Msidhanie watu wote ni wajinga kama nyie msivyo na akili. Kuna mabadiliko ya serikali tangu JPM afe? Hii ni serikali ilele na na wala hakuna uchaguzi mpya uliofanyika. Acheni ubumunda ufisadi huu unawahusu hata watawala wa sasa.
View attachment 2187985
Usiishi katika uwendawazimu.
Kwenye uongozi wa nchi, kinachoongoza ni katiba. Kama katiba inasema kwamba mabadiliko ya Serikali yanaweza kufanyika kwa njia mbili au tatu, basi utambue kuwa zote hizo ni serikali halali na ni tofauti, japo upatikanaji wake unakuwa kwa njia tofauti kwa kuzingatia katiba inavyoelekeza.
Unaishi kwa kukariri kuwa Serikali itapatikana kwa njia ya uchaguzi tu. Ndiyo upeo wako ulipoishia.
Mathalani katiba yetu inatamka wazi kuwa Rais anaweza kupatikana kwa njia 4 tofauti:
1) uchaguzi mkuu
2) Rais ambaye yupo kwenye madaraka akifariki
3) Rais ambaye yupo madarakani akawa mgonjwa kwa kiwango ambacho hakimwezeshi kutimiza wajibu wake kama Rais
4) Rais ambaye yupo madarakani akiondolewa na Bunge kwa kufuata utaratibu ambao katiba imeelekeza.
Na kwenye mazingira hayo, Rais mpya atakayepatikana, kwa kuzingatia maelekezo ya katiba, atakuwa ni Rais halali, mwenye mamlaka kamili,na mwenye uwezo wa kuunda Serikali yake kwa kuzingatia katiba. Hakuna Rais anayerithi Urais wa aliyeondolewa.
Kosa pekee alilolifanya Samia, nadhani ni kutokana na woga ambao haukuwa halisia, ni kutomteua Waziri Mkuu Mpya ili Serikali nzima, hata kwa wasio na uelewa, ionekane ni Serikali mpya.
Katiba inaelekeza ni namna gani Serikali ya Rais mmoja inavyoweza kukoma: muda wa miaka 5 kumalizika, kifo, kuondolewa na Bunge na maradhi ya kumzyia Rais kutimiza wajibu wake. Serikali ya Magufuli ilikoma kwa kifo chake. Hajafa akauacha Urais wake ukiishi.
Msipate taabu uchafu wa Serikaki ya marehemu unapofunuliwa. Aliufunika kwa udikteta, utaendelea kuwekwa wazi, na kuna siku atatangazwa rasmi kama mtawala dhalimu aliyewahi kuongoza nchi kwa ukatili,bila weledi, matumizi mabaya ya fedha za umma, kuwapora watu mali zao, upendeleo, n.k.
Zoeeni kwa haya machache yanavyofunuliwa ili yatakapoanikwa yote msife kihoro, na kujilaumu kwa nini mlimwamini sana mtu ambaye alitenda uovu mwingi.
Baadhi ya waliopo Serikalini sasa, nakubaliana nawe, kuwa nao ni sehemu ya uovu, na hawana haki ya kukwepa lawama japo tunajua wengine waliutumikia uovu wa marehemu kutokana na unafiki na uoga maana dikteta angeweza kukufanya chochote kama ungeenda kinyume naye.