Kwa hiyo mama anataka kusema nini?
Yaani kwa mfano Lissu angepigwa lisasi tatu tu na kufariki hapo ndio tungehitimisha kuwa hao waliompiga Lissu ni askari wa serikali ya CCM!
Hiyo ni akili ya uwendawazimu.
Hivi huyo mama anajua kuwa waliomuua Rais Abeid Karume kule Zanzibar walikuwa ni askari wa serikali ya CCM na walimimina zaidi ya risasi kumi mwilini mwake?
Hivi huyo mama anajua kuwa waliomuua aliyekuwa mkuu wa idara ya usalama wa taifa, Imrani Kombe kule Kilimanjaro walikuwa ni askari wa serikali ya CCM na walimimina zaidi ya risasi tatu mwilini mwake?
Mama anapaswa kutuambia kwa nini mpaka leo hii wahusika wa tukio lile la kutaka kumuua Lissu hawajatafutwa, kutajwa, kukamatwa na kushtakiwa na serikali?
Kama mama Samia anawajua wahusika wa tukio lile la shambulizi dhidi ya Lissu basi awataje, na kama hawajui (ama anaogopa kuwataja) ni vyema akakaa kimya, kuliko kuchokonoa mzinga wa nyuki.
Ni bora hata mama Samia angetuambia basi kwa uchache ni akina nani walimlisha sumu Mzee Mangula akiwa ndani ya ofisi kuu za CCM kiasi cha kuponea chupu chupu kupoteza maisha.
Mwisho napenda kumwambia mama Samia anapaswa kufahamu tu, kikulacho kiko nguoni mwako, asitukane mamba kabla ya kuvuka mto, kilichompata Lissu huenda kitakuja au kingeweza kumpata mtu mwingine yoyote katika Tanzania hii ya sasa.
Yote kwa yote, mama Samia anapaswa kujua Karma ipo, na ipo siku itajibu mapigo. Namkumbusha tu Dr. Omar Ali Juma alifariki ghafla kwa mshtuko wa moyo (Cardiac arrest) mwaka 2001 akiwa makamu wa rais wa Mkapa, ambapo miaka 19 baadaye Mkapa naye alifariki ghafla kwa mshtuko wa moyo (Cardiac arrest). Wote hao wanahusishwa na vifo vya wazanzibar kwenye maandamano ya mwaka 2001.