FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Kiswahili kimekupiga chenga.Ni kweli kabisa kiswahili sio lugha mama yangu. Ila uongo nautambua. Kusema huo ukumbi uko Ikulu ni uongo.
Amandla...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiswahili kimekupiga chenga.Ni kweli kabisa kiswahili sio lugha mama yangu. Ila uongo nautambua. Kusema huo ukumbi uko Ikulu ni uongo.
Amandla...
Amechamba kama vyoteHotuba ya mama Samia leo inatakiwa iandikwe kwa wino wa dhahabu.
Unajishuku tu.Amechamba kama vyote
Kwa mara ya kwanza wananchi wanarudisha kadi za chama chetu kwasababu ya mapungufuHuyu mama nchi imemshinda hii!
Hakuna awamu ya 6 ...hiyi ni awamu ya ajali ...baada ya kifo cha jiweMkialikwa, njooni, msipotokea TWASONGA MBELE!
N.b, mabwana zenu E.U,wamefika mkutanoni na wanaona kazi nzuri inayofanywa na serekali ya awamu ya sita (6).
Zito hahaha, yaani huyu jamaa ni kama katuni kabisa. Akili hana kabisa.Zitto anaona furahaaa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama va Siasa na Wadau wa Demokrasia katika ukumbi wa JNICC leo tarehe 11 Septemba, 2023 katika viwanja vya Ikulu, jijini Dares Salaam.
Kituo cha TCD kinafanya kazi vizuri tangu Rais Samia aingie madarakani, na ndie amekipa uhai. TCD ilifanya mkutano na wadau kujadili hali ya demokrasia kuelekea chaguzi za 2024 na 2025, baada ya kujadili kuna mambo tulifanyia maazimio na tutayaleta hapa.
Kuhusu Katiba, mchakato wa kupata katiba mpya uweze kuendelea, lakini kwa muda uliopo huenda tunaweza tusipate Katiba Mpya. Lakini mabadiliko ya katiba yanaweza kufanyika ikiwemo kufanya mabadiliko kifungu cha 74 cha Katiba ili tume huru iweze kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Pawepo mgombea binafsi, kufanyia marekebisho kifungu cha 39 (2) cha katiba ya sasa kuhusu Rais na kifungu cha 67(1) kuhusu wagombea ubunge. Kuwa Rais atangazwe akishinda kwa zaidi ya 50% ya kura kwa hiyo kurekebisha kifungu cha 41 (6) na uchaguzi wa Rais uweze kuhojiwa mahakamani hivyo kubadilisha kifungu cha 41 (7).
JENISTA MHAGAMA, WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE NA URATIBU)Amemshukuru Rais Samia kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huu.
Kwenye siku tatu za Mkutano huu, wajumbe watashiriki kujadiliana ni namna gani taifa letu litaimarisha na kuboresha demokrasia hapa nchini.
Pia, tathimini ya maoendekezo ya kikosi kazi yatajadiliwa kwenye mkutano huu.
Rais Samia amedhihirisha kuwa ni kiongozi anayezingatia utawala bora na kutenda haki kwa watanzania wote.
SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIALeo tunapokutana na kuzungumza mapendekezo ya kikosi kazi ni mapendekezo ambayo wote wadau wa siasa nchini wameyaleta kwa pamoja.
Tutapishana tu kwa jinsi ya kusukuma utekelezaji, huyu anataka kalileta leo lifanywe kesho, mwingine ana subira kidogo, lakini wote maono yetu ni kama yanaenda pamoja.
Tayari Serikali imeanza kuchukua hatua ya baadhi ya mapendekezo ya kikosi kazi na mnayajua, kwa mfano kuruhusu Mikutano ya hadhara, tayari imeruhusiwa watu wanakwenda na tunawasikia yanayosemwa huko.
Lakini pia tulishauriwa kuunda kanuni za kuendesha hiyo mikutano ya hadhara, zimeundwa na zinatekelezwa, hilo limeshafanyika.
Lakini pia kuna jambo mahsusi ambalo ndio kila mtu analisubiri la katiba, marekebisho ya katiba yetu ambalo nalenyewe limeanza kufanyiwa kazi na pengine mkutano huu ni kuelekea huko pia.
La mikutano ya hadhara, tumeruhusu tukiwa na nia ya vyama vya siasa vizungumze wananchi wasikie sera zao, mada zao, mipango yao ili vyama vikue na virudishe watu wale walio wapoteza, vyama visimame, viwe madhubuti, tukienda kwenye uchaguzi kila chama kimejijenga vya kutosha na ndio maana ya kutoa fursa hii ya mikutano ya hadhara.
