Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
Kupitia kauli hii kanisa la ujerumani litaanza kuwatambua mashoga na kiwafungisha ndoa,
 
Alichofanya papa ni sawa na kumkuta mwizi anapigwa mawe, ukatuliza kadamnasi yakuwa mwizi hapaswi kupigwa kwakuwa kuna haki za binadamu na kumpiga ni kumvunjia haki yake BILA kusema kuwa alichofanya mwizi ni KOSA/DHAMBI na anastahili hukumu.

Hawa viongozi wa dini wako kiupigaji zaidi hawakemei dhambi directly just ni kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa.
Nani hana dhambi,?
 
Roman Catholic soon mtaanza kupelekeana moto, hivyo ndivyo kiongozi wenu anavyo taka
 
Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani Papa Francis amekemea sheria zote zinazopinga ushoga na kusema hizo sheria sio za haki kwani Mungu anawapenda watu wake wote bila ubaguzi, bila kujali kama ni mashoga au lah.

Soma mwenyewe hapa.
Pope Amepita Mule Mule Alimo Fundisha Yesu!
[emoji116][emoji116]
Luke 5:29-32
[29]Na Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake; palikuwa na mkutano mkuu wa watoza ushuru na watu wengineo waliokuwa wameketi chakulani pamoja nao.

[30]Ikawa Mafarisayo na waandishi wao kuwanung’unikia wanafunzi wake, wakisema, Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

[31]Yesu akajibu akawaambia, Wenye afya hawana haja na tabibu, isipokuwa walio hawawezi.

[32]Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.

TUSIWE KAMA MAFARISAYO![emoji56][emoji15][emoji12]
 
Hello Wadau.

Papa Francis wa RC ya Vatican ameupiga mwingi kwa kuunga mkono ushoga na kusema mashoga siyo wahaliifu, na kwamba ni wana wa Mungu pia.🙄🙄

Haijaeleweka mara moja ikiwa huu ndiyo msimamo wa Kanisa Katoliki au ni maoni binafsi ya Papa Francis.

Commets ziwe fupi fupi tafadhali.
Video 👇

------
Papa Francis amekosoa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja kuwa "sio haki", akisema Mungu anawapenda watoto wake wote jinsi walivyo na kuwataka maaskofu wa Kikatoliki wanaounga mkono sheria hizo kuwakaribisha watu wa LGBTQ kanisani.

"Kuwa mpenzi wa jinsia moja si kosa," Francis alisema wakati wa mahojiano Jumanne na The Associated Press.

Francis alikiri kwamba maaskofu wa Kikatoliki katika baadhi ya sehemu za dunia wanaunga mkono sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja au kubagua jamii ya LGBTQ, na yeye mwenyewe alitaja suala hilo kwa maneno ya "dhambi".

Lakini alihusisha mitazamo hiyo na asili ya kitamaduni na kusema maaskofu hasa wanahitaji kupitia mchakato wa mabadiliko ili kutambua utu wa kila mtu.

"Maaskofu hawa wanapaswa kuwa na mchakato wa uongofu," alisema, akiongeza kwamba wanapaswa kutumia "huruma, upole, kama Mungu ana kwa kila mmoja wetu".

Baadhi ya nchi 67 au mamlaka duniani kote zinaharamisha shughuli za ngono za watu wa jinsia moja zilizokubaliwa, 11 kati ya hizo zinaweza au kutoa hukumu ya kifo, kulingana na Human Dignity Trust, ambayo inafanya kazi kukomesha sheria hizo. Wataalamu wanasema kwamba hata pale ambapo sheria hazitekelezwi, zinachangia unyanyasaji, unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wa LGBTQ.

Nchini Marekani, zaidi ya majimbo kumi na mbili bado yana sheria za kupinga mapenzi ya jinsia moja kwenye vitabu, licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu wa 2003 kutangaza kuwa ni kinyume cha katiba.

Umoja wa Mataifa mara kwa mara umekuwa ukitoa wito wa kukomeshwa kwa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja , ukisema zinakiuka haki za faragha na uhuru wa kutobaguliwa na ni ukiukaji wa majukumu ya nchi chini ya sheria za kimataifa kulinda haki za binadamu za watu wote, bila kujali mwelekeo wao wa kijinsia au utambulisho wa kijinsia.

