Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
Huwa sichangii topics ambazo watu hutumia hisia zaidi kuliko akili Ila nitajibu kwa huu upotoshaji unaofanywa na hii thread

Papa hajasema ushoga sio dhambi na hana mamlaka hiyo ya kuihalalisha dhambi maana ukisema anayo bhasi utaamini papa yupo juu ya mamlaka ya Mungu, kitu ambacho si kweli

Ila kitu alichomaanisha
"Kila uhalifu ni dhambi Ila si kila dhambi ni uhalifu"

Ndio maana hata wewe upo huru kuisaliti ndoa yako utakavyo pasipo dini kusema upigwe mawe kwa sababu si uhalifu

Kingine Mungu aliiteketeza sodoma na Gomorah kwa sababu ya homosexuality lakini gharika ya Mungu iliteketeza kila mtu. hata Yona alitumwa kuwahubiria watu wa ninawi kuwa hasira ya Mungu ipo juu yao na mji ungeteketezwa
Hivyo, utaona kuwa HASIRA YA MUNGU IPO KATIKA KILA UHARIBIFU NA UCHAFU TUNAOUFANYA

Na kama haitoshi, biblia ikaainisha wazi kuwa ni dhambi gani isiyosameheka

M A R K O 3:28-29 “Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele”.


Hivyo, wewe mzinzi, mlevi, msengenyaji, mwizi na kila aina ya dhambi, HASIRA YA MUNGU IPO JUU YETU SOTE lakini Mungu kwa rehema zake, wote ni wake na tunastahili msamaha wake tukijinyenyekeza na kufanya toba

Hivyo,kwa kauli hii, papa hajakosea [emoji1431][emoji1431]
Thank you,
Tena umefanya vizuri kumtolea mfano yeye mwenyewe sababu kutwa anatuletea visa vya michepuko na watu wanachangia kwa furaha bila kuhukumu hali ya kua ni uzinzi na uzinzi umekatazwa kwenya hayo hayo maandiko yaliyokataza homosexuality, tunaona kuna mada tele za pombe na watu wanachangia kwa kupeana viwanja vya kupombeka hali ya kua Pombe imekatazwa kwenye hivyo hivyo vitabu vilivyokataza homosexuality,

Papa yupo sahihi, kama ambavyo watu wazima Me na Ke wameamua kwa hiari yao kuzini wakijua wanatenda dhambi na hukumu wataikuta kwa Mungu wao basi hivyo hivyo kwa homosexuality wanajua wakifanyacho ni dhambi na hukumu wataikuta kwa Mungu wao, iweje hao walevi, wazinzi, wasengenyaji, watoa mimba, wanyanyasa yatima na wajane, n.k wajipe ukuu wa kuwahukumu homosexuality hali ya kua wao hawajahukumiwa?

Sisi wote ni wa Mwenyeezi Mungu na kwake tutarejea tutake tusitake.
 
Ni uongo, Wakatoliki wapo tangu zamani, sasa inakuwaje wao ndio waedit? Nilitegemea aliyekuja baadaye ndio ataedit
Baadhi ya mafundisho ya kikatoriki yanakinzana na biblie hivo basi viongonzi wanahaha ni namna gan biblie ifanyiwe uchakajuaji ili wahalalishe niaovo kwa jamii,ukienda kichwa kichwa utanunua biblia ya hovyo,refer amri10 za Mungu ambavyo zimechezewa huko roma
 
Dini inayonyumbulika kutokana na wakati

They are known to be conservatives, makanisa mengine hata ndoa wanawafungisha but sio RC.
Kwa upande wa dini ushoga ni dhambi.
Japo akienda kanisani ama sehemu ingine hatofukuzwa ushoga wake.
Dhambi kubwa tukiamza kuuana ikiwa uchoko wao hauletwi kilazima kwangu.
 
Kiongozi wa Dini ana kazi ya kuzungumzia kila dhambi kama chukizo mbele za Mungu maana kila dhambi inaleta uharibiifu hivyo, Papa sio kiongozi wa kuendana na matakwa yetu sisi kuliko uhalisia wa kimaandiko na sheria ambazo anazisimamia

Japo kama kweli kasema, hii topic ni sensitive sana haswa kwa kipindi hiki ambazo tabia hizi zinakithiri na kupigwa vita hasa katika nchi ambazo kidini na kitamaduni zinauchukulia ushoga kama dhambi kubwa kuliko uuaji

Hivyo, lazma awe makini sana kama wale waliopita ambao hawakulizungumzia hili suala kiundani kabisaa kuogopa hizi backlash..

Ubaya kwa tunapokwenda, there is no way taasisi kubwa kama kanisa katholiki itaepuka kuliongelea japo kwa msimamo wa kibiblia there is no way wataitofautisha na dhambi nyinginezo kwa sababu hakuna kifungu imetofautishwa. Ngoja tuone
Ushoga sio dhambi ya kipekee iliyosababisha moto sodoma? Anyways, mm nimekuwa nikidhani ushoga kwa wakristo ni dhambi ya kipekee sana huenda nilikuwa wrong.

Basi kwa sababu ushoga na pampas ni mapacha, wanaume tukubaliane kuwa ni dhambi ya kipekee isiyofaa hata kama papa hataki.
 
Baadhi ya mafundisho ya kikatoriki yanakinzana na biblie hivo basi viongonzi wanahaha ni namna gan biblie ifanyiwe uchakajuaji ili wahalalishe niaovo kwa jamii,ukienda kichwa kichwa utanunua biblia ya hovyo,refer amri10 za Mungu ambavyo zimechezewa huko roma
ni vyema ukaionyesha hiyo unayoiita 'biblia ya hovyo hovyo', vinginevyo ni stori tu. ameshakwambia ni dhambi, unataka biblia gani inayosema sio dhambi?
 
Binafsi naona kuna mambo ya kuwa straight na mambo ya kulainisha lainisha. Mkuu wa kanisa akiuzungumzia ushoga auadress kama jambo ambalo kweli ni chukizo mbele za MUNGU.
Labda unashauri vipi kati ya haya:
1. Angelinyamazia tu jambo hili kama vile halipo?
2. Angesema uongo kuwa ni kosa?
3. angesema uongo kuwa si dhambi?
4. (ongezea)
 
Back
Top Bottom