Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

"Nitoe rai kwa wananchi kuwa Serikali imesikia malalamiko ya wananchi na tayari tumeendelea kuyafanyia kazi, Waziri Mkuu ameshaitisha kikao kesho kuendelea kupitia masuala haya haya."

"Kwa sababu hii ni sheria ya Bunge, na tayari imeshapitishwa na inatakiwa kutekelezwa, lakini kuna maeneo ambayo yanaangukia kwenye kanuni ambazo zinaangukia Wizara ya Fedha na Wizara ya Teknolojia ya Mawasiliano."
2025 iwe fundisho, waliokuwemo na wasiokuwemo wote wapigwe chini tuanze upya
 
Wale wabunge wa CCM kule bungeni ndio wajue kelele za wananchi nje ya bunge zina nguvu zaidi ya maamuzi yao "kipofu" ya kugonga meza, na kuitikia ndio, hili liwe fundisho kwa wote, spika wa bunge, naibu wake, wabunge wote wa CCM na mawakala wao (Covid 19), na Rais anaetia saini sheria bila kufikiria.
 
Nimemsikia Mwigulu akihojiwa na BBC jioni hii.

Yeye bado anasisitiza haoni tatizo na tozo; tatizo ni wananchi hawajaelimishwa vizuri.

Hivyo kilichopo ni kuendelea kuwaelimisha wananchi.
 
Serikali SIKIVU.....

Serikali ADHIMU....

KONGOLE KWA VIONGOZI WETU🙏
 
Wale wabunge wa CCM kule bungeni ndio wajue kelele za wananchi nje ya bunge zina nguvu zaidi ya maamuzi yao "kipofu" ya kugonga meza, na kuitikia ndio, hili liwe fundisho kwa wote, spika wa bunge , naibu wake, wabunge wote wa CCM na mawakala wao (Covid 19), na Rais anaetia saini sheria bila kufikiria.
Mmmhhh...wabunge wenyewe hao wa viti maalum...bashiru...polepole...
Tutegemee nn???!!!
 
Wale wabunge wa CCM kule bungeni ndio wajue kelele za wananchi nje ya bunge zina nguvu zaidi ya maamuzi yao "kipofu" ya kugonga meza, na kuitikia ndio, hili liwe fundisho kwa wote, spika wa bunge , naibu wake, wabunge wote wa CCM na mawakala wao (Covid 19), na Rais anaetia saini sheria bila kufikiria.
Sijui wataficha wapi aibu wale waliokuwa wanaipigia debe humu humu jamii forum. Bunge kibogoyo
 
Back
Top Bottom