Akitangaza sheria kama hizo "sio za haki", Francis alisema Kanisa Katoliki linaweza na linapaswa kufanya kazi ili kukomesha. "Lazima ifanye hivi. Ni lazima ifanye hivi,” alisema.

Francis alinukuu Katekisimu ya Kanisa Katoliki kwa kusema wapenzi wa jinsia moja lazima wapokewe na kuheshimiwa, na hawapaswi kutengwa au kubaguliwa.

"Sisi sote ni watoto wa Mungu, na Mungu anatupenda jinsi tulivyo na kwa nguvu ambayo kila mmoja wetu anapigania utu wetu," Francis alisema, akizungumza na AP katika hoteli ya Vatican anakoishi.

Sheria hizo ni za kawaida barani Afrika na Mashariki ya Kati na ni za wakati wa ukoloni wa Waingereza au zimeongozwa na sheria za Kiislamu.

Baadhi ya Maaskofu wa Kikatoliki wameziunga mkono kwa nguvu kwamba zinaendana na mafundisho ya Vatikani ambayo yanachukulia vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kuwa "vina machafuko ya asili", huku wengine wakitaka zibatilishwe kama ukiukwaji wa utu msingi wa binadamu.

Mnamo mwaka wa 2019, Francis alitarajiwa kutoa tamko la kupinga kuharamishwa kwa mapenzi ya jinsia moja wakati wa mkutano na vikundi vya haki za binadamu ambavyo vilifanya utafiti juu ya athari za sheria kama hizo na kile kinachoitwa "matibabu ya ubadilishaji".

Hatimaye, papa hakukutana na makundi, ambayo badala yake yalikutana na mtu Nambari 2 Vatikani, ambaye alithibitisha tena "hadhi ya kila mtu na dhidi ya kila aina ya vurugu".

Siku ya Jumanne, Francis alisema kuna haja ya kuwa na tofauti kati ya uhalifu na dhambi kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja.

"mapenzi ya jinsia moja si kosa," alisema. "Sio uhalifu. Ndio, lakini ni dhambi. Sawa, lakini kwanza tutofautishe kati ya dhambi na uhalifu.”

"Pia ni dhambi kukosa hisani," aliongeza.

Mafundisho ya Kikatoliki yanashikilia kwamba ingawa wapenzi wa jinsia moja lazima waheshimiwe, vitendo vyao "vina machafuko ya asili". Francis hajabadilisha mafundisho hayo, lakini amefanya kufikia jumuiya ya LGBTQ kuwa alama mahususi ya upapa wake.

Kuanzia na tamko lake maarufu la 2013: "Mimi ni nani kuhukumu?" alipoulizwa kuhusu kasisi aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa jinsia moja , Francis ameendelea kuhudumu mara kwa mara na hadharani kwa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia .

Akiwa askofu mkuu wa Buenos Aires, alipendelea kutoa ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja kama njia mbadala ya kuidhinisha ndoa zao, jambo ambalo mafundisho ya Kikatoliki yanakataza.

Licha ya mawasiliano hayo, Francis alikosolewa na jumuiya ya Wakatoliki wa LGBTQ kwa amri ya 2021 kutoka ofisi ya mafundisho ya Vatikani kwamba kanisa haliwezi kubariki muungano wa watu wa jinsia moja "kwa sababu Mungu hawezi kubariki dhambi".

Vatikani mwaka wa 2008 ilikataa kutia saini tamko la Umoja wa Mataifa lililotaka kukomeshwa kwa mapenzi ya jinsia moja, ikilalamika kuwa maandishi hayo yalikwenda nje ya upeo wa awali na pia yalijumuisha lugha kuhusu "mwelekeo wa kijinsia" na "utambulisho wa kijinsia" .

Katika taarifa yake wakati huo, Vatikani ilizitaka nchi kuepuka "ubaguzi usio wa haki" dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kukomesha adhabu dhidi yao.

Chanzo: BBC Swahili

pope naye atakuwa na wakwake anafumuliwa marinda kule kwenye deep sea
 
The Roman Catholic Church is among the most conservative institution. Yaani:

Kanisa Katoliki la Roma ni miongoni mwa taasisi zisizobadilika katika mafundisho na taratibu zake.

MASHOGA WASIJIPE TUMAINI KUWA KUNA SIKU KANISA LITABARIKI USHOGA KUWA NI JAMBO JEMA.

