Dr. Mariposa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,264
- 10,535
Watakushangaa sana my dear, mfano sehemu imeandikwa Zahanati wewe ukaulize kama kuna Hakimu [emoji1]sasa angalia hiyo statement aliyoandika kwamba ushawahi kuwauliza wana kanisa? Hivi nitakuwa na akili kwenda kuuliza sehemu imeandikwa freemason HALL kwamba mna kanisa embu nisaidie kwenye hili au mimi uelewa wangu finyu?
Lile Hall mimi binafsi na rafiki zangu enzi za utoto wa shule tuliwahi kwenda pale, tukakutana na Walinzi wakatutwanga maswali kadhaa tukaondoka tumenywea, walikua wana haki kwanza walitaka kujua tuna shida gani ya kuingia mule ndani, 'hatukua nayo ni umbea wetu tu' [emoji1], wakataka kujua kama kuna Mtu tunafahamiana nae mule tunamuhitaji 'hatukua na huyo Mtu', mwisho wakatuambia ile ni ofisi hawawezi kuruhusu watu kuingia hovyo bila kua na ahadi na muhusika wa ndani.
Nadhani huyo ndugu yetu na yeye alijaribu akakutana ma majibu hayo ndio maana ana hasira nao.