Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Polisi Nyamongo wameshambulia msafara wetu kwa mabomu ya machozi wakizuia njia kuelekea kwenye mkutano wetu wa kampeni

Nadhani baada ya Lissu kuwasifia kwa kazi nzuri mkuu kampigia simu igp na kumfokea na kumuuliza siro.... "hayo mabomu tumewanunulia ya nini" mbona sioni mkiwapiga mabomu chadema?
 
What a load of nonsense, kuendelea kumchekea Lissu ni ku entertain his fantasy; yaani azuie shughuli za watu wengine barabarani kisa tu kichwani kwake anajiona ni sawa na raisi.

This joke has gone too far.
Kwa muda mrefu watanzania tulikua tunasema
We can't breathe
Lakini Sasa jiwe ndo linasema
I can't breathe
 
Mmheshimiwa, kama hufuati ratiba, jee polisi wafanye nini? na ratiba ni ya nini? kwa nini tunakuwa na ratiba? ajitahidi kufuata ratiba mikoa mingine.

Kuna sehemu akikutana na askari ambae anafahamu sheria atakwama.
Unasahau JPM alifanya mkutano eneo ambalo Lisu alikuwepo..!? Polisi na tume walifanya nini!?
 
Ukisikia uhuni na ujinga ndio huu!
Sirro huyu RPC mpuuzi mchukulie hatua!
Angalia kamanda usifuate ujinga na ulimbukeni wa mtu huyu polepole!
 
Naeapongeza jeshi la polisi kwa kurndelea kuwadhibiti magaidi wa chadema
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime Rorya William Mkonda amesema wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakishambulia askari Polisi kwa mawe baada ya kukatazwa kufanya mkutano katika eneo ambalo halipo kwenye ratiba ya CHADEMA kwa leo. tatizo la Chadema wanadhani hao wavuta bangi wao ndo watawapeleka Ikulu na hao viongozi wao ni wataalam sana wa kuongea uongo, jambo linatokea hawawezi kutoa ufafanuzi ni kwa nini imekuwa hivyo bali wanapotosha umma tena mbaya zaidi wanaungwa mkono na huyo Askofu wao uchwara Emmaus Mwamakule.
 
Mgombea wa CCM siku zote anaahidi balaa
Amewaambia wakuu wa polisi watakae shindwa kumdhibiti lissu watafukuzwa Kazi
Lissu anaahidi neema ya kupandisha mishahara na vyeo
Sera mbili tofauti
 
Kuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha mashambulizi?
Agizo toka juu linapokelewa bila kufikiria adhari zake kwa sababu polisi hawana akili zao za kuongezea ili waepushe dhoruba watakayopata maelfu ya hao wananchi wakiwageukia na kuwashambulia. Polisi wasivyo na akili wanaamini silaha walizonazo zilizonunuliwa kwa kodi za hao wananchi zitawalinda dhidi ya Raia wenye hasira huku majeshi na silaha za kivita nchi nyingine yalishindwa kuwathibiti raia wenye hasira ilibidi watoa maagizo huko juu wakimbie nchi zao na mapambano hayajaisha hadi leo. Nyuki ni wadudu wadogo sana lakini wakikasirika hakuna salia Mtume!
 
Tundu kaanza kupinga uonevu wa makampuni ya wachimbaji na Serikali kwa wananchi kabla ya kuwa Mbunge. Hayo mengine mnamsingizia tu
 
Camera does not lie
Katika huu uzi angalia ile video yule kamanda uchwara anapewa somo na lissu
Tunashukuru technology wakati mkapa anaua wapemba alikua anatumia maneno hayo kwa Sasa no where to hide
Kwa muda mrefu wataanza tulikua tunasema
We can't breathe
Lakini Sasa jiwe ndo linasema
I can't breathe
 
Kabaki ameachama mdomo wazi. Hizi kazi za upolisi bwana unaambulia aibu aliyekutuma amelala nyumbani
 
Mkuu umeongea nini hapa, Kama rais anataka kubaki ofisin Basi asigombee,ila elewa mpaka Sasa Kama mgombea yuko sawa na wagombea wengine ,msitishe watu, yupo alie na yupo kweli mtakipata mtakacho
Kama yupo sawa na wengine kwenye uchaguzi kwanini aitwe ‘incumbent president’?

Raisi wa nchi atabaki kuwa ivyo na ata anapomaliza muda wake kuna taratibu za kubadilishana madaraka. Dr Shein bado ukienda Zanzibar security ritual zake zipo pale pale ina maana kule bunge alijavunjwa.

As far as security planning is concerned it’s way cheaper raisi kusimama barabarani kuliko kufanya mikutano mikubwa kila mara he uses a lot security of resources kwenye mikutano mikubwa both capital and human.

Lissu yeye sio raisi ni raia tu acheni kumuongea he is Magufuli equal.
 
Hakuna siku hata moja toka mbinguni polisi wa Tanzania wana kosa sababu.. Wanasahau teknologia haidanganyi. Kwanini mrushiwe mawe??
 
Tundu kaanza kupinga uonevu wa makampuni ya wachimbaji na Serikali kwa wananchi kabla ya kuwa Mbunge. Hayo mengine mnamsingizia tu
Tunafahamu sana huo ndio ulikuwa msimamo wake - kupinga KILA KITU - na huo ulikuwa ni mkakati wa muda mrefu tangu akiwa LEAT. Hayo aliyokuwa akipinga yametekelezwa na seriklai ya AWAMU YA TANO! Sasa bado anapinga nini au anataka haya mazuri, ambayo kwake ni mabaya, yawanufaishe mabeberu waliomtuma sasa?
 
Kwa muda mrefu watanzania tulikua tunasema
We can't breathe
Lakini Sasa jiwe ndo linasema
I can't breathe
Magufuli ndio kwanza katoka kwenye mapumziko leo ndio anaendelea na campaign.

Anaeangaika kila kukicha Lissu hana jumatatu wala jumapili kutwa barabarani na kulialia Magufuli sijui kafanya hivi, CCM imefanya vile; badala ya kunadi sera za chama chake.

Sasa hapo nani asielala vizuri? Nikusaidie tu jibu Tundu Lissu wala sio CDM wote maana wengine washamchoka wamemwachia huo mziki wa Magufuli pekee yake kama anadhani anaweza ucheza.

Keshajua kazi ya Magufuli imetukuka sasa hivi anakimbilia kwenye kutunga uongo na character assassination kwa ivyo kama kuna mtu kupumua shida basi ni Lissu.
 
Kweli, siyo untouchable. Na wa CCM siyo untouchable. Watendewe sawa. Hiyo ni haki yao wote, siyo hisani
 
INASIKITISHA SANA !!!

Ulimwengu mzima wataona viongozi wetu ni watu wa ajabu sana. Yaani mtu anayegombea urais anapigwa mabomu ya machozi akiwa anaelekea kwenye viwanja vya mkutano? Watu wote duniani watajiuliza:- Kama mgombea urais anaweza kupigwa mabomu kirahisi hivyo, watu wa kawaida kama mimi na wewe watakuwa wanateswaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…