Kanisa Katoliki halijawahi kubariki ushoga na wala halijawahi kutoa kauli ya kubariki ushoga. Ushoga unahusisha mambo ya kuingiliana kinyume cha maumbile, na kwenye kuingiliana kimaumbile kunahusisha maneno haya magumu yasiyopendeza kuyatamka lakini tunalazimika kuyatamka, UFIRAJI na ULAWITI. Matendo haya ni dhambi, na hata siku moja Kanisa Katoliki kwa msingi wake, haliruhusu kubadilisha amri yoyote ya Mungu, manabii wa Mungu au mitume wa Kristo.

Baadhi ya watu, au kwa makusudi au kwa kukosa uelewa, wakaja na maneno ya uwongo kuwa Kanisa Katoliki kwa kupitia Kiongozi Mkuu wa Kanisa, Papa Francis eti limebariki ushoga.

Na hayo waliyatoa kutoka kwenye kauli aliyoitoa Papa kuhusiana na mashoga, baada ya kuulizwa na wanahabari kuhusiana na haki za mashoga. Papa Francis, jibu lake lilikuwa wazi kabisa na thabiti kwa wenye uelewa: Kwa kauli yake alisema, "HOMOSEXUALITY IS NOT A CRIME BUT IT IS A SIN. Kitu ambacho kila mwenye uelewa atakubaliana nacho.

NINI MAANA YA CRIME na SIN, na NINI UTOFAUTI WAKE:

Mtu anayefanya tendo ambalo ni crime, anakuwa criminal. Crime ni jinai. Kwa wale waliopotosha kauli ya Papa, hivi wanaamini kuwa ushoga ni jinai?

Papa alikemea tabia ya baadhi ya Serikali kufanya ushoga kuwa ni jinai, na baadhi ya Serikali kuweka sheria kali, ambapo shoga akithibitika, adhabu yake ni kifo.

Sin, ni dhambi. Dhambi ni tendo lolote lile ambalo hata kama wanadamu wote mkakubaliana ni jema, lakini maagizo ya Mungu ni tofauti, hilo lililokatazwa ukalitenda, itakuwa ni dhambi.

Kuna matendo ambayo ni dhambi (sin) na ni jinai (crime). Mathalani kuua ni dhambi, na ni jinai. Kuiba ni dhambi na ni jinai.

Kuna matendo ni dhambi lakini siyo jinai. Kwa mfano, uzinzi ni dhambi, lakini kwa mataifa mengine siyo jinai, ndiyo maana kuna baadhi ya mataifa hutoa mpaka leseni za kufanya biashara ya uzinzi. Kutowaheshimu wazazi wako ni dhambi lakini siyo jinai.

Sasa kwa msimamo wa Kanisa, na mafundisho ya Kristo, mtenda dhambi anafundishwa, na wakati mwingine anakemewa, lakini kwa upole na upendo, ili abadilike. Hatengwi. Na ndicho alichokisistiza Papa.

Yesu, katika utume wake, alikaa na kula na watu ambao wayahudi waliamini ni watenda dhambi, na wakamshutumu kuwa huyu si mwana wa Mungu, mbona anakula na kunywa na wenye dhambi? Naye akawaambia kuwa tabibu hayupo kwaajili ya walio wazima bali wagonjwa. Tena akaongeza kuwa, ni furaha ilioje mkosefu mmoja akiongoka. Na akatoa mfano juu ya mfugaji wa kondoo 100, ambaye kondoo wake mmoja akitoweka, huwaacha tisini na kenda, akamfuata yule mmoja aliyepotea. Na akimpata huyo mmoja aliyepotea hufanya sherehe. Akasema ndivyo alivyo Baba wa Mbinguni, maana yake Mungu huweza kuwaacha mamilioni walio wema na kumfuata mkosefu mmoja ili arudi kwenye kundi lake. Na mkosefu huyu akibadilika na kuongoka, huwa na furaha kubwa kwa ufalme wote mbinguni.

Mafundisho ya Kanisa Katoliki yanaegemea sana sehemu mbili, yaani maandiko matakatifu na mapokeo. Tena mapokeo yanachukua nafasi kubwa zaidi. Sababu ipo wazi, Yesu alipoondoka, hakuacha kitabu/biblia, bali aliwaacha mitume. Biblia tunayoisoma leo, imekuja kuwa kwenye muundo unaokaribia sana na wa sasa, karibia miaka 300 baada ya Kristo.

