Rais Samia na msafara wa Magari zaidi ya 150, tulipe tozo nchi ijiendeshe
Rais wetu namfananisha na Marie Antoinette Mke wa King Lousi wa Ufaransa kabla ya Mapinduzi.

Rais anasisitiza sana tulipe Tozo na kodi ili nchi ijiendeshe yenyewe bila mikopo. Wakati huo huo yeye akiwa ndio mtumaiji mbaya wa hizo pesa na akiwa na matumizi ya anasa, akiwa anatumia Ikulu mbili za Dodoma na Dar es salaam, akiwa na msafara mkubwa kuliko sasa kiongozi yoyote yule Afrika na Duniani.

Ukiangalia huo msafara ni inatisha, huwezi amini kuna shule hazina matundu ya vyoo na tunangoja USAID watujengee.

Gun-boot diplomay!
 
Nimehesabu nimeishia 200 hadi nimechoka.huyu ndiyo atakuwa rais fisadi kuwahi kutokea nchini kwetu.tumerithisha mabalaa.gari Moja Kwa siku linakula mafutata si chini ya milioni na nusu na zaidi na magari Yako zaidi ya miambili halafu anaenda kuzindua kidaraja Cha milioni mia nne ambacho kinalingana na gharama ya mafuta tu anayotumia Kwa siku.Nchi inachezewa sana
 
Rais wetu namfananisha na Marie Antoinette Mke wa King Lousi wa Ufaransa kabla ya Mapinduzi.

Rais anasisitiza sana tulipe Tozo na kodi ili nchi ijiendeshe yenyewe bila mikopo. Wakati huo huo yeye akiwa ndio mtumaiji mbaya wa hizo pesa na akiwa na matumizi ya anasa, akiwa anatumia Ikulu mbili za Dodoma na Dar es salaam, akiwa na msafara mkubwa kuliko sasa kiongozi yoyote yule Afrika na Duniani.

Ukiangalia huo msafara ni inatisha, huwezi amini kuna shule hazina matundu ya vyoo na tunangoja USAID watujengee.

Yani wewe unawaza kunyakunya tu. Matundu ya choo ya nini? Toka enz na enz tunakunya porini.
 
"Mama Kizimkazi na hapa ipo" anatukosea sana sisi wavuja jasho ,msafara wa gari 152 za nini? Kwenda kuzindua barabara ya 107km unaenda na ujumbe wa zaidi ya watu 600 wote hao unawalipa per diem ya laki 2 kwa siku? Kwenda hadi KATAVI zaidi ya km 1000 kwenda na kurudi km 2000 hapo gharama za wese ni hatari.

Mnatukata mitozo kibao kwenye miamala just imagine unatransfer Tsh 2000 kutoka bank kwenda kwenye simu unakatwa Tsh 2000 yaani ni kichekesho ,huo msafara gari ni LC300 na Mkonga Farasi Mweupe gari expensive sana.
 
Tanganyika kinacho watesa ni Ujinga, kutojitambua na uoga. Siku hayo matatu yakitoweka automatically huo upumbavu wanao fanya hao viongozi utaondoka.

Ila Tanganyika kuna viongozi wa ajabu sana sijapata kuona. Mbaya zaidi hawajali lolote lile ata mpige kelele kiasi gani, ina maana anavyo lalamikiwa kila uchwao haoni wala kusikia? Ni dharau na anaamini hakuna chochote kile mtafanya.
 
Mimi nadhani Wakati mwingine hajui kama anasindikizwa na msafara wa magari mengi! Na huenda Safari zake zinaratibiwa na ikulu yeye anaelekezwa apande gari tu.
Sasa hilo ni kosa la nani? Bora hata iwe anajua maana kama hajui basi hiyo ni hatari zaidi kama kiongozi kutokujua anachokiongoza.
 
Rais wetu namfananisha na Marie Antoinette Mke wa King Lousi wa Ufaransa kabla ya Mapinduzi.

Rais anasisitiza sana tulipe Tozo na kodi ili nchi ijiendeshe yenyewe bila mikopo. Wakati huo huo yeye akiwa ndio mtumaiji mbaya wa hizo pesa na akiwa na matumizi ya anasa, akiwa anatumia Ikulu mbili za Dodoma na Dar es salaam, akiwa na msafara mkubwa kuliko sasa kiongozi yoyote yule Afrika na Duniani.

Ukiangalia huo msafara ni inatisha, huwezi amini kuna shule hazina matundu ya vyoo na tunangoja USAID watujengee.

Hii ichi imejaa wapumbavu sana, shida inaanzia kwenye quality ya elimu tunayopewa Watanzania
 
Back
Top Bottom