Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya
Kwa muda mrefu nlikuwa natumia simu kufanya miamala ya fedha. Kwa ujambazi na uzandiki huu wa Mwigulu Nchemba nairudia ATM yangu. Eti Mwigulu anabwabwaja mate bungeni kuwa anawahurumia Watanzania!...
Mimi tangu wapandishe ya kutuma na kutuma sijihangaishi kabisa kumbe naweza kuishi bila kutuma na kutoa na ilibidi acha niende tu ATM hamna namna.

Hivi kwa nature yetu ni mtanzania gani utamkata Hela nyingi aendelee kutumia hyo huduma, I do believe transcations za mitandao zitashuka kabisa kuliko maelezo na mawakala kukosa ajira nchi nzima. Uchumi sio swala la majaribio
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba...
Mwigulu utafukuzwa sio muda mrefu umejitia kitanzi.

Wewe juzi ulisikika ukisema wizara yako haiwezi kubadirisha tozo kwani tiyari ni sheria hadi irudishwe bungeni. Leo baada ya wananchi kukutapika na hata bosi wako SSH na Majaliwa kuwa na mashaka na uwezo wako unaanza kutetemeka ohhh wizara nayo ina nafasi yake au mamlaka kudhibiti tozo.

Viatu vya uwaziri wa fedha mkabidhi Hussein Bashe.
 
Tozo zilionekana kichomi kabla ya utekelezaji kuanza,wasitafute misifa,hatuna waziri wa fedha hapo[emoji24]
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba...
Kodi ni sawa tutaipa, ila shida ziko kwenye kanuni. Hili kweli ni swala la wizara husika. Ukiangalia kimsingi, makato ni makubwa mno.
 
Hii nchi ngumu sana yaani, limwigulu ndilo lenyewe lilipendekeza hizo tozo na wakati linahitimisha wakalizingira mpaka nusura walibebe kule Bungeni leo hii, imekua sio yeye tena, hatari sana hawa wanasiasa wa dizaini hii
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba...
Mwigulu lazima aondolewe kwenye uwaziri, hawezi hiyo kazi, nasema atolewee 🤣🤣
 
Je tusingepiga kelele mabo yao yangetimia nasisi tungeumizwa tu.
 
Mama, ukisikia kushindwa ndiyo huku hii mbaya sana ni bora ungekomaa nayo tu kwanza hayo malalamiko!
 
Kwa sababu hii ni sheria ya Bunge, na tayari imeshapitishwa na inatakiwa kutekelezwa,
Si rais ndo mtia sahihi ili itumike.sasa yeye kama ameona umuhimu wa kufanya mabadiliko wabunge wasisite kumuunga mkono.
 
Kama kawaida ya CCM

Tengeneza tatizo, litatue, uonekane shujaa
Kazi yao kubwa ndio hiyo,yaani kwa hiyo tozo masikini watazidi kuwa masikini waliotopea,na wale wajasiliamali wadogo wadogo lazima wapotee kabisa
 
Si rais ndo mtia sahihi ili itumike.sasa yeye kama ameona umuhimu wa kufanya mabadiliko wabunge wasisite kumuunga mkono.
Yaani kina Zungu waunge mkono raia kupata afueni ya maisha?hiyo haipo
 
Amesikia?

Hapo Mwanzo alikuwa ameweka pamba kwenye masikio?

AU Kusikia mpaka aambiwe zaidi ya mara kumi?
 
Mwigulu nadhani anashindwa kuwaelewa watz ,sisi waTZ tunamaindi vitu vidogo sana ,tuko tayari kutembea kilomita moja kwenda kununua unga kilo 2 uliopunguzwa Tsh 100 na kuacha duka lililo mita 20 kutoka mlangoni mwake.
Watanzania ni wazuri kwa mgomo baridi, sasa walete polisi CCM walazimishe watu kutuma miamala.
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba...

swali walikuwa wapi kabla ya kupitisha bajeti hii kandamizi.

wafanyakazi hawana nyongeza ya mishahara kwa takribani miaka 7...na tangu kipindi chote hicho kodi zimekuwa zikipanda kila mwaka....hebu watuache tumechoka unafiki wao.
 
Hii la tozo kubwa kwenye miamala ya simu, lazima iondoke na ccm 2025. Wanaenda kurekebisha lakini itakuwa kdg sana Kama kuturidhisha.

Kampeni za ondoa ccm 2025 zianze sasa.
 
Ndani ya siku chache transactions za e-money zimeshuka kwa 70%. Asanteni watz kwa mgomo!
 
Back
Top Bottom