Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
img_20190113_214330_521-jpg.994015
 
Umeelewa kilichoandikwa? Au unasoma lakini uelewa ndiyo shida?
Badala ya kujishughulisha na hoja wewe unaanza kydandia watu ili wakubebe na utabebwa kweli.

Yeye amesema hilo tendo siyo uharifu bali ni dhambi.
Kuna mambo yanatafsiri uharifu, na dhambi ina tafsiri yake.

Haya hebu wewe tutafsirie uharifu wa hao watu?

Wenye uelewe mdogo ndiyo mmejiweka mstari wa mbele kupinga ushoga matokeo yake ninyi ndiyo chambo mnadakwa kilaini kabisa na kumegwa kimasikhara.
 
4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.

5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?

6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.

10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]
Mnajichanganya, moja ya haki za mashoga ni kufunga ndoa huko sheria zilikopita. Unapanda nini ukiwa na sheria hizi? Kwa karne nyingi hakukuwa na haki za mashoga, tunatafuta nini sasa?

Tutajieni hizo haki za mashoga ambazo hawana wakati ni raia kama wengine. Hizi sheria zikipita alafu Padre akahubiri kuwa ushoga ni dhambi na ndoa zake ni laana unajua sheria hizo hizo zitatumika kuwafunga mapadre?

Sheria ya kutoa mimba unajua imefunga mapadre wanaopinga kuwa na hizo clinic legally? Hamjui kinachoendelea duniani na Pope analivua nguo Kanisa.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
ipo siku Papa atasema kanisa linakubaliana na ushoga,nasema ipo siku kama sio Papa huyu basi anaefata.
Kuna haja gani sasa ya kusema ushoga sio kosa wakati zipo nchi ushoga ni kosa na wanahukumiwa?,kiongozi wa Dini jambo kama hili baya la ushoga alitakiwa anyooke kwamba ushoga ni dhambi full stop.
 
ipo siku Papa atasema kanisa linakubaliana na ushoga,nasema ipo siku kama sio Papa huyu basi anaefata.
Kuna haja gani sasa ya kusema ushoga sio kosa wakati zipo nchi ushoga ni kosa na wanahukumiwa?
Basi usubiri kwanza ifike hiyo siku, usilazimishe ili upate cha kujadili sasa
 
Kuna mtu ameandika kuwa humu kuna watu wengi wavivu wa kusoma. Hebu onyesha mstari ambao amehimiza sheria za kiraia zipitishe haki ambazo Kanisa linapinga
Ukisema ushoga si uhalifu chanzo chake si sheria zilizopitishwa kuwa si uhalifu? Anaposema kanisa liwapokee kwani Kanisa lini limewakataa? Kanisa lifanye nini kipya?

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom