Ripoti hii ya CAG asilimia kubwa ni ya enzi ya utawala wa Jiwe, ulijaa upigaji
Na hiyo awamu ya tano makamu wa rais alikuwa nani ,waziri mkuu alikuwa nani ,waziri wa fedha alikuwa nani?

Zito ana tatizo kubwa sana
Ile ilikuwa one man show jamaa yangu. Sio vp, pm wala mof, hakuna aliyeachiwa nafasi ya kupumua.
 
Sukuma gang haya yote mmeyataka wenyewe Nyie sukuma gang mmekazana kumshangilia Ndugai Sasa mliposhikwa hamchomoki Tena hata list yenu ña madhambi yenu vipo wazi Kuna wenzenu wapi madaraka I awamu hii ya sita nao wataumbuka tu
 
Humphrey Polepole alikuwa akijinasibu kwamba eti anajua kufundisha uongozi.

Huyu ndiye alikuwa mshauri mkuu wa JPM, lakini pembeni tu mwa Ofisi yake alipigana vikumbo na makonda.

Pale Arusha alipishana na Mrisho Gambo, Hai, Sabaya, pale Kuna Waziri wa mambo ya ndani aliyekuwa anakata mauno kuliko wote, Mbeya Kuna chalamila alikuwa anachapa viboko wanafunzi. Ally Happy akitukana wastaafu na kuingilia shughuli za mahakama.

Sasa kuna ufisadi wa awamu ya tano,kama ni mwalimu wa uongozi, mbona hawa walikuwa chini yake wakamshinda? .

Au ndiyo yale ya kiafrika, ya kutopiga kelele wakati wa kula?
 
Tuanze sasa kunadi ripoti ya CAG wa awamu hii mbele ya wananchi kwa njia ya mikutano ya hadhara..
Mbona umekomalia mikutano ya hadhara? Si mliipiga marufuku.

Usiwapangie watu namna ya kufikisha habari kwa jamii.

Wao wameamua kutumia njia hiyo, wewe itisha hiyo mikutano uwaambie kuwa si kweli.

Kumbuka, namba hazidanganyi.
 
Aliyefariki ni Magufuli tu. Wengine wote wako hai na ndiyo wanaendeleza kilichofanyika, hivyo huwezi kutenganishwa ufisadi wa mwaka juzi na utawala uliopo.
Hiyo ilikuwa serikali ya mtu mmoja, hata yeye aliita "serikali ya magufuli" hiki kikombe akinywe mwenyewe
 
Kwa sasa kila awaye na ghadhabu na JPM lolote lile baya akikutana nalo humsingizia Hayati Magufuli.

Tupo wengi wenye chuki/husda/hasira na JPM na hii ni kwa sababu ALITUVUNJIA NYUMBA ZETU,ALITUFUKUZA WAFANYAKAZI TULIOKUWA HATUNA SIFA na ALITUZIBIA MIANYA FULANI; Pengine.

Sasa hofu yangu ni muda wa kuendelea kumsingizia unakaribia kukoma na haupo mbali.

Ripoti ijayo ya CAG kwa mfano sioni ni kwa namna ipi ikija na mapungufu atasingiziwa Hayati!

Upigaji wa 2022 na kuendelea sioni ni kwa namna ipi atasingiziwa Hayati!

Hasara ya ATCL na Mashirika ya Umma ijayo sioni ni kwa namna ipi atasingiziwa Hayati!

Hakika nauona mwisho wa kumsingizia Hayati Magufuli ukija kwa kasi na binafsi nausubiri mwisho huo kwa hamu.
 
Sasa hivi watu hawapigwi marisasi, hawatekani kwenye Noah, magazeti yanafunguliwa, wafanyabiashara hawafichi fedha majumbani kuogopa sabaya na genge lake wasi freeze account, TRA hawabambiki Kodi, bunge live limerudi.

Sasa nani ahangaike kumsingizia?
 
Kwa sasa kila awaye na ghadhabu na JPM lolote lile baya akikutana nalo humsingizia Hayati Magufuli.

Tupo wengi wenye chuki/husda/hasira na JPM na hii ni kwa sababu ALITUVUNJIA NYUMBA ZETU,ALITUFUKUZA WAFANYAKAZI TULIOKUWA HATUNA SIFA na ALITUZIBIA MIANYA FULANI; Pengine...
Fact

Ni suala la mda tu
 
Huyu ndiye alikuwa Katibu Mkuu wizara ya fedha. Aitwe atoe maelezo, kama vipi aelekezwe kisutu Kisha segere matata
 
Hata Mimi hili naliwaza sana hili muda unakwenda kasi sana na kichaka cha kufichia udhaifu kinafyekwa.
 
Sasa hivi watu hawapigwi marisasi, hawatekani kwenye Noah, magazeti yanafunguliwa, wafanyabiashara hawafichi fedha majumbani kuogopa sabaya na genge lake wasi freeze account, TRA hawabambiki Kodi, bunge live limerudi.

Sasa nani ahangaike kumsingizia?
Tusubiri report ya CAG ijayo natamani kuona utaandika nini.
Mungu atujalie uzima
 
Back
Top Bottom