Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
Hayo maneno kama angeongea kiongozi wa waislam saa hz huu uzi angekua anatukanwa muhammad tu lakini sijaona muislam hata mmoja kamtukana
Kukaa kimya nako ni kutotekeleza wajibu. Lazima viongozi wa dini wawajibike kurekebisha jamii, na mashoga huwezi ukawatengenezea kisiwa chao wakae peke yao, lazima wahubiriwe neno wakiwa katika jamii zetu.
 
4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. 5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? 6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki.

Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. 10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako?

Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? 11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]
 
Labda ninaweza kuwa nje ya mada kidogo lakini ni sehemu sahihi kulingana na mada husika.

Kila mtu anamtizamo wake kuhusu kauli ya Papa juu ya ushoga kama ni Dhambi lakini si KOSA kisheria. Ikiwa nchi flani baada ya kuona athari hasi za ushoga katika mamlaka yake na ikaamua kuufanya ushoga ni kosa kisheria,inakujae Papa aingilie uhuru wa kujiamlia wa jamii husika kwamba sio kosa kisheria? Alitakiwa aiongelee Vatican yake na si dunia nzima juu ya sheria za ushoga maana tumepishana.

Ukija katika mustakabali wa uwepo wa dunia,ikiwa 50% ya wanaume na 50% ya wanawake wakaamua kushiriki mapenzi ya jinsia moja,baada ya miaka 50 dunia itakuwa ujao kweli au hili linafanywa kwa makusudi gani hasa?
 
Huwa sichangii topics ambazo watu hutumia hisia zaidi kuliko akili Ila nitajibu kwa huu upotoshaji unaofanywa na hii thread

Papa hajasema ushoga sio dhambi na hana mamlaka hiyo ya kuihalalisha dhambi maana ukisema anayo bhasi utaamini papa yupo juu ya mamlaka ya Mungu, kitu ambacho si kweli

Ila kitu alichomaanisha
"Kila uhalifu ni dhambi Ila si kila dhambi ni uhalifu"

Ndio maana hata wewe upo huru kuisaliti ndoa yako utakavyo pasipo dini kusema upigwe mawe kwa sababu si uhalifu

Kingine Mungu aliiteketeza sodoma na Gomorah kwa sababu ya homosexuality lakini gharika ya Mungu iliteketeza kila mtu. hata Yona alitumwa kuwahubiria watu wa ninawi kuwa hasira ya Mungu ipo juu yao na mji ungeteketezwa
Hivyo, utaona kuwa HASIRA YA MUNGU IPO KATIKA KILA UHARIBIFU NA UCHAFU TUNAOUFANYA

Na kama haitoshi, biblia ikaainisha wazi kuwa ni dhambi gani isiyosameheka

M A R K O 3:28-29 “Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele”.

Hivyo, wewe mzinzi, mlevi, msengenyaji, mwizi na kila aina ya dhambi, HASIRA YA MUNGU IPO JUU YETU SOTE lakini Mungu kwa rehema zake, wote ni wake na tunastahili msamaha wake tukijinyenyekeza na kufanya toba

Hivyo,kwa kauli hii, papa hajakosea 🙏🏽🙏🏽
💪💪
 
Ushoga sio dhambi ya kipekee iliyosababisha moto sodoma? Anyways, mm nimekuwa nikidhani ushoga kwa wakristo ni dhambi ya kipekee sana huenda nilikuwa wrong.

Basi kwa sababu ushoga na pampas ni mapacha, wanaume tukubaliane kuwa ni dhambi ya kipekee isiyofaa hata kama papa hataki.
Ndio maana nikasema huwa sichangii mada ambazo watu wapo emotional zaidi na nikichangia ni kwa nadra sana hasa masuala ya dini, siasa au kabila za watu

Kwa point yako

Kwani Gharika ya Nuhu ilisababishwa na mashoga pekee pia mkuu

Naelewa dhambi ya ushoga na usagaji kwa akili ya kawaida inaenda kinyume na maumbile ya kawaida na hata kitamaduni ni kosa la kipekee lisilopaswa msamaha lakini kidini na kimaandiko

Haijatamkwa hivyo unless nipewe kifungu na nitakubali kubadilisha fikra zangu

Hapo ndipo papa alipoegemea kwa hiyo haijalishi kama wanaume au nchi iamue nini Ila haiwezi kubadilisha msimamo wa kimaandiko kuwa ushoga haujachukuliwa kama case isiyosameheka au iwekwe kwenye category tofauti na uzinzi ambayo wengi tunaichukulia kawaida