Kwa kuzingatia mapokei, ndiyo maana kuna maswali ambayo Kanisa Katoliki huwa halijitesi kutafuta sababu za kisayansi au kijamii. Kwa mfano, kwa nini wanawake hawawi makasisi? Hatujui, lakini tunachojua ni kwamba katika wale mitume wa Kristo, hakumchagua hata mwanamke mmoja kuwa mtume. Na hata wale mitume, baada ya Kristo kupaa mbinguni, hawakuwahi kumwekea mikono mwanamke yeyote kuwa mtume. Hilo ndiyo jibu. Wapo wanaharakati wa kutetea haki za wanawake, kwa nyakati tofauti wamepigania ili wanawake wawe na nafasi sawa katika utumishi wa Kanisa, lakini haiwezekani kwa sababu ya hizi sababu za kimapokeo. Lakini tunajua kila walikoenda mitume na hata Yesu, kuna akina mama waliandamana nao, wakiwaandalia chakula, na wengine wanasifika sana kwa unyofu na utakatifu wao. Kanisa likawaandalia nafasi yao ndani ya Kanisa, hao ndio wanaitwa watawa.

Kama kuna jambo lolote lile ambalo ni agizo la Kristo, Mungu Baba kwa kupitia manabii, au ni agizo la mitume wa Kristo, nina hakika, hata kufanyike jitihada gani ya kulibadili, na hata mataifa yote Duniani yaafiki, Kanisa Katoliki haliwezi kuridhia.

Kanisa Katoliki, ndiyo la kale zaidi na ndiyo lenye kumbukumbu nyingi za historia ya Ukristo, kuliko Kanisa jingine lolote, na ndilo lililokataa kuwa haliwezi kwenda na wakati katika mambo ya kiimani.

Ushoga ni dhambi, siyo kwa sababu ya wanaume wawili kuishi pamoja, au wanawake wawili kuishi pamoja, bali ni kutokana na tendo la kuingiliana kinyume cha maumbile, UFIRAJI na ULAWITI. Na kwa msingi wa kiimani, hata mwanaume anayemwingilia mkewe kinyume cha maumbile, ni mtenda dhambi, sawa na shoga maana kitendo wanachokifanya ni kile kile kilichokatazwa na Mungu. Kanisa linaweza kumbariki mtu anayefanya ushoga lakini siyo ushoga. Kwa mfano, shoga ambaye ameamua kuanza process ya kuacha ushoga, akaenda kwa Kasisi kuomba ambariki katika safari yake ya kutaka kubadilika, atabarikiwa. Atabarikiwa yeye, siyo ule ushoga wake. Ni sawa na mtu mwenye mitala, anataka aachane na baadhi ya wake zake, na kuna mchakato wa kuufuata ili kila jambo liende kwa mwongozo wa Mungu, anaweza kwenda kwa Kasisi kuomba baraka yake ili akamilishe dhamira yake njema inayoendana na ukristo. Huyo anayebarikiwa mpaka wakati huo atakuwa ni polygamist, lakini kilichobarikiwa siyo polygamist relationship yake.

Je, tubebe mawe kuwaua au tuwatie jela mashoga tunaowafahamu, na wanaume wote wanaowaingilia wake zao kinyume cha maumbile? Au vijana wanaowatafuta wasichana halafu wanawaingilia kinyume cha maumbile?

Kama ilivyo dhahiri kuwa Kanisa haliwezi kubariki ushoga, ndivyo vile lisivyoweza kubariki ufiraji, utoaji mimba, ulawiti, uzinzi, uwongo, au uabudu miungu na sanamu, na mengine yanayofanana na hayo, japo mambo hayo yapo, na wanaoyatenda tunaendelea kuhysiana nao kwenye maisha yetu ya kila siku.

Lakini kiimani, watu hawa wote tuwaendee kwa upole, upendo na unyenyekevu tuwafikishie ujumbe wa Mungu, kuwa Mungu anawapenda, na anawataka wabadilike, waoshi kwa kadiri ya maagizo na mpango wake.

