Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
Mbali na pale Posta vikao vyao usiku mnene siku maalumu jumanne na ijumaa v8 kali blacks zinaingia,pia Wanakutana majumbani mwao kuna mahekalu yao huko Mbezi beach,msasani nk.Only member ndio ujua.
Lile jengo la Posta KWA nje ni dogo lakini lina heka 20 lile na ni ghorofa kwenda chini Kati ya tatu hadi saba hivi. Ndio makao yao makuu KWA tza, east africa ni Nairobi. Pia KILA mkoa hata wilaya kubwa Wana makanisa yao ambayo yapo kwenye majumba ya kifahari mitaa ya matajiri mikoani
Boss naomba unionyeshe hekari hizo 20? Huwa napenda kujifunza nijue vitu vingi
 
Usiwe mshamba wa Mjini.
Nenda kathibitishe utuletee mrejesho kwani unashindwa nini kuuliza tu pale Posta, wapi liliko Kanisa la Freemason
Mimi sijaleta madai hayo. wewe uliyeleta madai kuwa ni Freemason ndio unatakiwa kuthibitisha. Yaani umpeleke mtuhumiwa wa wizi mahakamani halafu umwambie yeye alete ushahidi kuwa aliiba?
 
Usiwe mshamba wa Mjini.
Nenda kathibitishe utuletee mrejesho kwani unashindwa nini kuuliza tu pale Posta, wapi liliko Kanisa la Freemason
Boss mimi nilitaka kujua hilo jengo ni lile freemason HALL au kuna jengo lingine limeandika kanisa la freemason kama unavyodai?
 
Boss naomba unionyeshe hekari hizo 20? Huwa napenda kujifunza nijue vitu vingi
KWA macho ya kawaida huwezi ona, ukiwa na macho ya kuona uzuri wa mji wa Gamboshi wenye ghorofa refu l ghorofa 140 na treni ya kisasa toka Gamboshi hadi Bermuda triangle kupitia lagos utaweza ona huo ukubwa wa heka 20 za jengo la freemason posta nyuma ya Kempsink hotel
 
Hello Wadau.

Papa Francis wa RC ya Vatican ameupiga Mwingi Kwa Kuunga mkono ushoga na kusema Mashoga sio wahaliifu, na kwamba ni Wana wa Mungu pia.🙄🙄

Haijaeleweka mara Moja ikiwa huu ndio Msimamo wa Kanisa Katoliki au ni maoni ya binafsi ya Papa Francis.

Commets ziwe fupi fupi tafadhali.

------
Papa Francis amekosoa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja kuwa "sio haki", akisema Mungu anawapenda watoto wake wote jinsi walivyo na kuwataka maaskofu wa Kikatoliki wanaounga mkono sheria hizo kuwakaribisha watu wa LGBTQ kanisani.

"Kuwa mpenzi wa jinsia moja si kosa," Francis alisema wakati wa mahojiano Jumanne na The Associated Press.

Francis alikiri kwamba maaskofu wa Kikatoliki katika baadhi ya sehemu za dunia wanaunga mkono sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja au kubagua jamii ya LGBTQ, na yeye mwenyewe alitaja suala hilo kwa maneno ya "dhambi".

Lakini alihusisha mitazamo hiyo na asili ya kitamaduni na kusema maaskofu hasa wanahitaji kupitia mchakato wa mabadiliko ili kutambua utu wa kila mtu.

"Maaskofu hawa wanapaswa kuwa na mchakato wa uongofu," alisema, akiongeza kwamba wanapaswa kutumia "huruma, upole, kama Mungu ana kwa kila mmoja wetu".

Baadhi ya nchi 67 au mamlaka duniani kote zinaharamisha shughuli za ngono za watu wa jinsia moja zilizokubaliwa, 11 kati ya hizo zinaweza au kutoa hukumu ya kifo, kulingana na Human Dignity Trust, ambayo inafanya kazi kukomesha sheria hizo. Wataalamu wanasema kwamba hata pale ambapo sheria hazitekelezwi, zinachangia unyanyasaji, unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wa LGBTQ.

Nchini Marekani, zaidi ya majimbo kumi na mbili bado yana sheria za kupinga mapenzi ya jinsia moja kwenye vitabu, licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu wa 2003 kutangaza kuwa ni kinyume cha katiba.