Lakini je, Mungu kakubaliana na matakwa yetu HAPANA
 
Ushoga sio dhambi ya kipekee iliyosababisha moto sodoma? Anyways, mm nimekuwa nikidhani ushoga kwa wakristo ni dhambi ya kipekee sana huenda nilikuwa wrong.
Na papa ametamka wazi kuwa ni dhambi
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Yuko sahihi. Kwanza hauwezi kumjua huyo shoga mpaka umchungulie huko vyumbani anafanya nini. Hii mambo ya kuitana mashoga kwa muonekano wa mtu, au sauti au tembea au hata mitizamo yetu siyo njia sahihi kwa watu waliostaarabika. Kwa hiyo na wewe uko tayari tukuchunguze unafanya nini vyumbani na bafuni?
 
Uzinzi Ni dhambi kubwa sawa na ushoga nashangaa watu wanafanya Uzinzi then wanaona sio dhambi hizi nchi za Dunia ya tatu zinawajinga wengi ktk Mambo ya dini.
Wazee wa upinde 😀😀😀😀tunawaona
 
Ukilisoma neno la Mungu na kuelewa vizuri huwezi kuyumbishwa na mtu yoyote yule haijalishi ana cheo gani kwenye kanisa, poleni Sana wakatoliki kwa sababu huyo jamaa hua mnampa nafasi Sana kwenye maisha yenu ya Imani poleni Sana
 
Swala kuwa uhalifu au sio uhalifu sio kazi yake! Kazi yake kuu ni injili na abebe ujumbe wa wokovu " tubuni na kuiamini injili".
Kwa nini akae kimya? Kumnyonga mtu aliyeua ni sheria ya nchi kadhaa ikiwemo Tanzania. Lakini kanisa linaipinga hiyo sheria. Je, unataka kusema kanisa linaunga mkono watu wawaue wenzao?
 
Uzinzi Ni dhambi kubwa sawa na ushoga nashangaa watu wanafanya Uzinzi then wanaona sio dhambi hizi nchi za Dunia ya tatu zinawajinga wengi ktk Mambo ya dini.
Dhambi ya uzinzi haifanani na ushoga ata kidogo ndyo maana aliwaangamizaa watu wa sodoma na gomoraa
 
Huwa sichangii topics ambazo watu hutumia hisia zaidi kuliko akili Ila nitajibu kwa huu upotoshaji unaofanywa na hii thread

Papa hajasema ushoga sio dhambi na hana mamlaka hiyo ya kuihalalisha dhambi maana ukisema anayo bhasi utaamini papa yupo juu ya mamlaka ya Mungu, kitu ambacho si kweli

Ila kitu alichomaanisha
"Kila uhalifu ni dhambi Ila si kila dhambi ni uhalifu"

Ndio maana hata wewe upo huru kuisaliti ndoa yako utakavyo pasipo dini kusema upigwe mawe kwa sababu si uhalifu

Kingine Mungu aliiteketeza sodoma na Gomorah kwa sababu ya homosexuality lakini gharika ya Mungu iliteketeza kila mtu. hata Yona alitumwa kuwahubiria watu wa ninawi kuwa hasira ya Mungu ipo juu yao na mji ungeteketezwa
Hivyo, utaona kuwa HASIRA YA MUNGU IPO KATIKA KILA UHARIBIFU NA UCHAFU TUNAOUFANYA

Na kama haitoshi, biblia ikaainisha wazi kuwa ni dhambi gani isiyosameheka

M A R K O 3:28-29 “Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele”.

Hivyo, wewe mzinzi, mlevi, msengenyaji, mwizi na kila aina ya dhambi, HASIRA YA MUNGU IPO JUU YETU SOTE lakini Mungu kwa rehema zake, wote ni wake na tunastahili msamaha wake tukijinyenyekeza na kufanya toba

Hivyo,kwa kauli hii, papa hajakosea 🙏🏽🙏🏽
...... Asante kwa ufafanuzi
MTAZAMO
 
Yuko sahihi. Kwanza hauwezi kumjua huyo shoga mpaka umchungulie huko vyumbani anafanya nini. Hii mambo ya kuitana mashoga kwa muonekano wa mtu, au sauti au tembea siyo njia sahihi kwa watu waliostaarabika. Kwa hiyo na wewe uko tayari tukuchunguze unafanya nini vyumbani na bafuni?

Najiuliza mbona hivi vifaa vimekua vingi mtaani? Kumbe watoto wa kiume wanazid kuharibiwa na viongozi wa dini hadi inapelekea hii jinsia ya kike wa taabike kiasi hikiView attachment 2495250
Hapo ni kwako mkuu?
 
Back
Top Bottom