Wakaedit Basi na maandiko yanayokemea ushoga na usagaji kwny biblia tuelewe Moja[emoji3525]
Huwa sichangii topics ambazo watu hutumia hisia zaidi kuliko akili Ila nitajibu kwa huu upotoshaji unaofanywa na hii thread
Papa hajasema ushoga sio dhambi na hana mamlaka hiyo ya kuihalalisha dhambi maana ukisema anayo bhasi utaamini papa yupo juu ya mamlaka ya Mungu, kitu ambacho si kweli
Ila kitu alichomaanisha
"Kila uhalifu ni dhambi Ila si kila dhambi ni uhalifu"
Ndio maana hata wewe upo huru kuisaliti ndoa yako utakavyo pasipo dini kusema upigwe mawe kwa sababu si uhalifu
Kingine Mungu aliiteketeza sodoma na Gomorah kwa sababu ya homosexuality lakini gharika ya Mungu iliteketeza kila mtu. hata Yona alitumwa kuwahubiria watu wa ninawi kuwa hasira ya Mungu ipo juu yao na mji ungeteketezwa
Hivyo, utaona kuwa HASIRA YA MUNGU IPO KATIKA KILA UHARIBIFU NA UCHAFU TUNAOUFANYA
Na kama haitoshi, biblia ikaainisha wazi kuwa ni dhambi gani isiyosameheka
M A R K O 3:28-29 “Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele”.
Hivyo, wewe mzinzi, mlevi, msengenyaji, mwizi na kila aina ya dhambi, HASIRA YA MUNGU IPO JUU YETU SOTE lakini Mungu kwa rehema zake, wote ni wake na tunastahili msamaha wake tukijinyenyekeza na kufanya toba
Hivyo,kwa kauli hii, papa hajakosea 🙏🏽🙏🏽