Umoja wa Mataifa mara kwa mara umekuwa ukitoa wito wa kukomeshwa kwa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja , ukisema zinakiuka haki za faragha na uhuru wa kutobaguliwa na ni ukiukaji wa majukumu ya nchi chini ya sheria za kimataifa kulinda haki za binadamu za watu wote, bila kujali mwelekeo wao wa kijinsia au utambulisho wa kijinsia.

Akitangaza sheria kama hizo "sio za haki", Francis alisema Kanisa Katoliki linaweza na linapaswa kufanya kazi ili kukomesha. "Lazima ifanye hivi. Ni lazima ifanye hivi,” alisema.

Francis alinukuu Katekisimu ya Kanisa Katoliki kwa kusema wapenzi wa jinsia moja lazima wapokewe na kuheshimiwa, na hawapaswi kutengwa au kubaguliwa.

"Sisi sote ni watoto wa Mungu, na Mungu anatupenda jinsi tulivyo na kwa nguvu ambayo kila mmoja wetu anapigania utu wetu," Francis alisema, akizungumza na AP katika hoteli ya Vatican anakoishi.

Sheria hizo ni za kawaida barani Afrika na Mashariki ya Kati na ni za wakati wa ukoloni wa Waingereza au zimeongozwa na sheria za Kiislamu.

Baadhi ya Maaskofu wa Kikatoliki wameziunga mkono kwa nguvu kwamba zinaendana na mafundisho ya Vatikani ambayo yanachukulia vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kuwa "vina machafuko ya asili", huku wengine wakitaka zibatilishwe kama ukiukwaji wa utu msingi wa binadamu.

Mnamo mwaka wa 2019, Francis alitarajiwa kutoa tamko la kupinga kuharamishwa kwa mapenzi ya jinsia moja wakati wa mkutano na vikundi vya haki za binadamu ambavyo vilifanya utafiti juu ya athari za sheria kama hizo na kile kinachoitwa "matibabu ya ubadilishaji".

Hatimaye, papa hakukutana na makundi, ambayo badala yake yalikutana na mtu Nambari 2 Vatikani, ambaye alithibitisha tena "hadhi ya kila mtu na dhidi ya kila aina ya vurugu".

Siku ya Jumanne, Francis alisema kuna haja ya kuwa na tofauti kati ya uhalifu na dhambi kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja.

"mapenzi ya jinsia moja si kosa," alisema. "Sio uhalifu. Ndio, lakini ni dhambi. Sawa, lakini kwanza tutofautishe kati ya dhambi na uhalifu.”

"Pia ni dhambi kukosa hisani," aliongeza.

Mafundisho ya Kikatoliki yanashikilia kwamba ingawa wapenzi wa jinsia moja lazima waheshimiwe, vitendo vyao "vina machafuko ya asili". Francis hajabadilisha mafundisho hayo, lakini amefanya kufikia jumuiya ya LGBTQ kuwa alama mahususi ya upapa wake.

Kuanzia na tamko lake maarufu la 2013: "Mimi ni nani kuhukumu?" alipoulizwa kuhusu kasisi aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa jinsia moja , Francis ameendelea kuhudumu mara kwa mara na hadharani kwa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia .

Akiwa askofu mkuu wa Buenos Aires, alipendelea kutoa ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja kama njia mbadala ya kuidhinisha ndoa zao, jambo ambalo mafundisho ya Kikatoliki yanakataza.

Licha ya mawasiliano hayo, Francis alikosolewa na jumuiya ya Wakatoliki wa LGBTQ kwa amri ya 2021 kutoka ofisi ya mafundisho ya Vatikani kwamba kanisa haliwezi kubariki muungano wa watu wa jinsia moja "kwa sababu Mungu hawezi kubariki dhambi".

Vatikani mwaka wa 2008 ilikataa kutia saini tamko la Umoja wa Mataifa lililotaka kukomeshwa kwa mapenzi ya jinsia moja, ikilalamika kuwa maandishi hayo yalikwenda nje ya upeo wa awali na pia yalijumuisha lugha kuhusu "mwelekeo wa kijinsia" na "utambulisho wa kijinsia" .

Katika taarifa yake wakati huo, Vatikani ilizitaka nchi kuepuka "ubaguzi usio wa haki" dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kukomesha adhabu dhidi yao.