Hatukutoa fursa ile watu wakavunje sheria, watu wakasimame kutukana, watu wakasimame kukashfu, watu wakasimame kuchambua dini za watu. Lakini sishangai kwanini haya yanatokea, kwa sababu ya kuzungumzwa hakuna.
Tulianza na katiba, tukaenda ikakatika katikati, bandari imeenda sasa katiba tena. Tumieni hiyo fursa kajijengeni kwa wananchi, elezeni sera zenu, mtafanya nini, ili wananchi warudi wawaunge mkono ili tukienda kwenye uchaguzi vyama vyote vimejijenga vizuri.
Uendeshaji wa Tanzania unahitaji fikra za kila mtu, hakuna mtu mwenye hati ya kuimiliki, hata kitoto kilichozaliwa yeye kina haki, ili tuendeshe vizuri kila kundi litoe mawazo tuendeshe nchi yetu.
Niseme tena, fursa hii iliyotoka isiende kuharibu neema na baraka aliyotupa Mungu. Isiende kuharibu misingi ya uendeshaji nchi hii wazee wetu waliyotuachia.
Lingine, hakuna aliye juu ya sheria. Kila anayefanya makosa sheria itamshika. Kama umekiuka sheria, sheria itakushika. Ajenda yetu kubwa kama watanzania ni kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Tulitoa uhuru wa maoni, maoni mengi sana yanatoka kwa watanzania, tunayaona, mazuri tunayachukua na mengine unayapima maoni yao. Nina kikundi maalumu kinachoangalia maoni yote maoni na kuchukua yale mazuri na kuyaweka kwenye mipango yetu kuyafanyia kazi.
Kuna uhuru wa maoni lakini huu uhuru wa maoni una mipaka yake, sio tu kisheria, hata kibinadamu.
PROF. MUKANDALA
Mapendekezo ya Kikosi Kazi:
Hapa ninawasilisjha mapendekezo tu. Na ninayawasilisha kama yalivyopitishwa na kikosi kazi. Sitabadilisha chochote, nitayafikisha kama yalivyokubaliwa na kikosi kazi.
Kuhusu mikutano ya vyama vya siasa, Kikosi Kazi kilipendekeza kuwa:
a) Kikosi kazi kilipendekeza kuwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa katiba na sharia.
b) Mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote.
c) Yafanyike mabadiliko ya sheria ili kuhakikisha nmikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi. Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Vyama vya Siasa, sura ya 258; Sheria ya Jeshi la Polisi
Kuhusu Demokrasia ndani ya Vyama vya Siasa, Kikosi Kazi kilipendekeza kuwa:
a) Sheria ya Vyama vya Siasa ifanyiwe marekebisho ili kulipatia Baraza la Vyama vya Siasa, linaloundwa na vyama vyenyewe mamlaka ya kulishulikia suala la uvunjifu wa maadili ndani ya vyama vya siasa kupitia Kamati yake ya Maadili – yaani vyama vyenyewe vijisimamie.
b) Msajili wa Vyama vya Siasa aandae Mwongozo wa Uchaguzi wa ndani ya Vyama vya Siasa
c) Kuwe na Masharti kwamba idadi ya jinsi moja katika vyombo vya maamuzi ya chama cha siasa isipungue asilimia 40
d) Kukitaka kila chama cha siasa kuwa na Sera ya ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli za chama husika
huyo lisu wako alitandikwa risasi na magufuli hao mabalozi wako walichukua hatua gani?Mikutano sio hisani ni kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Asitufokee… Kama umetukanwa nenda mahakamani.
Kama unaona unakerwa fanya moja achilia.
Karibu tunafika
Kumkamata Tundu Lissu jana hamkusoma alama za nyakati kwa ufupi mkuano wako leo kama ni mabalozi walihudhuria wamekuja kukamilisha maelezo subiri majibu…
Dunia jana imejua nchi ipo kwenye utawala gani..
Acha kulalamika rekebisha unapokosea…
Maombi yao Mungu aliyapokea ndiyo maana yuko hai na anaendelea kumjambisha m/kiti wa maccmhuyo lisu wako alitandikwa risasi na magufuli hao mabalozi wako walichukua hatua gani?
walaniwe wafuatao wanaochanganya dini na siasa: mzee mbowe, tundu lisu na yule mcanada mzee lemaDini na siasa