Wewe ndiye ungeacha wenye akili Timamu na wanaojitambua wajadili hoja
Wewe nakusamehe na kukuouuza maana hujui unenalo. Lakini ujie kuwa uhai wa binadamu ni zaidi ya kelele za uchawa. Uhai wa mtu siyo wa kuwekea uchawa.

Tutofautiane kwa mambo mengine lakini siyo kwenye umuhimu wa thamani ya uhai wa mwanadamu. Ukipuuza na kuona uhai wa wanadamu si chochote, kuna siku utaoneshwa kwa namna ambayo itaamsha akili na dhamira yako iliyolala ili upate hekima. Usifanyie mzaha maisha ya mwanadamu. Mungu aliyetupatia uhai, akaupa heshima na thamani ya pekee, hadhihakiwi katika kile alichotujalia.
 

Mwambie mtu wako aweke ushahidi na siyo kuongea vitu na kuleta taharuki bila ushahidi wa aina yoyote ile
 
Long time bro... Mambo vipi?
 
Mwambie mtu wako aweke ushahidi na siyo kuongea vitu na kuleta taharuki bila ushahidi wa aina yoyote ile
Ni lini Lisu aliwahi kushindwa kupeleka ushahidi?

Fuatilia Lisu aliwahi kushtakiwa mara ngapi, na mara ngapi alitiwa hatiani? Unadhani ni kwa nini?

Lisu hajawahi kutoa kitu chochote public bila uhakika wa ushahidi. Hapa tayari amevituhumu vyombo vya dola, wamwite wamhoji, uone kama atakosa ushahidi.
 
Lisu angetulia zake tu km Mzee wa ubwabwa asije acha mke mjanee ,maana Hali ilivyo c poaa
 
Wa kupuuzwa huyo!
 
Duh.... So Tundu Lissu ni shetani, Hana rafiki CHADEMA wala CCM?
Unajua hiki alichokiandika Lissu haraka sana mimi nilikijua kwamba kitatokea, unaambiwa mbwa ukimjua jina hakung'ati.

CCM iko transparent mno kwenye mambo ya Utekaji na mauaji, ila kwa kukosa maarifa wao wanadhani wamejificha!

Huwezi kuwa na nchi inayowaza kuua tu raia wake halafu ikaendelea
 
Inaumiza sana.. Wanafanya hivi baada ya mbingu zote kushindikana
 
Katika andiko lake hilo la X ameweka ushahidi wa tuhuma zake? Unaweza kusaidia kuweka hapa jukwaani? Alisema kwenye chama chake yameingizwa manilioni ya rushwa je amewahi kuthibitisha tuhuma hizo? Je unaweza kutuwekea hapa majina ya hao watoa na wapokea rushwa wa CHADEMA? Yeye kama makamu Mwenyekiti alishughulikia vipi masuala hayo? Lissu alisema kuwa alitaka kuhongwa mapesa na mtoto wa Rais je amewahi kuweka ushahidi wa hata CCTV camera? Unaweza kutusaidia kuweka hapa?
 
Mwee! Nini tatizo tumwombee kwa Mungu apone haraka
Yaani unataka watu wamwombee Mafwele apone? Ili azidi kuwamaliza wengine? Labda kwanza atubu na kuahidi kuapa kutorudia ushetani wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…