Uchaguzi 2020 Samia Suluhu Hassan: Askari wa Serikali ya CCM akipiga mtu risasi 3 akamkosa atawajibika

Ulitaka waanze kumuhoji na kampeni hizi si atalalamika! Halafu usitumie tuli mi sihusiki wewe acha kuwa na akili mgando..
Matukio mengine yanahitaji muda.. tunajadili hatima ukifata process hutaelewa kamwe.
Kumbe na wewe huwa unatetea unyama ???
 
Maza umeongea upuuzi wa kiwango cha juu sana.kwa kipindi chote hicho umekaa kimya leo umewashwa na nini sasa?achana na mipasho isiyokuwa na ulazima ili uendelee kuheshimiwa.
 
Hebu tujiulize yaliyofuata baada ya shambulizi lile
 
Nayaheshimu Sana maandiko, Ila nusingeweza kukaa kimya na kuvumilia, hata baada ya wewe kuniita sherwani🤔!
Ninachokiona hapa Ni kwamba, unajaribu kutusi watu huku ukijificha kwenye mrengo wa maandiko matakatifu, kitu ambacho sio kizuri kabisa🙏
 
Nan kakwambia shule kila mmoja inamtoa ujinga?wengne wamezidi kuwa mazumbukuku
 
Dr omary alilishwa Sumu baada ya taarifa kuvuja kuwa anajiaandaa kuvunja muungano awe Rais wa Zanzibar huru isiyo koloni la Tanganyika hata mkapa zipo tetesi kuwa nae kifo chake kina utata kutokana na yeye kuwa alikuwa amekasirika akataka kuanika ukweli juu ya mikataba ya madini
 
Hebu tujiulize yaliyofuata baada ya shambulizi lile
Hiyo bado haitoshi kumattack Magufuli moja kwa moja.Tambua kwamba Tz tuna mihimili mitatu, binge Ni mihimili unaojitegemea, kwa mujibu wa katiba.
 
Huu ndio ukweli hakuna askari mwenye mafunzo apige risasi kumi na sita akose hahahah chadema ndio walumpiga risasi lissu kisa Urais! Lissu amepigwa na watu wa chadema
Alafu watu wa Chadema ndo walizuia pia Lissu kulipiwa matibabu na serikali????

Watu wa Chadema ndo walizuia Lissu kuchangiwa damu?????

Watu wa Chadema ndo walizuia watu kuvaa tshirt za pray for Lissu na kumfanyia maombi viwanja vya sinza pale?????

Watu wa Chadema ndo walienda mbali zaidi hadi kumvua Lissu Ubunge?????

Watu wa Chadema ndo hadi leo hawajamuhoji yeyote yule juu ya tulio laLissu kupigwa risasi????

Watu wa Chadema ndio walioenda eneo la tukio na kutoa CCTV camera zote????

CCM kweli damu ya Lissu inawatesa sana!!! Hadi mnatia huruma!!
 
Lissu itakuwa alipigwa risasi na Wadeni wake au alikua anachukua wake za watu, ndiyo hayo matatizo kajisababishia!!
Ni kweli alipigwa na wadeni na wale alikwachukulia wake zao. Walimfuatilia muda mrefu hadi aliwatolea taarifa polisi, wakamfuata hadi Dodoma, wakaondoa ulinzi area C, wakammiminia risasi, wakang'oa CCTV camera, wakazuia asichangiwe damu, wakazuia albadri zisisomwe, wakazuia malipo yake ya matibabu, wakazuia polisi wasifanye uchunguzi wowote, wakazuia mzuia Ndungai asijua mbuge wake yuko wapi. Huyo mke Ni mke wa aina gani? First Lady? Hapana! Huyu mama anajihesimu. Makamu wa Rais? Hapana! Huyu Ni muadilifu! Ni nani Sasa huyo?
Kama Ni mdeni, Lisu anafanya biashara gani? Ni wakili, Ndiyo Ni wakili. Inamaana ameshindwa kutekeleza jukumu la uwakili, Kuna mteja kashindwa kesi Sasa ameamua kufanya haya yote kushirikiana na kamanda anyepanga walinzi, akamtuma house boy wa Kalemani anyofoe camera, akamshawishi spika amvue Lisu ubunge? Huyo mteja anakesi gani? Ya madai au jinai? Tumuachie Mungu, yeye anajua kwanini alimponya, kwanini ameteuliwa kuwa Mgombea urais, yeye anajua kwanini watu wanavutiwa na ujio wake na kumiminika kwa wingi katika mikutano yake, Mungu anajua kwanini dunia imemulika macho yao kwa uchaguzi huu, Mungu anajua kwanini kaka wa Taifa wa Lupaso ametangulia mbele ya haki, Mungu anajua kilakitu kuhusu uchaguzi huu, tumpe muda.
 
Haya co maneno yangu kama unayataka yapo ktk suratinnaasi, ukiona binaadamu yoyote anashabikia lile jaribio la mauaji kwa namna yoyote ile ujue huyo hana tofauti na shetani
 
Kumbe na wewe huwa unatetea unyama ???
Kuwa muelewa sisemi natetea lissu kupigwa risasi ila naona Kuna utofauti serikali kuhusika moja kwa moja kwenye tukio lake.. ukiangalia anaehusishwa zaidi ni rais Tena ambae anawatu wenye weledi mpana wanaoweza kufanya tukio timilifu zaidi ya kile kilichowaunganisha!.. tukio la lissu ni tata Sana na ndio maana hata serikali hawataki kukurupuka hovyo maana linaweza tumika kisiasa!.. tanua ubongo wewe usikariri..
 
Tusaidie kuwaambia maana watufanya Sisi mapoyoyo
 
Tundu alishambuliwa na hao aliowatuhumu na sasa analindwa na mungu pamoja na malaika
 
Usisahau kama kuna Mungu
 
Mlitaka afe kwa risasi zenu kwa sababu Mungu ni mkuu kamponya kuwaonyesha Mungu ni mkubwa kuliko madaraka yenu.

Nyoyo zenu zimejaa Sonona kwa Mungu kuwaumbua na huo unyama wenu, miili yenu mizima lakini nyoyo zenu zimekufa kwa kujitwisha Uungu wa kutoa uhai wa wenzenu.

Mnachopaswa kutambua Mungu ni mwema sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…