ana uwezo wa kufikiri, lakini si kila mtu anaweza kufikiri kwa umakini. Ili kufikiri kwa umakini, mtu anapaswa kufundishwa" (Elder & Paul, 2008). Kama hivi ndivyo, basi usiweke mategemeo makubwa kwa mtu kisa tu ni msomi. Elimu isiyo sahihi na utamaduni vina mchango mkubwa sana katika kuua tafakuri tunduizi. Huu ni ugonjwa kwa nchi za Kiafrika, Tz ikiwemo.

Hallelujah!
 
Msimpunguzie Mama Kura zake mwaka 2025.
Hili la Miamala ya Simu kama lisipofanyiwa kazi haraha litamtia doa Raisi. Mwaka 2025.
 
Sio kirahisi hivyo ndugu yangu
Sasa tufanyeje? Maana wanatuonea sana hawa wanasiasa. Halafu wanaongea kwa kiburi utafikiri sisi ni watoto wao. Tena watoto wa kindergarten!
 
Sasa tufanyeje? Maana wanatuonea sana hawa wanasiasa!!!! Halafu wanaongea kwa kiburi utafikiri sisi ni watoto wao!!!! Tena watoto wa kindergarten!!!!
Kuandamana watatupiga risasi tuwe wapole tu huku tukilalamika labda watasikia kilio chetu
 
Nimesgangazwa kuona maagizo ya Rais kwa Waziri wa Fedha eti waangalie upya suala la Tozo za simu!..
Hili suala lilizungumzwa kwenye kikao cha baraza la mawaziri, na yeye Samia akiwa kama Mwenyekiti wa baraza. Waliyajadili, wakakubaliana na ndo maana likapelekwa bungeni kama muswada.

Sasa vichekesho ni kuibuka sasa baada ya kelele na kuagiza hili suala liangaliwe upya. Hakuliona hili tokea wakati wanajadili kwenye baraza la mawaziri?

Tuna shida kubwa sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…