Papa, katika kusisitiza kuwa Kanisa haliwezi kubariki dhambi, amesaini waraka maalum wa kuwaelekeza makasisi wote wote kuwa hairuhusiwi kubariki muungano wa mashoga (homosexuality union). Lakini shoga, bado ni mwana wa Mungu, anayestahili kutubu, na wana wa Mungu tunatakiwa kumwendea kwa upole na upendo kumfikishia ujumbe wa Mungu.
 
maelezo mareeeeefu Msingi wake ni ku dilute dhambi ya ushoga ionekane kama vile kusengenya
 
Mkishampa Papa nguvu ya kuwaamulia kipi sahihi na kipi sio sahihi...msije kasirika na kumkana akija kuwaambia muunge mkono mnayo yapinga..
 
Ushoga ni jinai pia ni dhambi labda kwenye nchi unayoishi itakuwa siyo jinai lakini si Tanzania.
Anajirubu kutetea ushoga indirect way

Uelewa wako ni mdogo
Wenye uelewa mdogo huamini wanaelewa kuliko wanaoelewa.

Jielimishe ili uweze kuelewa. Hivi unafahamu ni nani anayelifanya tendo fulani kuwa ni dhambi? Ni na nani hufanye tendo fulani kuwa ni uhalifu?

Kukusaidia kukuelewesha, maana inaonekana huelewi kabisa mwenye mambo haya.

Tendo fulani kuwa dhambi, huelezwa na sheria ya Mungu.

Tendo fulani kuwa ni uhalifu huelezwa na sheria za nchi au jamii. Tendo hilo hilo linaweza kuwa ni uhalifu Tanzania, Uganda isiwe ni uhalifu. Ndiyo maana sheria hutengenezwa na nchi husika. Mathalani kufanya biashara ya ukahaba Tanzania, ni uhalifu. Sheria zetu zinatamka hivyo. Kufanya biashara ya ukahaba Canada au Thailand, siyo uhalifu.

Lakini kwa msingi wa kiimani, kwa wakristo na waislam, Dunia nzima, kufanya ukahaba ni dhambi, wala haiwezi kuwa biashara.
 
maelezo mareeeeefu Msingi wake ni ku dilute dhambi ya ushoga ionekane kama vile kusengenya
Siyo mimi. Kama wewe ni mkristo, soma maandiko. Nimejaribu kufafanua neno la Mungu, na hii ni kwa wake waliopata neema ya kuwa waumini.

Papa ni kiongozi wa kiimani, lazima kauli zake zitaegemea kwenye msingi wa kiimani.

Kiimani, tumepewa amri 10 za Mungu. Katika zile 10, hakuna tunapoambiwa ipi ni kubwa kuliko nyingine. Yaani kuiba na kusema uwongo, na kuzini, kuua, kutamani mali ya mtu mwingine au mke asiye wako, zote ni dhambi. Hatuambiwi kubwa zaidi ni ipi.

Kwenye sheria za nchi, tunapoongelea uhalifu, ndiko kwenye utofauti wa uzito wa kosa, na adhabu zinaendana na ukubwa wa kosa.

Kiimani, tunaambiwa, dhambi kubwa kuliko zote, ni kumkufuru Roho Mtakatifu.
 
Wewe unatetea ushoga kupitia mlango wa nyuma.
Ni hivi ushoga ni zambi na ni jinai pia, full stop. Hizi hoja zingine ni porojo tupu.
 
Mkishampa Papa nguvu ya kuwaamulia kipi sahihi na kipi sio sahihi...msije kasirika na kumkana akija kuwaambia muunge mkono mnayo yapinga..
Kwanza hiyo nguvu hatujampa sisi, anayo mamlaka aliyopewa na Yesu mwenyewe Mt 16:18 na hii mamlaka imekuwa ikiendelea hadi leo.

Papa hatuamulii nini tuamini, imani yetu ina misingi ya kimaandiko na mapokeo na Kanisa limeishi hivyo zaidi ya miaka 2000 sasa. Hata hili la Ushoga Pope Francis amefafanua tu hajaleta jambo jipya.

Pamoja na mimi binafsi kupinga mara nyingi namna Pope Francis anashindwa kuwa bold kwenye mafundisho ya Kanisa hata kupelekea mmomonyoko kama unaoendelea huko Ujerumani, lakini kauli yake hii juu ya ushoga kwa asilimia kubwa imewekwa chumvi nyingi na vyombo vya habari vyenye nia ovu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kwa kifupi msimamo wa Papa Ushoga ni dhambi lakini sio jinai. Wakatoliki wa Tanzania wanataka ushoga uendele kubaki jinai ikiwezekana jinai ya hukumu ya kifo!

Back
Top Bottom