Chanzo: BBC Swahili
Tatizo hili kweli dini ni imani
 
KWA macho ya kawaida huwezi ona, ukiwa na macho ya kuona uzuri wa mji wa Gamboshi wenye ghorofa refu l ghorofa 140 na treni ya kisasa toka Gamboshi hadi Bermuda triangle kupitia lagos utaweza ona huo ukubwa wa heka 20 za jengo la freemason posta nyuma ya Kempsink hotel
Anhaa.. kumbe unazungumzia KWA upande wa ki IMANI zaidi hapo SAWA KWA sababu maswala ya kiimani huwa hayana uthibitisho huenda ukawa tu umetunga kutufurahisha. Mana nipishapewa stori nyingi sana wengine wakisema hekari10, mwningine5, mwingine 50 wengine WANASEMA ni chama cha misaada kwahyo ni stori nyingi huwa kila mtu anajitungia. Kama ungenipa ushahidi unaonekana kiukweli ningekubaliana na wewe ILA nishasikia stori nyingi mpaka basi
 
Anhaa.. kumbe unazungumzia KWA upande wa ki IMANI zaidi hapo SAWA KWA sababu maswala ya kiimani huwa hayana uthibitisho huenda ukawa tu umetunga kutufurahisha. Mana nipishapewa stori nyingi sana wengine wakisema hekari10, mwningine5, mwingine 50 wengine WANASEMA ni chama cha misaada kwahyo ni stori nyingi huwa kila mtu anajitungia. Kama ungenipa ushahidi unaonekana kiukweli ningekubaliana na wewe ILA nishasikia stori nyingi mpaka basi

Mambo ya kiroho uthibitika kiroho kwa matokeo ya kimwili
 
Mambo ya kiroho uthibitika kiroho kwa matokeo ya kimwili
Ndo mana nikasemaje havina uthibitisho KWA sababu kila mmoja hiyo sehemu anataja anachokijua yeye. Wewe ni mwanadamu unayesema kuna hekari20, na wapo watu waliniambia hekari50, 10, 5 na mambo mengine mengi. Ndo mana kasema hilo ni unalijua wewe kwa mana halina uthibitisho ni hayo tu
 
Ingekuwa Dini ni siasa, muda mchache tu wafuasi mbali mbali duniani wangeanza kurudisha kadi na kujivua uanachama baada ya Mkulungwa kutoa kauli hiyo! Ila kwa bahati mbaya Dini ni kitu ambacho anaepewa ana nguvu zaidi kuliko ilikotoka.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Ingekuwa Dini ni siasa, muda mchache tu wafuasi mbali mbali duniani wangeanza kurudisha kadi na kujivua uanachama baada ya Mkulungwa kutoa kauli hiyo! Ila kwa bahati mbaya Dini ni kitu ambacho anaepewa ana nguvu zaidi kuliko ilikotoka.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Nimerudisha kadi rasmi ya Kanisa Katoriki la Roma.
 
Kumbe ndio maana kuna wajinga walishika bango eti Lisu anaunga mkono ushoga, ni ujinga mtupu kama hujaelewa ujumbe wa Papa.

Mashoga wanatakiwa Kwa wengi kanisani ili wahubiriwe habari njema na wajuwe matendo yao ni dhambi.

Hapa wanaolaani kauli ya Papa wengi ni wafiraji wazuri tu lakini hawajui kwamba hiyo pia ni dhambi lakini kanisa haliwatengi.
Elewa kati ya kufanya jambo kwa kificho na kifanya jambo kihalali.
Sasa ukiishafanya ndoa za jinsia moja kuwa ni haki kisheria then nani atajutia tendo la haki ili alitubie?
Kwa hiyo kujaribu kumwita kanisani ili atubu ni uongo wako maana anachokifanya ushamwidhinishia kuwa ni haki yake.
 
Ushafika na kuuliza ?
Ndio boss. Ila wengi freemason HALL ndiyo huwa WANASEMA kanisa lakini sijawahi kuona jengo limeandikwa kanisa la freemason ILA wengi watakuonyesha freemason HALL hoja yangu ni hilo neno KANISA. Ndo mana nikamuuliza limeandika kanisa la freemason mimi picha za freemason HALL zipo kwenye mitandao hata wewe unaweza kuiona ILA jengo lililoandikwa KANISA LA FREEMASON ndiyo linalotatiza huenda labda sijatembea sana. Unaweza kutumia pic ya hilo jengo lililoandikwa KANISA LA FREEMASON?
 
Back
Top Bottom